Ofisini kwetu wapo kwenye vikao vya mwisho kuamua likizo ya lazima hali si nzuri

mtotomtamuu

JF-Expert Member
Dec 4, 2016
602
1,454
Mimi nafanya kazi kwenye kampuni kubwa tu, Kuanzia wiki iliyopita kumekuwa na vikao vya wakurugenzi na mmiliki wa kampuni hali imekuwa mbaya, raw materials zote za uzalishaji wa material ya kutengeneza matrailer mali nyingine hamna, nchi zilizokuwa zinategemewa kuingiza material kutoka Ulaya zipo kwenye lockdown na hawafanyi kazi.

Kampuni haizalishi wala kuuza chocote na wameona wafanyakazi wote tunaenda kupewa likizo ya miezi miwili yenye malipo, lakini hali ikiendelea tunaweza ongezewa likizo ndefu isiyo na malipo, na hapa kinachosaidia wengi tulikuwa na mikataba ya kudumu

Tuombeane jamani na tuwe makini, hii hali isikukute ukiwa na familia inayokutegemea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hali imesha kuwa tete...
 

Attachments

  • IMG_20200406_203726.jpg
    IMG_20200406_203726.jpg
    16.1 KB · Views: 2
  • IMG_20200406_203721.jpg
    IMG_20200406_203721.jpg
    18.7 KB · Views: 2
Mkuu usikate tamaa, na itakapotokea jitahidi kukubaliana na hali halisi vinginevyo ukilegea tu ujue KISUKARI na Magonjwa ya Moyo yatajenga kibanda kwenye mwili wako. Aminisha akili na mwili wako kwamba kuna Maporomoko ya Kiuchumi Dunia nzima kwahiyo hilo pigo siyo lako peke yako bali ni la Ulimwengu wote. Pia kumbuka msiba wa wengi ni sherehe.
Pamoja sana mkuu
 
Bora ninyi mnapewa likizo yenye malipo.
Kuna wenzenu kampuni flani kubwa tu inafanya uhuni inataka kuwapa watu likizo bila malipo.
Wakabanwa wakasema watawalipa nusu mshahara, leo wanawaaambia wasaini makubaliano ya likizo ya malipo robo mshahara.

Kampuni kwa zaidi ya miaka 20 inatengeneza faida hakuna hasara, na malengo yakizidi hawawapi bonus au incentives wafanyakazi, kuna wakati hawalipi overtime na wanafanyisha watu kazi kweli kweli.

Wafanyakazi wameibeba kampuni na sasa imefika zamu ya kampuni kuwabeba wafanyakazi ndio wanataka kuwatendea unyama huo tena wafanyakazi wenye mikataba ya kudumu sio vibarua.

Naiomba serikali iingilie kati na kutoa muongozo kama walivyofanya UK.
Wachezaji wa timu za mpira wanaolipwa pesa nyingi wameombwa kukatwa mishahara yao na kuwalipa mishahara wale wenye malipo ya kila siku kama vibarua au wafanyakazi wa kawaida wenye mishahara midogo.

Rwanda imetoa muongozo wa kutowalipa watumishi wa hadhi ya juu wenye mishahara mikubwa ili kusaidia kutatua janga hili.

Hapa ningeomba serikali itoe muongozo kwa sekta zote waajiri bora wapunguze mishahara kwa wale wanaolipwa mamilioni mengi na kuwalipa angalau nusu mshahara watu wa chini wanaotaka kuwapa likizo bila malipo.

Utaona kampuni kama hiyo niliyo ilalamikia unaweza kukuta uongozi wa juu wakajilipa mishahara nusu au kamili huku wakitaka kulipa wa chini robo robo. Unakuta hao wa juu wanalipwa mamilioni kibao na sio watu wa uzalishaji kama hao wa chini.
Hawa wa juu wanashinda ofisini kwenyye internet, kunywa chai, maziwa na kahawa kisha wanarudi nyumbani kwa miezi yote miwili.

CC: Waziri wa Kazi/Ajira, Waziri wa Sheria, Waziri wa Fedha, Waziri Mkuu na Mh Raisi Magufuli.
Toeni muongozo wazee wangu.
 
Back
Top Bottom