Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,005
- 9,872
Leo ni Kumbukizi ya Kitaifa ya miaka 21 ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kilichotokea Oktoba 14, 1999 nchini Uingereza alipokuwa anapatiwa matibabu.
Mwalimu Nyerere ni mmoja kati ya waasisi wa Taifa la Tanzania, ambaye alishiriki kikamilifu katika harakati za kulikomboa Taifa kutoka kwa ukoloni wa Waingereza.
Alikuwa Rais wa kwanza wa Tanganyika na aliongoza tangu Taifa lilipopata Uhuru, Desemba 9, 1961 hadi mwaka 1985
Alikuwa muasisi wa falsafa ya Ujamaa na Kujitegemea ambapo aliamini ili Taifa liendelee kunahitajika watu, ardhi, Siasa safi na Uongozi bora.
Endelea kupumzika kwa amani, Mwalimu Nyerere!
===
PIA SOMA
= > Ubalozi wa Marekani wamkumbuka Mwl. Nyerere. Wasema maendeleo ni watu sio vitu

Wakuu Salaam:
Leo October 14 inatimia miaka 21 tangu muasisi wa Taifa hili atutoke duniani.
Yapo mengi ambayo alifanya na kila mmoja ni shahidi katika hili.
Katika uongozi wake alienzi Siasa safi zenye zilizo na amani ndani yake kama msingi wa maendeleo ya watu na vitu.
Wakati kifo chake kimetangazwa, binafsi mimi sikua na uwelewa kuhusu hilo hivyo sijukujua chochote kinachoendelea. Mwaka wa 2000+ ndiyo naelewa sasa.
Kuuliza uliza, kipindi kile tulikua moshi wakati hiyo taarifa imetoka na ilitangazwa usiku.
Lipo unalokumbuka wakati wa Uongozi wa Mwalimu. Ni kipi?
Na pia wakati kifo cha Mwalimu kinatangazwa, Ulikua wapi kipindi kile?
PIA SOMA
= > Ubalozi wa Marekani wamkumbuka Mwl. Nyerere. Wasema maendeleo ni watu sio vitu