OIC: Kawawa, Mwinyi Watoe Kauli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

OIC: Kawawa, Mwinyi Watoe Kauli

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ibrah, Nov 5, 2008.

 1. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #1
  Nov 5, 2008
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Samahani Mod, imenibidi niitenganishe hii mada ili kuwaomba wadau na hasa Mwanakijiji kupitia KHL wawatafute hawa wazee ili watoe mawazo yao kuhusu IOC kwa sababu zifuatazao:-

  KAWAWA
  Ni mpigania Uhuru pamoja na Nyerere na amefanya kazi na Nyerere kwa muda mrefu, pia ni Muislamu na alikuwa Waziri wakati Nyerere akifuta Mahakama ya Kadhi na kutaifisha Shule za Wakristo.

  Wakati suala hili la OIC likiendelea, Mzee Kawawa amekaa kimya kabisa na hatujui msimamo wake ni upi katikahili akiwa kama Mzee aliyefanya kazi na Nyerer na kupitisha maazimio magumu pamoja naye.

  MWINYI
  Alikuwa Rais wa Tanzania na ni wakati wa utawala wake ndipo Waislamu walidhinikiza sana masuala ya Uislamu katika nchi yetu, pia amewahi kunukuliwa kusema kuwa Wakristo wasiohofu kuhusu Mahakama ya Kadhi maana itakuwa haihusiki na mabo ya Jinai.

  Hata hivyo hatujawahi kusikia kauli yake kuhusu Tanzania kujiunga na OIC ingawa tunajua kuwa OIC na Mahakama ya Kadhi ni mapacha!

  Ni wakati wa Utawala wake ndipo Zanzibar ilijiunga na OIC na ni ajabu kuwa 'alikuwa hajui' hilo na sina uhakika kama lilifanyika kwa kibali chake kama Rais wa Tanzania au la.

  OMBI LANGU:
  Waandishi mliomo humu muwatafute Wazee hawa ili Watanzania tusikie kauli na misimamo yao kuhusu masuala haya; kimya chao kinanipa wasiwasi maana kama Rais ameshituka juu ya mwelekeo wa majadiliano nao Wazee wetu wapo kimya maana yake nini?
   
 2. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #2
  Nov 5, 2008
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,668
  Likes Received: 21,901
  Trophy Points: 280
  Misimamo yao sidhani kama inaweza kutatua mgogoro huu wa mahakama ya kadhi na OIC. Jambo la msingi ni kuangalia katiba yetu inasemaje kuhusu suala kama hilo na jambo lolote linalofanyika hapa nchini halivunji katiba basi.
  Tatizo letu Watanzania tunakuza sana mambo yasiyo na msingi na kusahau mambo ya maana. Sidhani kama suala la OIC lilikuwa lakuleta mjadala wa kitaifa kisa eti tutapata misaada, tufuate katiba yetu katika kukubaliana.
  Vinginevyo kama tunaona kasoro katika katiba yetu, basi tuitengeneze upya ikidhi matarajio.
   
 3. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #3
  Nov 5, 2008
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Nia ni kujua misimamo yao kuhusu suala hili maana ni watu wa kuheshimika sana na kimya chao kinatia mashaka makubwa. Kwa nini wawe kimya hivyo wakati mshikamano wa nchi uko shakani?
   
 4. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #4
  Nov 5, 2008
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hao uliopendekeza hawahusiani na hii kadhia ya OIC. Anyway kupata maoni yao si vibaya. Lakini bora ungemjaliza na Rais Mstaafu wa Zanzibar Dr. Salmin Amour Juma. kwani lilipozuka suala hilo yeye ndiye aliyekuwa akiiongoza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
   
 5. M

  Masatu JF-Expert Member

  #5
  Nov 5, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Salmin nasikia anaumwa na at one point alishapoteza uwezo wa kuona kabisa.
   
 6. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #6
  Nov 5, 2008
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0


  UIli iweje?

  tunayo katiba na ni nchi ya watu milioni 40 bado tunategemea kauli za watu waliopitwa na nyakati

  Get a grip
   
 7. I

  Iga Senior Member

  #7
  Nov 7, 2008
  Joined: Dec 17, 2007
  Messages: 112
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hali kadhalika Mzee Malecela, Mzee Msuya, Salim Ahmed Salim, Gharib Bilali, Salmin Amour, Mzee Jumbe au wanae, Hawa Sinare, Aisha Sululu, Ami Mpungwe, mawaziri wote wa zamani Waislamu, wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya wote waislamu na wanachama wa vyama vyote vya siasa ambao ni Waislamu.

  Hawa wana dhambi kubwa kwa Mungu maana wakati dhuluma hii inafanyika walikuwepo madarakani au kwenye siasa kwanini sasa wanyamaze wakati watu wanadai haki zao za Msingi na kupakaziwa uongo wa kvvunja au kupasua katiba, umoja, amani na huu na ule!!!!
   
Loading...