Ohoo! CCM waanza kumkana Samia juu ya ubabe wake kwa Chadema.

Ohoo! CCM waanza kumkana Samia juu ya ubabe wake kwa Chadema.

Sexless

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2017
Posts
27,663
Reaction score
65,198
Screenshot_20250427-155322.png
 
CCM + CDM + ACT + TLP = Watanzania.

Tatizo CCM inatumika na walioishika nchi mateka, watu hawa ndio huwatumia wana CCM bila ya wenyewe kujijua.

Kwa sasa CCM ni adui namba moja wa jamhuri, ni nani hawa walioiteka CCM na kuiteka Dola?

Watanzania wote bila kujali vyama niwakati wakusimama na kudai haki maana haki ndio msingi wa amani na maendeleo, haki inayodaiwa sio tu ya kuchagua na kuchaguliwa bali haki Kila mahala, kwenye ajira, huduma za kijamii nk.
 
Mzee wasira ndo katufisha hapa ,maana anajua hana cha kupoteza ,umri uliobaki mbele yake ni mapenzi yake mola ,so hata taifa liteketee hana shida, mzee ana roho mbaya hataki vijana wale matunda ya nchi yao kama ambavyo ameyala kuanzia Nyenyeye yupo.
 
Hakuna mwanadamu anazaliwa akiwa mwovu, waovu wanatengenezwa. CCM inajitahidi sana kuwabadilisha watu wawe waovu. wapo waliojiunga na CCM wakiwa na dhamira njema, wakiamini CCM ina dhamira njema, wengi hawajui kuwa CCM imetekwa na maharamia, na wale wanaCCM wema wanatumika tu na maharamia.

Nguvu kubwa ya CCM katika kutengeneza watu maharamia imeelekezwa jeshi la Polisi na TISS. Ndiyo maana matendo ya taasisi hizi mbili ni ushetani mtupu.

Tunachokitaka ni nchi yetu iwe na haki, na wananchi wawe na maamuzi ya mwisho ya nani awaongoze, na hilo likiwepo hata huu ujambazi wa kubadilisha vyombo vyetu vya usalama kuwa vya kishetani, ungekoma.
 
CCM inaamini katika mawazo huru. Kila mtu ana haki ya kutoa maoni yake.

Ila kujibu haya maoni ni kwamba, sio CCM inayotumia Polisi, bali Polisi ni Mali ya Serikali na kazi yake ni kuhakikisha Serikali inafanya kazi zake katika mazingira yaliyo na utulivu na amani.
Hivyo, yeyote anayesumbua katika hilo atashughulikiwa tu!
 
Kwani hao Police wanaingia tu mzigoni pasipo mkuu wa mhimili ambaye ni ccm kusema kitu?

Kwani hakuna hoja kupambana na hoja za wanachadema mpaka police waingizwe mzigoni kuzima hoja za chadema kwa nguvu
 
Tupiganie HAKI bila kujali Vyama wala Itikadi.
HAKI ndio mtindo mzima wa maisha ya binaadam.
Hata ndani ya ukoloni pangekuwemo na HAKI ya kweli, pasingekuwepo na sababu ya kuuondoa ukoloni.

Sasa CCM hata hawaoni aibu kabisa kutaka kunyima HAKI ya waTanzania; maana yake ni kwamba wanawachochea waTanzania kuichukua HAKI yao kwa nguvu.
 
Back
Top Bottom