Oktoba 28 ni mashindano kati ya Reality vs Ahadi Hewa? Je, Watanzania watachagua nini kati ya visible, tangible Deliverables vs The Empty Promises?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,442
113,451
Wanabodi,

Kama kawaida yangu, kila nipatapo fursa, hutoa zile makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa", Watanzania tunajiandaa kwa Uchaguzi Mkuu wa rais, wabunge na madiwani hapo Oktoba 28, Watanzania tunakwenda kuingia kwenye uchaguzi uchaguzi wa 2020 ambao ni uchaguzi wa mashindano kati ya deliverable visible tangibles, ambayo ni maendeleo ya vitu vya ukweli vya kuonekanika ambavyo vimefanyika na kuwa deliverable vs ahadi, promises kuwa ukinichagua mimi nitafanya hiki na kile!. Ahadi ikitolewa usually huwa ni empty promise, ikiisha tekelezwa ndio inakuwa ahadi ya ukweli, a firm commitment.

Hili ni bandiko la swali, hiyo October 28, Je Watanzania watachagua nini kati ya deliverable tangibles za kuonekanika, na empty promises za kuahidiwa, with nothing to show?

Declaration of Interest
Kwa vile JF ni members generated forum, ukitokea kuna jambo unalijua, unalibandika humu ili kushare na wengine. Naomba ku declare interest kuwa mimi ni kada wa Chama Cha Mapinduzi, CCM, na humu tuna makada wengi wa vyama vyote. Enzi zile Prof. Kitila Mkumbo akiwa very active humu alikuwa ni kada wa Chadema. Zitto Kabwe bado yuko very active ni kada wa ACT, hivyo unaweza kuwa kada na bado ukawa mchambuzi objective kwa kusoma hoja zangu na sio kuniangalia ukada wangu.

Kumhusu JPM na Uchaguzi wa 2020, Nilisema Zamani Kuwa
Tarehe 29/10/2015 kuna kitu nilikisema kumhusu JPM na uchaguzi wa 2020!
Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?

Sasa baada ya CCM kutoa majina ya wagombea wake, kuna kitu naomba nikiseme, Je wajua kuwa kupitishwa na vikao vya uteuzi vya CCM ni kazi ngumu kuliko hata uchaguzi wenyewe?. Jee wajua kuwa jina lako likiishapitishwa na CCM, huo tayari ni ushindi tosha?. Ili CCM kupata ushindi wa kishindo, katika uchaguzi huu, hakuhitaji hata kupiga kampeni, kazi aliyoifanya JPM inaonekana wazi kabisa kwa naked eyes, wala huhitaji kuvaa miwani ya uchunguzi ndipo uone, wenye macho wanaona!

Tunakwenda Kuchagua Nini
Watanzania tunakwenda kuingia kwenye uchaguzi huku kuna chama kimoja kinaingia kikiwa na mtaji mkubwa wa vitu ilivyofanya katika utekelezaji wa ilani yake ya uchaguzi iliyokipatia ushindi ile 2015, kikiwa na mtaji wa vitu vya kuonekanika, a strong showcase, huku vyama vingine vikija with nothing to show case, ukitegemea Watanzania watachagua visible deliverable tangible or just empty promises?.

Ushauri wa Bure
Kwavile tunaingia kwenye mashindano kati ya mwenye kitu cha kuonyesha na asiye na kitu cha kuonyesha, ili kuwatendea haki Watanzania waweze kufanya an informed decision hiyo October 28, natoa wito kwa asiyenacho, ili aweze kuchaguliwa, asije tuu na ahadi bali aonyeshe hiki kilichopo sii lolote sii chochote, ningekuwa mimi ningefanya hiki na hiki na hiki.

Mfano mzuri ni kwenye elimu bure, inatolewa toka darasa la kwanza hadi kidato cha 4. Kwa vile wewe ulisema ungekuwa wewe ungetoa elimu bure toka chekechea hadi chuo kikuu, then unaeleza ungeitoaje kwa bajeti gani, ili Watanzania wakuchague wewe.

Uchaguzi Mkuu huu, tushindanishe sera na mikakati ya utekelezaji na sio kushinda kwa kutukana na kubeza kila kilichofanyika bali kueleza namna bora zaidi ya kufanya kuliko hiki kilichofanyika.

Mfano JPM amejenga barabara za juu kwa juu, wewe ukifika, kwavile hizi barabara za juu kwa juu za JPM, unapita juu kisha unashuka chini na kuendelea na safari yako kwenye barabara za kawaida, then wewe ahidi kwamba utajenga barabara za juu kwa juu za moja kwa moja, ukipanda juu, unakwenda juu tuu straight hadi mbinguni kwa Sir God God mwenyewe!.

Tuwe Wakweli, Tuwe na Shukrani
It's good to appreciate kilichopo, kilichofanyika na kueleza wewe ungefanya namna bora zaidi ili Watanzania wakikuchagua, wajue wanakuchagua ili kupata kilicho bora.

By The Way Jimbo la Kawe.
Kabla ya kumalizia, kwavile mimi ni mkazi wa Kawe, Mbunge wetu wa Kawe ni mwanamke, CCM imempitisha mgombea mwanaume kushindana na mwanamke, Kidunia, Kiafrika na kimila, sio vizuri kwa mwanaume kushindana na mwanamke, hivyo kwa vile Mbunge wa Kawe ni mwanamke na hana kizingiti, na kwa vile aliyepitishwa CCM pia ana sifa za ushenga, mimi nashauri kwa jimbo la Kawe, CCM hatuhitaji kabisa kufanya kampeni, kinacho hitajika kwa Kawe ni kuandika tuu barua ya posa na kumtuma mshenga aipeleke, tumpose huyo binti tutakuwa tumemaliza mchezo!.

Hitimisho
Namalizia kwa lile swali la msingi la bandiko hili hiyo October 28, Je Watanzania watachagua nini kati ya deliverable tangibles za kuonekanika, au empty promises za kuahidiwa, with nothing to show?.

Nawatakia Jumatatu Njema.
Paskali
 
We sio mtu huru wa kufanya uchambuzi huru kwahiyo sisi wengine tunakupuuza tu.

No wonder japo wewe ni mwanahabari, siku hizi uko kimya kabisa kuhusu uminywaji wa uhuru wa vyombo vya habar na ni wazi wewe ukipewa uwaziri wa habari, utakandamiza sana media na hata hii JF unaweza kuigeuka

Mtu mwenye akili timamu,alie-civilised hawezi kuwa-influenced na maendeleo ya vitu kiasi cha kupuuza kukosekana kwa utu kunakofanywa au kufumbiwa macho na watawala.

Pia jiulize hayo maendeleo ya vitu, yote ni vipaumbele sahihi na yanafanywa kwa kuzingatia taratibu na sheria za nch?

Kwa kifupi,uko biased kwa malengo yako binafsi na nyinyi ndio aina ya watu ambao Bwana yule anapenda kufanya nao kazi.

Mwisho:Siku ukipewe uteuzi,usisahau kuishukuru JF.
 
Kada mtiifu wa CCM aloambulia kura 1
emoji91.png
emoji91.png
emoji91.png
emoji91.png
 
Ukweli mchungu kwa chadema &Co., Kwanza, Kanda ya Ziwa inaaamua raisi wa Tanzania sababu ya idadi ya watu (Tundu lisu hata Mwanza hakutia mguu alipitiliza, Shy walimpotezea), pili Waislamu hawawezi kuipigia kura chadema na wako wengi ambao wataipigia kura CCM, tatu chadema sababu ya ubinafsi hawawezi kuungana na upinzani wengine, hivyo hata hizo kura kidogo za upinzani zitagawanywa pia, CCM itashinda kwa > 85% kama vile Mzee Mkapa alivyoshinda awamu ya pili.
 
Kwanza nataka kukueleza nilisoma tu kichwa cha habari, sikuwa na muda wa kusoma upuuzi wote.

Ni bora nimchague mtu anayeniahidi mazuri kuliko mtu aliyenifanyia mabaya.

1. Kupotea kwa uhuru wa habari
2. Viongozi kujichukulia sheria mkononi - Makonda alivyovamia Clouds
3. Uwanja wa ndege wa Chato bila idhini ya bunge
4. Wananchi kutekwa na kupotea n.k.
 
Kila mtu atajinadi kwa anayoenda kufanya na siyo yaliyofanyika. Yaliyofanyika hata kama yalikosewa huwezi kuyabomoa tena. Pia hayatasaidia chochote kile kwenye uchaguzi maana ni kazi lazima serikali iliyopo izifanye. Mtu akija na porojo za eti nilifanya au tulifanya nitamuona mjinga wa aina yake.

Pia naomba uelewe kuwa katika uongozi huwa tunaangalia "extra ordinary"
Sasa alichofanya Magufuli ni mambo ya kawaida ambayo hata wewe Mayalla pamoja na njaa zako ukipewa uongozi unayafanya. Kitu cha ajabu sana alichofanya Magufuli ni kuwanyanyasa wasio wanyonge hasa wasomi na wafanya kazi! Hilo kulifanya inakuhitaji uwe na roho Jiwe!

Sasa kama watanzania watamchagua kwa maajabu hayo ya roho jiwe ni wao ila kujenga sijui barabara kwa kufyeka haki za msingi za watumishi na wawekezaji halafu ukajisifia ni jambo la KIPUMBAVU na linafanywa na WAPUMBAVU waliopitiliza!

Halafu siku hizi una hoja za akili ndogo sana mkuu, uccm usikulemaze kiasi hicho.

Halafu pia ulinikera ulivyoandika eti "Wapo watu wenye nia ya kugombea ubunge kwa dhati ya kumsaidia Magufuli"
Naomba nikueleze kuwa kazi ya bunge siyo kumsaidia Magufuli, kazi ya bunge ni kusimamia na kuiongoza serikali iliyopo madarakani. Kuza akili yako mzee, uccm usikulemaze kiasi hicho!
 
Kaka Pasco hata huyo Magu aliingia kwakutumia empty promises, ndio akafanya au unataka kusema hayo aliyoyafanya Magu aliyafanya akiwa mtu wakawaida na si Rais?

Wacha kujitoa ufahamu bhana, anayo yasema LISSU atuwezi kumuhukumu nayo tukaacha kumchagua eti kisa Ni ahadi tu, wacha tumpe Ikulu tuone atatufanyia nini!
 
Ukweli mchungu kwa chadema &Co., Kanda ya Ziwa inaaamua raisi wa Tanzania sababu ya idadi ya watu (Tundu lisu hata Mwanza hakutia mguu alipitiliza, Shy walimpotezea), pili waislamu hawawezi kuipigia kura chadema na wako wengi ambao wataipigia kura CCM, tatu chadema sababu ya ubinafsi hawawezi kuungana na upinzani wengine, hivyo kura za upinzani zitagawanywa, CCM itashinda kwa > 85% kama vile Mzee Mkapa alivyoshinda awamu ya Pili, ...
Mataga mtataga tu mwaka huu hiyo kanda ya ziwa unayoisema haitampa lissu unamaanisha mwanza pekeyake wewe mjinga kweli sasas kwa taarifa lissu anakura nyingi kanda ya ziwa kuliko mgombea yoyote katika historian ya vyama vingi, na nikipindi hiki lissu atachukia majimbo mengi sana huku kanda ya ziwa labda kama hao kina mayala walowezi was dar es salaam wanawadanganya subirin October
 
Mataga mtataga tu mwaka huu hiyo kanda ya ziwa unayoisema haitampa lissu unamaanisha mwanza pekeyake wewe mjinga kweli sasas kwa taarifa lissu anakura nyingi kanda ya ziwa kuliko mgombea yoyote katika historian ya vyama vingi, na nikipindi hiki lissu atachukia majimbo mengi sana huku kanda ya ziwa labda kama hao kina mayala walowezi was dar es salaam wanawadanganya subirin October

Kanda ya Ziwa wanaenda na mtoto wao piga, ua garagaza, isistoshe hata kura za huruma Kanda ya Ziwa chadema haipati kwa maana Tundu Lisu katumia muda wake mwingi kumtukana na kumdhalilisha mwana wao JPM, hivyo ondoa kichwani na akilini kwako kabisa hilo, kwanza Tundu Lisu hata kwao Singida hatopata kura za kutosha, kura pekee chache Tundu lisu atakazopata ni labda za wanafunzi wa sheria tena siyo wote, huyo jamaa mmejitwisha zigo la mwiba.
 
Ukosefu wa ajira kwa vijana na kashindwa kuboresha maslahi ya wafanyakazi ni moja ya sera zikizoshindwa kutekelezwa kwa awamu hii.

hatujasahau mauaji ya watanzania wenzetu wengine wametekwa na kupigwa,kupotea ,kufungia uhuru wa vyombo vya habari. Hii si aina ya uongozi tunaoutaka Tanzania. Maendeleo hata kikwete alileta kama barabara alijenga za lami,shule za sekondari kila kata nchi hii alikuwa Kikwete,ujenzi wa vyuo vikuu na mengine mengi tu.

Kwahiyo ununuzi wa ndege wa magufuli na ujenzi wa sgr isiwe sababu ya kutandika watu risasi. Wananchi tuamue viongozi tunaowataka .
 
Wanabodi, October 28 ni Mashindano kati ya Reality vs Ahadi Hewa?, Jee Watanzania Watachagua Nini Kati ya Visible Tangible Deliverables vs The Empty Promises?
Wana JF, October 28 ni mashindano kati ya Freedom and Servitude. Je, Watanzania watachagua nini kati ya Liberty vs Bondage, kati ya Democracy vs Authoritarianism, kati ya Love vs Hate

For what shall it profit a man, if he shall gain the whole world, and lose his own soul? ... Matthew 16:26
 
Back
Top Bottom