Ndio maana nikasema , kwa wakati huo "pengine" yeye aliona muundo na muungano huo una faida kwa wakati huo .
Mwaka 2014 Lissu alihoji bungeni hati ya muungano iletwe ,tukajionea kituko wakagoma kuileta badala yake kikasambazwa kipeperushi mtandaoni kuwa ndio hati ya muungano ila bado wakachemka kwenye saini ya Karume baada ya Lissu kuleta sheria za nyuma zenye saini halisi ya Karume kabla ya hiyo inayoitwa hati ya muungano ya 1964.
Hatuwezi kumlaumu , ukinisoma vizuri ndio maana nimesema kwa alichokifanya aliona pengine kina manufaa wakati huo, ila kwetu sisi tuliopo sasa muungano huu hauna tija yoyote na sababu nimeweka hapo kwenye post ya juu kwa uchache tu japo zipo nyingi.
Nikatoa na mfano wa picha ya simu za 1960, 1970,1980 hatuwezi kumlaumu aliyetengeneza simu zile kwamba kwanini hakutuwekea teknolojia kama ya leo kuweza kufanya video calling.
Hatuwezi kumlaumu sababu alitwngeneza simu kuwezesha mawasiliano kwa muda huo na nyakati hizo ila kwa wakati huu aina hii ya simu aliyotengeneza haifai ndio maana tumehamia katika teknolojia mpya ya simu za kisasa.
Hivyo pia kwa Nyererw tusiwe rigid kusema kwakua aliunda muungano basi tutakapoona hauna tija tusiuvunje , maana njia ya kutatua kosa ni kujisahihisha na sio kusema hakuna kosa kama mleta mada alivyokumbatia eti tusivunje muungano.