Ohooo mchungaji Antony lusekelo utakosa la kujitetea.shauri yako

mbagokizega

Senior Member
Oct 22, 2016
111
297
Nawasalimu.

Nyote si mnajua kwamba pombe ya viroba imepigwa marufuku? Na tayari polisi wameashaanza operesheni za kuwasaka wauzaji wa pombe hiyo kinyemela?.

Bila shaka marufuku hii itasababisha kushamiri kwa pombe ya gongo,na bila shaka kwa mujibu wa watendaji wetu hii nayo itakuwa habari itakayoteka anga la siasa za hapa mjini.na kwa aina ya uongozi wa kutafuta kiki tutarajie viongozi kutaka kulitumia suala hili la kupambana na wauzaji wa pombe gongo kujitafutia majina.

Hivii ikitokea mkuu wa mkoa akiwataja wauza gongo papa hapa mjini na miongoni mwao akawemo mvhungaji lusekelo je tutapata wapi hoja ya kumtetea au ye binafsi atajiteteaje ilhali alishaahid tangu huko nyuma kwamba endapo waandishi wale waliomuandika vibaya hawajafa mpaka kufikia mwezi wa tatu ataenda kuuza gongo.

Babaangu mchungaji atajiteteaje kwamba hahusiki na biashara ya gongo?.tutamlaumu tena kaka bashite au tutayaamini maneno yake mwenyew mchungaji.

Binafsi natamani lisitokee jambo lolote litakaloenda kutia mashaka huduma ya kiroho inayotolewa na baba mvhungaji lusekelo lkn Niko jaribuni kwamba tamanio langu hili la kuifanya jamii iheshimu huduma ya kiroho itolewayo naye ni kuombea vifo vya hao waandishi kitu ambacho Mungu huyu tumuabudiye hakimpendezi
 
Hata sijakuelewa.gongo na Lusekelo,sijajua umeongea na umemaanisha nini
 
Nina hesabu siku tu mwezi ukisha bila wale waandishi waliomuandika mzee wa upako hawajafa basi nitaamini zilikuwa ni konyagi na si Lusekelo

Wafuasi wake mmkumbushe ahadi yake ya biashara ya gongo msisahau sadaka kwa ajili ya mtaji
 
Biashara ya Gongö wakati viroba vimepigwa marufuku atapiga hela mbaya..
 
Kwani bado unamashaka na Mzee wa Upako Baba mchungaji Anthony Lusekelo kwamba hatumii divai iyochacha (kalinya)..?

Na Hilo la kusema kuwa atakwenda kuuza Gongo hiyo ni lugha ya picha tu alitumia.
 
Back
Top Bottom