OIC kumlipukia Membe; Wabunge waandaliwa kumsulubu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

OIC kumlipukia Membe; Wabunge waandaliwa kumsulubu

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by nngu007, Mar 19, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Mar 19, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145  [​IMG]


  HOJA ya kujiunga na Jumuiya ya Nchi za Kiislamu Duniani (OIC) huenda ikazikwa mjini Dodoma mwishoni mwa wiki, MwanaHALISI limegundua.
  Taarifa kutoka Riyadh, Saudi Arabia; London, Uingereza; na New York, Marekani; zinasema kuingia kwa mataifa makubwa katika umoja huo kumezua utata na migogoro ambayo "imetibua hadhi ya OIC ambayo wengi walitaka kujiunga nayo."
  Taarifa za kibalozi na mashirika ya habari zinasema, hata hivyo, kwamba wimbi la kutaka kujiunga na OIC limepungua nguvu kutokana na ushindani wa mataifa makubwa kujipenyeza kwenye taasisi hiyo, wengine wakihofu kwamba ni kwa "shabaha ya kuudhoofisha."
  Awali nchi masikini na zile zenye uchumi wa kati zilijiunga na jumuia hiyo kwa malengo ya kupata misaada mbalimbali, wakati mengine yalitaka kujitambulisha nayo kwa misingi ya madhehebu ya Kiislamu.
  Tanzania imewahi kuwa na mjadala juu ya umuhimu wa kujiunga na OIC wakati wa utawala wa Rais Ali Hassan Mwinyi.
  Alikuwa baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere aliyezima mjadala huo na kujenga hoja kuwa Zanzibar iliyokuwa imejiunga, ilikuwa imekiuka katiba na kwamba kama ni uanachama, "basi inayojiunga ni Tanzania."
  Tangu hapo mjadala wa kujiunga na OIC imekwenda kimyakimya hadi mapema 2006 wakati hoja hiyo ilipoanza kupamba moto upya ikienda sambamba na hoja ya Mahakama ya Kadhi nchini.
  Suala la OIC linatarajiwa kuibuka kwa nguvu bungeni wakati Waziri wa Mambo ya Nje, Benard Membe atakapowasilisha bajeti ya wizara yake Jumamosi.
  Madai ya uanachama OIC yatakuwa makubwa kutokana na kauli ya serikali wiki mbili zilizopita, kuonekana kutotilia maanani suala la Mahakama ya Kadhi ambalo limepelekea baadhi ya viongozi wa Kiislam kuapa kutopigia kura Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu wa 2010.
  Mjini Dodoma na hasa kwenye viwanja vya bunge, tayari kuna mvumo juu ya hatua ya baadhi ya wabunge kumkwamisha Membe iwapo hataonyesha uwezekano wa serikali kuruhusu kujiunga na OIC.
  Membe, ambaye ameanza kuhusishwa na nia ya kugombea urais mwaka 2015, atakuwa na kibarua kigumu; hivyo atatakiwa kuwa mwangalifu katika kauli zake ili kupenyeza bajeti yake bila mikwaruzo.
  Angalau wabunge watano (majina tunayo), ambao wanapiga chapuo kwa ajili ya watumainiwa wa ugombea urais mwaka 2015, wamekuwa wakijiapiza "kumpa Membe wakati mgumu."
  Hata hivyo, wiki mbili zilizopita, Membe alionyesha ukomavu wa diplomasia pale alipokataa kujibu mashambulizi bungeni, akisema kwa vile suala lililoletwa na Mbunge wa Mchinga, Mudhihir M. Mudhihir linatokea mkoani kwao, basi atalipeleka kwenye vikao vya CCM vya mkoa.
  Mudhihir alimtuhumu Membe kuathiri maamuzi ya ujenzi wa kiwanda cha saruji nje ya jimbo la Mchinga, akisema waziri huyo ni "nyoka kidimu."
  "Katika hili, Membe ameonyesha ukomavu. Kulumbana hakuna maana, hasa unapokuwa na wadhifa kama alionao," ameeleza mmoja wa wabunge kutoka mkoani Lindi.
  Suala la OIC litafuatia kauli ya Membe mwaka jana alipkuwa akiwasilisha bajeti ya wizara yake. Alisema, "hakuna madhara yoyote kwa Tanzania kujiunga na IOC" na kwamba ni suala linalojadilika.
  Baadaye Oktoba mwaka jana, Membe alikaririwa akiwashangaa baadhi ya Watanzania kwa kile alichoita "kutoa kauli zinazoashiria kuiogopa OIC na baadhi ya nchi za Kiislamu."
  Alikuwa akielezea hatua iliyofikiwa katika mazungumzo kati yake na Rais wa Iran, Mahmoud Ahmednejad iliyolenga kuomba nchi hiyo kufuta madeni inayoyadai Tanzania yapatayo zaidi ya Sh. 200 bilioni.
  Membe aliwageuzia kibao waandishi wa habari na kuuliza, "Kwa nini tunashikwa na woga? Tukipewa msaada na Marekani tunaambiwa kuna mkono wa mtu; tukipewa na Iran tunaambiwa vivyo hivyo. Sasa niambieni mimi, kama Waziri wa Mambo ya Nje, niende wapi?"
  Mhadhiri wa Chuo Kikuu Dar es Salaam amenukuliwa akisema, hakuna tena haraka ya kujiunga na OIC kwa vile tayari jumuiya hiyo imekumbwa na migogoro ya "wakubwa."
  "Mimi siyo Mwislamu wala msemaji wa serikali, bali sioni umuhimu wa kujiunga na OIC kwa sasa; mataifa makubwa ya Marekani na Uingereza yamejiingiza huko ili kuiuwa. Kuna haja ya kuendelea kutafakari," ameeleza bila kutaka kutajwa jina gazetini.
  MwanaHALISI haikuweza kumpata Waziri Membe wala naibu wake kwa kile msaidizi wake alisema "wana kikao kirefu."
   
 2. n

  nguluvisonzo JF-Expert Member

  #2
  Mar 19, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 511
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Bwawa lishaingia ruba hakuna haja wala manufaa tutakayopata tena huko.
   
 3. s

  shadhuly Senior Member

  #3
  Mar 19, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 141
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  NAONA BADO TUNAYO NAFASI NZURI TU YA KUJIUNGA HUKO.Maana hayo mataifa makubwa kama Marekani yashajiunga kwa kutambua faida yake hususan ukizingatia waisilamu sio wengi nchini humo.sembuse sisi?nadhani hoja hamna hoja yoyote ya sisi watanzania kutojiunga labda tu uwe ni ushindani wa kijinga wa kiitikadi.
   
 4. m

  mamakunda JF-Expert Member

  #4
  Mar 19, 2011
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 371
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hivi jamani kwa nini watu wanang'ang'ania kujiunga na hii jumuiya ya nchi za kiislam? Kwa upande wangu naona haileti mantiki kabisa, Hapo ndo tutaaanza kukaribisha udini ambao tayari umeshaanza kuonekana. Na udini ni hatari sana
   
 5. C

  Chintu JF-Expert Member

  #5
  Mar 19, 2011
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 3,403
  Likes Received: 857
  Trophy Points: 280
  Kwani kila anachofanya marekani na sisi lazima tufanye? leta hoja zenye mashiko na si hizi za kujidhalilisha. marekani wamefanya mangapi mabaya? mbona hatujaiga?
   
 6. T

  Tiote Senior Member

  #6
  Mar 19, 2011
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 139
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sitaki kujibu hili swali. Lakini mimi najiuliza! Hii story ilitolewa na Mwanahalisi mwaka 2009, kwanini leo igeuzwe thread ili watu waitolee maoni? Kwa nini iibuke leo? Hizi ni zile zile vita za kipuuzi ambazo nia yake ni kupima upepo wa wana JF na vile vile kuendelea kuwafanyia character assassination watu wasiowapenda. Mimi naona hii thread iondolewe maana haina tija na inatuondoa kwenye mijadala ambayo ni current maana Membe alishayatolea ufafanuzi mambo haya na kwamba Tz haitajiunga na jumuiya hiyo!
   
 7. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #7
  Mar 19, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  hii habari ni ya lini?
   
 8. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #8
  Mar 19, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Hii Habari ni ya March 17th 2011; na iko kwenye ajenda kujadiliwa na Wabunge Mwaka huu na pia Mahakama ya Kadhi
   
 9. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #9
  Mar 19, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Angalia Ramani hii hakuna US as Mwanachama wa OIC

  Sioni Vibaya kama Serikali ya Zanzibar na Pemba wakitaka kujiunga kwa bara the organization is very discriminatory to other religions followers kama shule kama imegharimiwa na OIC you must be a muslim to attend the school; kwetu bara waisilamu walisoma shule za kikristo bila matatizo ya kusengenywa.

  [​IMG][​IMG][​IMG][​IMG][​IMG][​IMG][​IMG][​IMG][​IMG][​IMG][​IMG][​IMG][​IMG][​IMG][​IMG][​IMG][​IMG][​IMG][​IMG][​IMG][​IMG][​IMG][​IMG][​IMG][​IMG][​IMG][​IMG][​IMG][​IMG][​IMG][​IMG][​IMG][​IMG]
   
 10. Kingcobra

  Kingcobra JF-Expert Member

  #10
  Mar 19, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,008
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  OIC ni udini tena ulioota mvi. Siku zote naomba ife kifo cha asili na kusahaulika milele.
   
 11. S

  Salimia JF-Expert Member

  #11
  Mar 19, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 665
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Well said Tiote!
   
 12. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #12
  Mar 19, 2011
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Let it die. Kwani huku kujiunga kujiunga kunatusaidia nini zaidi ya wao kupata fadhila na maisha bora kwa familia zao.
   
 13. k

  kibokogiziba Member

  #13
  Mar 19, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama OIC ni idini ubalozi wa vatcan uliopo hapa chini ni uapagani ? au hujui chemsha bongo kabla hujatoa maoni
   
 14. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #14
  Mar 19, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,248
  Likes Received: 3,836
  Trophy Points: 280
  Yakaisari aachiwe kaisari waislamu waachiwe imani yao kitendo cha srkal kuingilia imani za watu ni kukiuka katiba ya jamhuri ambayo inasema wazi kuwa tz haina dini
   
 15. g

  gidytitus JF-Expert Member

  #15
  Mar 19, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 332
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Tafakarin kabla ya kutoa matamko yenu jamen! Wengne hapa hatujui kuna nin nyuma ya hyo OIC, lazima tuwe na pulse kwanza! Tujiulze kwa nin kpnd kile ilshndkana na ni kwa nin upande mmoja miongon mwa iman za watanzania ulpinga kwa nguvu juu ya Tz kujiunga na OIC? Tuachen ushabiki, em tufaham kwanza faida za kujiunga na hyo OIC kabla hatujajiingiza huko, tusiangalie faida moja tu ya kufutiwa maden af madhara yakawa ndo meng zaid! Tukumbuke dawa ya deni ni kulipa na huleta heshima na adabu kat ya mkopesha na mkopeshweji! Mkwere ahakikshe analpa maden yote coz hela tayar tushampatia! Hatutaki iyo mambo ya kusamehewa samehewa wakat tunaweza, af aache kukopa kopa ovyo coz hata hyo mikopo yenyew hatuioni ikfanya cha maana!
   
 16. S

  Songasonga Senior Member

  #16
  Mar 20, 2011
  Joined: Mar 13, 2011
  Messages: 152
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ninavyojua Mimi OIC imesimamisha shughuli zake sasa iweje tena ijadiliwe? Au gazeti hili linataarifa tusiyo kuwa nayo wengine? Au nia ni Membe Hebu wanaojua tujuze
   
 17. S

  Salimia JF-Expert Member

  #17
  Mar 20, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 665
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hizi ni propaganda tu za kutaka kuwashalilisha baadhi ya watu tusiowataka,, ni kupuuzia tu utumbo kama huu
   
 18. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #18
  Mar 20, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 738
  Trophy Points: 280
  mheshimiwa waziri alilitolea maelezo ya klutosheleza jambo la OIC.
  nina shaka na nia ya watu kuelekea kujadili watu na sio hoja.
  la msingi ni wananchi wajue kiundani OIC ipoje ili watu wasipate nafasi ya kupiga propaganda chafu
   
 19. NGUZO

  NGUZO JF-Expert Member

  #19
  Mar 20, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 253
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  mamakunda udini upo wapi hapo? Je umeona udini wowote kwa nchi zilizotuzunguka zilizojiunga na oic? Acheni roho mbaya, hawa waislamu ni ndugu zenu wakipata misaada nyie mnaumia kwa nini? Mbona nyie mna ubalozi wa vatican hapa bongo na misaada mingi ya kanisa inapitia humo, au waislamu hawana haki ya kuendelea?
   
 20. shemasi

  shemasi Member

  #20
  Mar 20, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hakuna udini wowote na kujiunga na OIC,hao wanaopinga wana ajenda ya kupandikiza hofu hii kwa raia.
  kama kuna udini huyu waziri wa mambo ya nje nae ni muislamu? bdugu zangu tujikite kwnye kujenga nchi na sio hoja za udini.
   
Loading...