Environmental Security
Senior Member
- May 21, 2020
- 181
- 261
Kama tunavyofahamu kuwa mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi, na kama ilivyo katika chaguzi zilizopita, hali ya hewa huwa inaanza kujulikana mapema kwa kuzingatia mambo mbalimbali, kwa kuanzia na utekelezaji wa ahadi, kukubalika kwa wagombea, uimara wa chama hadi kufikia kipindi cha uchaguzi ikiwemo pamoja na mambo mengine.
Kama ilivyo kawaida tayari hali katika mitaa, vijiji, kata, wilaya na mikoa, inaonesha kuwa Rais wetu mpendwa ndugu. John Pombe Joseph Magufuli ataashinda kwa idadi kubwa sana ya kura, na hii inatokana na uungwaji mkono mkubwa sana alionao kutoka kwa waTanzania wa kada mbalimbali. Hii ni kutokana na ukweli kwamba kasi yake katika kuleta maendeleo na kushughulikia changamoto mbalimbali za kitaifa hadi za watu binafsi katika ziara zake, lakini pia jinsi ambavyo ameshughulikia janga la corona ambapo amezingatia sana hali ya WaTanzania walio wengi hivyo kuamua kutumia mbinu ambazo zinawezekana na zina matokeo kwa mazingira yetu na maisha yetu, hasa ikizingatiwa kuwa yapo mataifa makubwa ambayo yameumizwa na yameshindwa kudhibiti janga hili pamoja na uwezo wao wa kisayansi na kiteknolojia, amedhihirisha kuwa si kila wakati lazima uendeshe mambo kwakuwa fulani anafanya hivyo - (katika hili nafahamu viongozi wa dini wanauthibitisho wa wazi na ni mashahidi muhimu sana), barabara, vituo vya afya, watalam wa afya, vifaa tiba, reli, elimu bure, mikopo vyuo vikuu, reli, ndege, kukuza uchumi, nidhamu serikalini, kuondoa ufisadi na urasimu, pamoja na hayo yapo mengi sana lakini kwa kadiri siku zanavysonga nitakuwa nakueleza kwa kina kila alichofanya kwa kila eneo, najua wajua lakini napenda kukujuza zaidi ili wote tutembee kifua mbele kwa alichofanya kwa taifa letu kwa kipindi hiki.
Jambo jingine ni jinsi alivyoweza kukiimarisha Chama Cha Mapinduzi kwa nafasi yake ya uenyekiti, (bila kusahau wasaidizi wake katika chama) hivyo wanachama wote kuwa proud na chama chetu, na hivyo wote kwa pamoja kuwa wakwanza kuhakikisha tunampatia kura zetu, kwakuwa sasa chama kinaisimamia serikali katika utekelezaji wa ilani yetu makini, chama kina mapato yakutosha toka katika vyanzo vyake vinavyosimamiwa vizuri, chama kinakubalika na ni chama pekee Tanzania ambacho ni mali ya wananchi, sio mali ya mtu fulani au kundi fulani.
Kingine ni kuwa wapinzani wamekosa kabisa ajenda ya kusimama nayo, wamebaki kudandia matukio na kutoa matamko ambayo ni ya kitambo tu na baadae kudakia jingine, maana kasi ya Chama Cha Mapinduzi kwasasa ni kushughulikia kila changamoto ya wananchi na kuleta maendeleo kwa vitendo, sio kwa bahati mbaya kwamba wapinzani hawana ajenda ni kwasababu kila waliyodhani wataitumia imeshughulikiwa tayari, hadi imefikia wale walio wa kweli na wanaoamini katika maendeleo ya kweli wameamua kuunga mkono juhudi za Rais na serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo.
Ushindi ni halali kabisa kwa Chama Cha Mapinduzi, Rais, wabunge na madiwani maana kazi inaonekana na wananchi wanaona na kuridhika,
Pamoja tunajenga taifa letu.