OIC - Zanzibar kujiunga kivyakevyake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

OIC - Zanzibar kujiunga kivyakevyake

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwiba, Jan 27, 2009.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Jan 27, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Zanzibar kujiunga na OIC kivyake

  2009-01-27 10:14:33
  Na Mwinyi Sadallah, Zanzibar

  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imetangaza kwamba itaiomba Serikali ya Muungano kuiruhusu Zanzibar kujiunga na Umoja wa Nchi za Kiisalm(OIC) endapo mpango huo utashindwa kufikiwa na Serikali ya Muungano.

  Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Kiongozi, Hamza Hassan Juma alipokuwa akijibu maswali ya wajumbe wa baraza la wawakilishi waliotaka kujua Serikali ina mikakati gani kuhakikisha Zanzibar inakuwa mwanachama wa jumuiya hiyo.

  Alisema kimsingi sula hilo bado linashughulikiwa na Serikali ya Muungano hasa kwa kuzingatia linahusu utaifa ``kwani Zanzibar ni nchi wakati taifa ni moja la Tanzania hivyo tutajiunga kama Nchi ,ndo maana yake.

  Alisema Zanzibar haijuingi katika jumuiya hiyo kwa matakwa ya kidini bali inatetea kuchukua hatua hiyo kutokana na sababu za kiuchumi.

  ``Ikiwa itashindikana kwa Serikali ya Muungano kujiunga, Serikali ya Zanzibar tutaomba tujiunge kwa kujitegemea badala ya kuwa wanachama kama sehemu ya Jamhuri ya Muungano,`` alisema Waziri Hamza.

  Alisema kitendo cha kuchelewa kujiunga katika jumuiya hiyo kunachangia kutochangamsha maendeleo ya Zanzibar kutokana na misaada ya kijamii na kiuchumi inayotolewa na OIC.

  Alitoa mfano kwamba endapo Zanzibar ingekuwa mwanachama ingesaidiwa matrekta 50 kupitia jumuiya hiyo na kusaidia katika sekta ya kilimo Zanzibar ambayo ingewanufaisha wananchi wote bila ya kujali imani zao za dini.
   
  Last edited: Jan 27, 2009
 2. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #2
  Jan 27, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,844
  Likes Received: 1,110
  Trophy Points: 280
  bila shaka itakuwa hivyo
   
 3. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #3
  Jan 27, 2009
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Sasa huyo mkulu anaongea nini wht is matrekta 50kwa Zanzibar???? Na kwa nini viongozi wetu wamejikita zaidi kwenye misaada ya wao kupewa na si kutoa pamoja na umasikini wetu?? Halafu bado eti ndani ya katiba tunasema Tanzania inafuat mfumo a ujamaa na kujitegemea.
   
 4. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #4
  Jan 27, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Yaani Zanzibar haiwezi kujinunulia matrekta 50 mpake ipewe na OIC?
   
 5. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #5
  Jan 27, 2009
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Yea it is ridiculous!!!!!!!!!!!!!!!
   
 6. J

  Jamco_Za JF-Expert Member

  #6
  Jan 27, 2009
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Sioni tabu kujiunga na OIC tatizo ni kwamba hata katiba ya tanzania ambayo zanzibar ni sehemu yake inawakataza kuingia kwenye hiyo jumuhiya kama wao then watawezaje au bado hajaridhika walipoambiwa kuwa zanzibar ni nchi ndani ya tanzania lakini nje ya tanzania zanzibar ni sehemu ya tanzania kama ilivyo mafia.

  Pamoja na kwamba mafia wanahitaji misaada na wenyewe lakini hawawezi kujiunga na OIC kwa kuwa sio nchi
   
 7. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #7
  Jan 27, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Kukaa tu na kupenda tu kupewa Misaada ndo imetufikisha hapa sasa miaka 40 tukiwa huru!
   
 8. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #8
  Jan 27, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Uvivu wa kufikiri na kufanya kazi ndiyo yanayotufanya kila wakati kuongelea kujiunga na OIC au zingine.Tufikirie namna ya kutumia rasilimali tulizonazo ili zitusaidie kwa maendeleo ya Nchi yetu.Tufanye kazi kwa bidii ili tuinue uchumi wa Nchi yetu.
   
 9. Sonara

  Sonara JF-Expert Member

  #9
  Jan 27, 2009
  Joined: Oct 2, 2008
  Messages: 730
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Miak 15 kutokea leo wengi wetu walala hoi tuta lazimika kuhama katika miji ya TZ kwa hiyari au kwa kulazimisha na hali maisha , matajiri ndio watakao hodhi kila kitu hivi sasa tunajionea leo Matajiri wanazidi kumiminika na kumiliki hata zile sehemu za wanyoge wa mungu wanapewa wao wakati familia moja yenye watoto wasiopunguwa wa3 inaishi katika chumba kimoja. Nyumba mojandani yake kuna familia kumi au zaidi,ni unyoge wa mwisho kufanyiwa mtu katika nchi yako .
   
 10. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #10
  Jan 27, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Na hii ina husiana vipi na Zenj kujiunga na OIC?
   
 11. Sonara

  Sonara JF-Expert Member

  #11
  Jan 27, 2009
  Joined: Oct 2, 2008
  Messages: 730
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hapa TUnajadili nchi kwa ujumla na sio zenji tu usiwe kama wale wenye uwezo na kifedha na madaraka wasiojali watu wa kima cha chini wenye kuhangaikia mlo mmoja ikiwa zanzibar au bara kila binadamu anastahiki kupigania haki katika maisha kwani walio vijiji au mijio wasiokuwa na uwezo hawana hisiya ???au ndiounawakejeli dharau haifai katika ulimwengu huu waleo
   
 12. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #12
  Jan 27, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Kuna tatizo gani kufungua thread mpya na ukajadili hayo ya nchi? Kwani hapa issue na mjadala ni Zenj na OIC...
   
 13. M

  Mkandara Verified User

  #13
  Jan 27, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kulingana na hali ya kisiasa nchi nadhani hili litakuwa wazo zuri sana.. Ni bora sana Zenji ijiunge na OIC kivyake kwa sababu wananchi wake ndicho wanachokitaka.. haya maswala la trekta 50 sijui ngapi hayawezi kusaidia mgogoro wa OIC hata kidogo kwani hata sisi bara tumepewa vyandarua na Bush ktk kuzuia Maleria..Kwa mwenye kufikiria ule ulikuwa uchuro mkubwa!
  Na kibaya zaidi hadi leo fungu kubwa la msaada aliotuahidi kutupa haukupitishwa na bunge lao hadi kaondoka madarakani...
   
 14. C

  Chuma JF-Expert Member

  #14
  Jan 28, 2009
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Matreka VS Vyandarua....hahahaha kweli kazi ipo....!!!
   
 15. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #15
  Jan 28, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,598
  Likes Received: 18,605
  Trophy Points: 280
  Zanzibar haiwezi kuruhusiwa kujiunga na OIC kwa sababu Zanzibar sio nchi. Kuiruhusu kujiunga itakuwa yaleyale ya uvunjaji katiba. Muungano wetu ni kama ndoa. Mke akililia sana kula chapati maji, ukamkatalia kwa vile wewe hupendi kula chapati hizo, akifikia hali ya kuomba kupika chapati hizo angalau ale yeye tuu na wewe usile. Kama mume mwenye busara, utamruhusu apike chapati maji na ili kumuonyesha unampenda, itabidi na wewe ukubali kula hizo chapati maji.
  Katika suala la OIC, Zanzibar ni mke na OIC ni chapati maji. Ili kudumisha ndoa yetu ya muungano,itabidi URT ijiunge na OIC hata kama haipendi ili Zanzibar ipate chapati maji.
   
 16. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #16
  Jan 28, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mtoto akililia wembe mpe, waswahili walisema. Kama wazenji wanataka huo ukoloni wa OIC, waacheni waende, kitakachowapata wasisaidiwe kulia
   
 17. Opaque

  Opaque JF-Expert Member

  #17
  Jan 28, 2009
  Joined: Oct 24, 2008
  Messages: 1,138
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Mi naona Zanzibar iruhusiwe tu, kidogo Bara kutakuwa hakuna maandamano, kwani atakayeomba tena OIC itakuwa rahisi kumpa jibu, kwamba ipo Zanzibar. Sikujua kama kuna mgawo wa matrekta 50 !!
   
 18. Netanyahu

  Netanyahu Senior Member

  #18
  Jan 28, 2009
  Joined: Oct 2, 2008
  Messages: 148
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Nimeamini baadhi ya wanasiasa wa Zanzibar uwezo wao wa kisiasa ni mdogo sana.

  Swali ni je Zanzibar ni nchi mbele ya Jumuiya ya kimataifa? Na je katika jumuiya ya kimataifa Zanzibar yatambuliwa kama nchi.Kama jibu ni hapana je tukiwaruhusu wajiunge wakati kijumuiya ya kimataifa Zanzibar haitambuliwi kuwa ni nchi je itakuwa ni sahihi kimaamuzi kwetu na hao jumuiya za kimataifa watatuona tuna akili kweli?

  Wanzanzibari wanaposema wanaomba ruksa wakati wao sio nchi mbele ya jumuiya ya kimataifa wana maana gani? Wana akili au hawana? Au wanachosema ni kuwa wanaomba kujitenga na muungano wa Tanzania au nini?

  OIC ni muungano wa nchi zinazozotambuliwa kama nchi katika jumuiya za kimataifa.Sasa Zanzibar ikienda kama ikiwa siyo nchi kuomba kujiunga na OIC ni ombi sahihi au la kijinga lenye upungufu wa akili ya kisiasa? Na OIC ikiwapokea wakati hiyo katiba ya OIC hairuhusu nchi ambayo si Nchi mbele ya jumuiya ya kimataifa kujiunga si itakuwa ni kuvunja katiba ya OIC yenyewe na Katiba ya Tanzania ambayo pia hairuhusu Zanzibar ambayo siyo nchi kijumuiya ya kimataifa kujiunga na jumuiya za kimataifa.Na kufanya hivyio itakuwa ni kuleta mtafaruku ndani ya OIC na TANZANIA pia?

  Labda nitoe ushauri wa bure kwa wanasiasa uchwara walevi waliozoea siasa za kwenye vijiwe vya kahawa kule Zanzibar kuwa kama wanataka Zanzibar ijiunge na OIC inabidi wafanye vitu vifuatavyo:

  1.Waombe katiba ya OIC ibadilishwe ili iwe inaruhusu hata ambazo si nchi kijumuiya ya kimataifa kujiunga na OIC.Waombe kuwa katiba ya OIC iruhusu mikoa,wilaya,kata na hata vijiji kujiunga na OIC.

  Wazanzibar labda kinachowachanganya ni kuwa kuna Rais na bendera ya Zanzibar.Wasisahau kuwa nchi hii ina maraisi wengi sana.Kuna Raisi wa Daruso,Raisi wa chama cha walimu Tanzania,Raisi wa Serikali ya wanafunzi chuo kikuu cha Sokoine n.k lakini si maraisi ni wakuu tu wa jumuiya zao huko waliko.

  Raisi wa Zanzibar pia ni kama Raisi wa DARUSO ila yeye ni Raisi wa jumuiya ya wazanzibar.Bendera ya serikali ya Zanzibar isiwape kiwewe hata chama cha skauti Tanzania wana bendera na raisi wa chama cha maskauti aweza ifunga na kuipeperusha kwenye gari yake lakini kupeperusha kule hakumfanyi kuwa Raisi hasa.

  2.Waombe katiba ya Tanzania ibadilishwe ili iitambue Zanzibar kama nchi huru kamili inayoweza kujiunga kwenye jumuiya za Kimataifa.Hii itakuwa na maana ya kuvunja muungano kisheria maana kama wao watakuwa huru na Tanzania bara itabidi uhuru huo uelezwe katika katiba kuwa Tanzania bara nayo itakuwa huru. Pia hiyo itabidi ihusishe kuwa na Raisi mtendaji wa upande wa Tanzania bara ambaye atakuwa na mamlaka kama raisi kamili wa Tanzania bara pekee ili awe na uwezo wa kuiamulia Tanzania bara pekee kama ambavyo Raisi wa Zanzibar atakuwa na uwezo huo.

  Hivyo Zanzibar kuomba kujiunga si kitu cha kutazama juu juu ni suala nyeti la kuhusiana na katiba ya OIC na ile ya TANZANIA.Na hatima ya muungano na muundo wake imelalia hapo.Bunge,serikali na mahakama wana Kazi ya ziada kwa chokochoko za huyo waziri Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Kiongozi Hamza Hassan Juma ambaye kwangu naona kama mtu aliyepewa uwaziri kwa bahati mbaya.
   
 19. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #19
  Jan 28, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,933
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  Nadhani hapa unawaonea Wazanzibari. Muungano wetu ni wa baadhi ya mambo tu sio muungano wa jumla. Zanzibar ni nchi kamili kama ilivyo Tanganyika (Tanzania Bara) katika mambo yasiyo ya Muungano.

  Nadhani wanaweza kuomba katiba ibadilishwe ili mambo ya nje and uhusiano wa kimataifa lisiwe jambo la muungano.
   
 20. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #20
  Jan 28, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  What is so special with OIC???????????????? personally I do not see the crucial point inhere. 50 tractors????? if really that is the issue let Zanzibar come up with feasible Agricultural project we will assist mobilize funds for 5o tractors is still domestically possible. I have never had agricultural project under pipeline in Zanzibar of which the only encumbrance for its take off being availability of 50 tractors.

  Still Zanzibar is part of Tanzania, JK recently said 'Mtu asithubutu kuchezea mapinduzi ...tuliahidi kuyalinda..' I appeal he should deal with any one coming up with such proposal for Zanzibar to personally join OIC.

  Nevertheless, neither Zanzibar nor Tanganyika we do not need OIC lets have proper plans to redeem ourselves from poverty not thinking of aids everyday. Note there is no free lunch in this world''

  Take care guys....
   
Loading...