Ofisi za TCU zavunjwa, computers na nyaraka nyeti zaibwa!

DATAZ

JF-Expert Member
May 25, 2012
2,449
5,974
Ofisi za TCU zimevamiwa usiku wa kuamkia leo na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi. Walinzi wake wamelewa kwa kinachaodhaniwa ni madawa ya kulevya waliyonyweshwa na hadi majira ya mchana huu hawajaamka. Eneo la ofisi liko chini ya ulinzi mkali wa polisi wakati uchunguzi wa tukio hilo ukiendelea.

Source: ITV.
 
maweeeee!,
tutegemee vyeti feki vya kumwaga mitaani sasa
 
lakini ofisi nyeti kweli kama TCU kweli haina walinzi wenye silaha za moto kama polisi wanavyolinda benki?, serikali haijui ile ni ofisi nyeti yenye hazina ya elimu ya wananchi wake?
dah, inauma.
 
Mi naona nxt time wavunje za HESLB,coz hazitusaidii chochote,zaidi ya kutuibia ela zetu za appeal,na application
 
  • Thanks
Reactions: GP
lakini ofisi nyeti kweli kama TCU kweli haina walinzi wenye silaha za moto kama polisi wanavyolinda benki?, serikali haijui ile ni ofisi nyeti yenye hazina ya elimu ya wananchi wake?
dah, inauma.

Jamani ,hivi si kuna tukio kama hili lilitokea miaka miwili au mmoja uliopita na kukaibiwa benzi ya mkurugenzi, laptops na cmuputers, na walinzi tena wakampuni binafsi wakaleweshwa madawa ya kulevya? Hawakujifunza chochote?
 
  • Thanks
Reactions: GP
Nimeipenda hii

Hizo ofisi za TCU zimevunjwa na Chadema. Wao ndiyo waliogiza wale vijana kuvamia ofisi hizo na kuiba nyaraka kwa lengo la kutaka kuonyesha kuwa serikali ya Chama Cha Mapinduzi na Rais wake Jakaya Kikwete, ni dhaifu.

Wananchi tutoke barabarani kukilaani chama hiki kwa hatua yake ya kufadhiri wezi: Vyuo vyote nchini vimeshikwa na Chadema – Nape Nnauye.
 
Jamani ,hivi si kuna tukio kama hili lilitokea miaka miwili au mmoja uliopita na kukaibiwa benzi ya mkurugenzi, laptops na cmuputers, na walinzi tena wakampuni binafsi wakaleweshwa madawa ya kulevya? Hawakujifunza chochote?
kuna ofisi nyeti za serikali kama hawa TCU hata HESLB hata NECTA, na kwa UDHAIFU wa watendaji wetu hata backup za data utakuta hawana.
mi kwa ushauri wangu hao TCU muhusika awajibishwe.
 
kwani hawana replication server nje na hapo walipo inayofanya backup ya kila kitu???
 
kuna ofisi nyeti za serikali kama hawa TCU hata HESLB hata NECTA, na kwa UDHAIFU wa watendaji wetu hata backup za data utakuta hawana.
mi kwa ushauri wangu hao TCU muhusika awajibishwe.

Usiwe na hofu mkuu, ingawa sijajua unamanisha muhusika gani, ila naamini wamekusikia. Kesho tu watamhamishia idara nyingine, ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama yake!
 
Ofisi za TCU zimevamiwa usiku wa kuamkia leo na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi. Walinzi wake wamelewa kwa kinachaodhaniwa ni madawa ya kulevya waliyonyweshwa na hadi majira ya mchana huu hawajaamka. Eneo la ofisi liko chini ya ulinzi mkali wa polisi wakati uchunguzi wa tukio hilo ukiendelea.

Source: ITV.

Kwa wanaomsakama Jk watasema ni yeye katuma majambazi TCU
 
Back
Top Bottom