Oktoba 28 ni mashindano kati ya Ukweli na Ubatili. Wanaojielewa, kujitambua na kutaka maendeleo ya kweli, watachagua ukweli. Wewe upo kundi gani?

Mkuu Invigilator , huu ndio uzuri wa demokrasia, rukhsa kumchagua yoyote, hivyo kuchagua ubatili pia ni haki yako ya kidemokrasia.
P
Mkuu Paschal wewe ni mwandishi wa habari uliyekuwa unajielewa na mwenye akili bora naweza kusema kusema kuliko yeyote nchi hii ,huwa nakaa na watu nawaonyesha maswali yako critical siku ile ikulu,nashindwa kuamini kama ni wewe huyu unayeandika haya sasa hizi,nini kimekuondolea ufahamu kiasi hicho?ni kikao cha Dodoma?.

Hivi kweli;
1.Katiba mpya ni ubatili?
2: Increment na promotion kwa wafanyakazi ni ubatili?
3:Ajira ni ubatili?
4:Haki leo ni ubatili?.

Uvunjanji wa katiba,madaraja,mauaji na ukatili ndiyo hekima!
 
Kwa sasa, kwa nchi yetu Tanzania, the top boss ni rais wa JMT, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, katika kampeni zake, rais Magufuli ameomba, ili kutuletea maendeleo ya kweli, rais Magufuli ameomba tumchagulie rais, wabunge na madiwani kutoka Chama Cha Mapinduzi, CCM, mkichagua upinzani, mtakuwa mmechagua ubatili, sahauni maendeleo!.

Mna jiamini sana CCM ,ndio maana Watu wanadai Uhuru wao na Haki zao.Kodi zina kusanywa bila upendeleo lakini kutawanywa kunakuwa na Upendeleo wa wazi kabisa.
 
Mimi nitamchagua Lissu ili vitendo vya kuteka watu,watu kupotea,,kubambikia watu kesi viishe.

Nitamchagua Lissu kwa sababu ya demokrasia,haki na uhuru wa habari.

Nitamchagua Lissu kwa sababu sitaki kuwa sehemu ya watenda dhambi,Siku Mungu akiniuliza nitamjibu sikuwachagua wauaji,watekaji,wabambikia watu kesi nk.

Kwa kifupi nina sababu bilioni moja za kumchagua Tundu Lissu.
 
Vipi kile kiapo chako kwamba Chadema kimekufa umekitengua? Nilikudharau kwa porojo hizo zilizokudhalilisha kwa kudhani unaweza kufikiri kwa niaba ya Watanzania
Mkuu Molemo , ni lini niliwahi kuleta kiapo chochote humu jukwaani?. Ila pia kwani CHADEMA bado iko hai?. Kilichomo ni Tundu Lissu ndie anashabikiwa na sio CHADEMA as chama, jee unamjua aliyemshauri Lissu agombee urais ni nani?. Angalia tarehe ya bandiko hili
Uchaguzi 2020 - Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha uwezo zaidi ya Magufuli!

P
 
Wanabodi,

Hili ni bandiko la swali, kuhusu uchaguzi wa mwaka huu ambao ni mashindano kati ya ukweli vs ubatili, Je, wewe utachagua nini? Utachagua ukweli au ubatili? The choice is yours!

Declaration of Interest
Japo mimi Pascal Mayalla ni kada wa Chama Cha Mapinduzi, CCM ila mimi ni Kada Mzalendo ambae ninatanguliza mbele maslahi ya taifa kwa kuwa mkweli daima, na siku zote huwa nausema ukweli halisi jinsi ukweli huo jinsi ulivyo, bila kujali ukweli huo kama ni ukweli wa haki, ni mchungu vipi au unauma vipi, as long as ni ukweli nitausema.

Sisi Watanzania tuko watu wa aina mbili:
1. Kundi la kwanza ni la Watanzania Wakweli, the realists wanaoukubali ukweli halisi jinsi ile ulivyo, hawa ni watu walio jitambua na wanao jielewa hivyo tarehe 28, October, watachagua ukweli.

2. Kundi la pili, ni kundi la ubatili, hawa ni wishful thinkers and day dreamers, hawa ni Watanzania wenzetu, wasiojielewa na wasio jitambua ambao wanaishi kwenye Tanzania ya kusadikika, utopian society, hawa tarehe 28 October, watachagua ubatili.

Je, wewe uko kundi gani?Je, uko kundi la ukweli au ubatili? Tarehe 28 October, utachagua kweli au utachagua ubatili?

Maendeleo ya Kweli vs Ubatili
Tanzania tulitawaliwa wakoloni Wajerumani kisha Waingereza, walituachia baadhi ya misemo ya kizungu ambayo ni ya ukweli mtupi japo ukweli mwingine ni ukweli mchungu kumeza lakini ndio ukweli wenyewe halisi!.

Moja ya misemo hii ya wazungu, ni msemo huu " The Boss is Always Right" yaani anachosema mkubwa, ndicho kitu cha ukweli, mkubwa huwa hakosei, na hata akikosea, kosa hilo hugeuka ndio kitu sahihi na ndio ukweli wenyewe!.

Kwa sasa, kwa nchi yetu Tanzania, the top boss ni rais wa JMT, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, katika kampeni zake, rais Magufuli ameomba, ili kutuletea maendeleo ya kweli, rais Magufuli ameomba tumchagulie rais, wabunge na madiwani kutoka Chama Cha Mapinduzi, CCM, mkichagua upinzani, mtakuwa mmechagua ubatili, sahauni maendeleo!.

Kauli hiyo ndio ukweli wenyewe halisi uliopo kwenye uchaguzi huu, kama wewe ni Mtanzania, ni mkweli, ni mtu anaejitambua na unaejielewa na then tarehe 28 October, utachagua ukweli.

NB: Ukweli sio lazima uwe the right thing, yaani ukweli halisi sio lazima uwe ni wa haki, hata kama ukweli huo sio ukweli wa haki, lakini ndio kitu halisi kilichopo. Kauli ya rais Magufuli kuwa usipochagua CCM, hataleta maendeleo, kwa vile maendeleo hayana chama, hivyo kauli hiyo sio kauli ya haki, lakini ndio kauli ya ukweli wenyewe uliopo!

Sasa kama wewe ni mkweli na unachotaka ni maendeleo ya kweli, then ili kuyapata hayo maendeleo, maadam the boss is always right, na the boss ameisha sema tumchagulie nani, ili atuletee maendeleo, then wakweli wote wanajua tarehe 28 October watachagua nini, nani na chama gani!.

Ukweli ni upi?
Ukweli ni kauli ya rais Magufuli, kuwa ili kupata maendeleo, tumchagulie viongozi wa kutoka CCM, mkichagua upinzani, maendeleo utaishia kuyasikia.

Ubatili ni upi?
Baada ya kusikia kuwa usipoichagua CCM hutapatiwa maendeleo, utaishia kuyasikia tuu hayo maendeleo, hii maana yake, ukiamua kuuchagua upinzani, maana yake ni umechagua ubatili. Je, wewe utachagua nini kati ya ukweli na ubatili?

Kwa vile uchaguzi wa mwaka huu ni mashindano kati ya ukweli na ubatili, Watanzania wanaojielewa, kujitambua na kutaka maendeleo ya kweli, Tarehe 28 October, hawa watachagua ukweli, lakini kuna Watanzania wenzetu ambao hawajielewi, na hawajitambui, hawa tarehe 28 October, watachagua ubatili. Je, wewe mwenzangu na mimi, uko kundi gani?

Nakutakia Uchaguzi Mwema.
Paskali

Pascal mayalla nilikuwa nakuheshimu sana,kumbe na wewe ni wale wale
 
Jimbo la KONGWA halijawahi ongozwa na Upinzani toka tupate Uhuru 1961 lakini ni Jimbo duni kuliko duni yenyewe. Je, kwenye hili Magufuli anasemaje?

Ndugu Yangu Paskali acha unafiki na Uongo wa kujipendekeza kwa rais ili tu upate nafasi za Uteuzi !!

NENO la Mungu linasema:
" Mwenye kutawala akisikiliza Uongo; basi watumishi wake wote watakuwa waovu" (Mithali 29: 12)
 
Back
Top Bottom