hata mimi
JF-Expert Member
- Oct 17, 2017
- 1,356
- 1,437
Ushauri wangu kama inawezekana tuachane na hii kitu badala yake (picha ya) nembo ya taifa pekee ndio iwekwe maofisini
Hoja yangu inakuja kwa sababu kwanza urais ni taasisi na si mtu kama mtu ingawa rais ni mtu mmoja.
Pili mihimili ya dola ile mingine haijaipa umaalumu picha ya kiongozi mkuu vinginevyo tungeona maofisini picha nne (ya Baba wa Taifa, ya Rais, ya Spika wa Bunge na ya Jaji Mkuu)
Tatu na mwisho kabisa ni kwamba Raisi akitoka madarakani picha yake inakosa thamani kabisa utafikiri haikugharamiwa maelfu ya shilingi kuifikisha hapo
Nina mfano mmoja mashuleni walimu walipelekeshwa sana kuwa na picha ya Raisi awamu ya tano muhula wa pili kisha alipoapishwa Rais awamu ya sita kukatolewa amri ya kuondoa/kutungua picha ya Rais awamu ya tano haraka sana na kuweka/kutundika picha ya Raisi awamu ya sita
Picha zile zilizotunguliwa kukasemwa zitunzwe kwenye kasiki mpaka kutakapotolewa utaratibu wa wapi zipelekwe lakini cha ajabu ni zaidi ya mwaka sasa picha zinaharibika tu bure mashuleni hakuna mwongozo wowote
Matokeo yake sasa baadhi yao wamezitupa na wengine wamediriki kuziweka mpaka chooni ili tu zisiwabane. Sasa kama haikuwa na umuhimu hivyo ni kwanini ilinunuliwa kwa gharama kubwa kiasi kile?