Okoa matumizi ya petrol na kuondoa shida za gari zisizotatuliķa kwa kufanya jambo dogo kwenye gari

SABABU ILIYOJIFICHA GARI YAKO KUTUMIA MAFUTA ZAIDI NA MATATIZO MENGINE

Wasiliana na mimi +255788624499 nikusafishie Mass Air Flow (MAF) senso.

Soma zaidi...

Dalili za MAF sensor inahitilafu ni,
1. Engine ni ngumu kuwasha.
2. Engine inazima muda mfupi baada ya kuwaka.
3. Engine inasitasita au kuvuta ikiwa na mzigo au ikiwa imepark bila kuzimwa.
4. Kusitasita na kutetemeka wakati wa kuongeza kasi.
5. Engine inapata "kwikwi"
6. Kuvuma sana ama kutetemeka kwa gari wakati imesimama.
7. Gari kuwa na missi
8. Code za P0100 hadi P0103, P0171, P0172 na P0300 kwenye diagnostic check up.

Inashauriwa kusafisha MAF sensor ya gari lako angalau kila unapobadili Air filter. Lakini kama ukiweza ni vizuri zaidi kuisafisha MAF sensor kila wakati unapoisafisha Air cleaner ya gari lako.

Ikumbukwe kwamba MAF sensor ndiyo inayodetect kiasi cha hewa kinachoingia kwenye engine ya gari lako na kuna sensor Intaken Air Temperature (IAT) yenye kupima nyuzi joto ya hewa inayoingia kwenye engine, hivyo MAF sensor inapokuwa chafu inaweza kupelekea control box (ECU) ikapiga vibaya hesabu ya mafuta na hivyo kupelekea ama gari yako kutumia mafuta mengi kuliko kawaida au gari yako kuchoma hewa nyingi kuliko kawaida.

Kama gari ikichoma mafuta mengi kuliko kawaida(Rich condition) inaweza kupelekea yafuatayo.


1. Gari yako itatumia mafuta mengi na hivyo utaingia gharama kubwa.
2. Mafuta hayataungua yote hivyo utakuwa unachafua mazingira.
3. Kuziba kwa catalytic converter kwa sababu ya mafuta kuendelea kuungua yakiwa katika bomba la moshi. Ikishaziba hutoweza kuendesha gari lako.
4. Kutengenezwa kwa kaboni kwenye valves na pistons
5. Kuisha sehemu mbalimbali za engine yako kwa sababu mafuta yatakuwa yanaosha kuta za cylinders na kudilute oil hivyo kupelekea kuisha kwa bearings na muda mwingine engine yako kufeli.
6. Gari kuwa na nguvu kidogo.
7. Gari kutetemeka ama.kuwa na dalili kama kwikwi ukiendesha
8. Gari kukosa nguvu ukiwasha AC
Na mengine mengi.

Kama gari yako ikichoma hewa nyingi kuliko kawaida(lean condition) inaweza kupelekea yafuatayo.


1. Gari kuwa na nguvu kidogo.
2. Kuzalishwa kwa Nitrogen dioxide kwa sababu ya joto kali na hivyo kuchafua mazingira.
3. Engine knocking ambayo huletwa na detonation na hivyo kufanya engine kupiga sana kelele.
4. Kuharibika kwa parts mbalimbali za gari lako kwa sababu ya kuknock kwa engine.
5. Na mengine mengi.

Hivyo kwa harakaharaka ukiyaangalia yote mawili unaona hakuna jema kwa sababu yote mawili yanaweza kukuharibia engine ya gari lako

Kama utaamua kutumia solution nyingine tofauti na zilizotambulika katika kusafisha MAF sensor yako basi fanya at your own risk. Na itapendeza kama utakuwa na MAF sensor mpya ya akiba pembeni sababu hiyo unayoisafisha inaweza ikafa na gari yako isiwake mpaka uweke MAF sensor nyingine. Pia katika kusafisha huwa tunatumia sprayer. Tunapulizia kwenye heating element ya sensor yako pamoja na kwenye wavu wa housing la sensor yako kama ina wavu.

Pia haishauriwi kabisa kugusa heating element ya MAF sensor. Ni moja kati ya sensors ambazo ni delicate sana. Na kama ikiharibika ni vizuri kununua mpya kuliko used kwa sababu hiyo used huwezi kujua waliihandle vipi wakati ilipokuwa dukani.

Wasiliana na mimi +255788624499 Whatsapp.

Kusafisha ni dakika 5-10

WASILIANA NASI +255788624499 WHATSAPP.

Sababu za MAF sensor kutokufanya kazi mara nyingi ni sababu ya vumbi inayopita kwenye MAF sensor kutokea kwenye air cleaner, kifaa hicho kinaweza hata kuganda vumbi na kuleta hitilafu tofaut ikiwemo gari kutumia mafuta zaidi.

Mafundi wengi hawana ujuzi wala vifaa sahihi vya kusafisha sensor kwani magari ya kisasa yanatumia mfumo wa computer.
Mafundi wengine wanaweza kukwambia fuel pump mbovu ya kubadilisha kumbe bado nzima.
Pia kama umebadilisha plugs na bado gari yako kuwa na dalili zilizotajwa hapo juu, basi inaweza kuwa MAF Sensor ni chafu na inahitaji kusafishwa

Tunasafisha kutumia spray solution maalum ya kusafishia mass air flow sensor.

View attachment 2084462

View attachment 2084463

View attachment 2084464

View attachment 2084465
Nahitaji complete Exhaust ya IST NEW model. ni Hatchback.

yangu wamekula masega.

Tuwasiliane kwa 0759888018 kwa majadiliano zaidi.
 
Back
Top Bottom