Ofisi za mawaziri ni 'vijiwe'

G.MWAKASEGE

Senior Member
Jun 29, 2007
153
15
Zaidi ya asilimia 90 ya mawaziri wanatumia ofisi zao kama `vijiwe` lakini muda wao mwingi wanautumia kufanya shughuli zao binafsi zikiwemo za biashara badala ya zile walizoajiriwa kuzifanya.

Maoni hayo yalitolewa juzi usiku na Profesa Mwesiga Baregu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alipokuwa akichangia mada katika kipindi cha `Jenerali on Monday` kinachorushwa na kituo cha televisheni cha Channel Ten.

Profesa Baregu alisema, hali hiyo inasababisha mawaziri wengi kushindwa kutekeleza majukumu yao ya kuwahudumia wananchi.

`Watu wanajua mawaziri wengi wa serikali hii ni wafanyabiashara hivyo ofisi kwao ni kama `kijiwe` kwa ajili ya kufanikisha shughuli zao binafsi` alisema.

Aidha, katika kipindi hicho watu mbalimbali walitoa maoni yao juu ya utendaji wa serikali ya awamu ya nne.

Baadhi yao walisema, hakuna dalili zozote za kutekeleza ahadi ya serikali ya awamu ya nne ya kuwaletea wananchi maisha bora.

Akichangia mada katika kipindi hicho, Bw. Abdalah kutoka Tanga alisema, hali ya maisha kwa wananchi wa kawaida inazidi kuwa ngumu kuliko kipindi chochote katika historia ya nchi hii.

Naye mchangiaji mwingine Bw. Benny kutoka Mwanza alisema, viongozi wengi wa serikali hivi sasa wanachukua raslimali za taifa bila huruma na kuzifanya mali zao.

Alisema watendaji wengi wa serikali hasa ngazi za juu hawajali wananchi wala hawafuati sheria zinazolinda maadili ya viongozi wa umma.

Aidha katika mjadala huo baadhi ya wachangiaji walisema, tabia ya ufisadi iliyopo hivi sasa inatokana na viongozi wengi kipindi cha nyuma kufuata falsafa ya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kwa unafiki.

Walisema Mwalimu Nyerere alikuwa na falsafa ya `Ujamaa na Kujitegemea` kwa kuwa aliamini kwamba hiyo ndiyo ilikuwa njia pekee ya kuwafanya watu wawe wamoja.

Walitoa mfano kwa marehemu Oscar Kambona ndiye kiongozi pekee aliyeweza kumpinga Mwalimu juu ya falsafa hiyo lakini wengine walimkubalia kwa unafiki.

Naye muongozaji wa kipindi hicho Bw. Generali Ulimwengu alisema, kama leo Mwalimu Nyerere angefufuka akaona ufisadi unaofanyika ndani ya serikali angekufa mara ya pili.

Alisema ni bora mawaziri wakatangaza kwamba wao ni wafanyabiashara na ikajulikana hivyo badala ya kuendelea kutumia nafasi walizonazo ili kufanikisha biashara zao.

Aliongeza kuwa viongozi wa sasa wanafanya ufisadi huu bila ya uoga kwa kuwa wanajua ifikapo mwaka 2010 kwenye uchaguzi watanunua kura kwa kilo moja ya sukari na kipande cha kanga.

SOURCE: Nipashe
 
Naye muongozaji wa kipindi hicho Bw. Generali Ulimwengu alisema, kama leo Mwalimu Nyerere angefufuka akaona ufisadi unaofanyika ndani ya serikali angekufa mara ya pili.

Hahahahah! Ulimwengu bwana anavituko kwelikweli
hii sentensi sijui aliipata wapi!
 
Niliangalia kipindi kile,

Hawa jamaa walifanikisha kuingiza serikali madarakani kwa fedha yao, unategemea hela yao itarudi vipi? Ni lazima wafanye biashara ndani ya ofisi na kutumia madaraka yao kurejesha hiyo fedha.

Hii ni hatari kwa mstakabali wa nchi, amani iliyopo tuelewe msingi wake nini, sio kusema ni SISIEM tu kirahisirahisi hivi. Mwangalieni mwalimu Nyerere aliyefanikisha hili aliishi vipi na hadi akatufikisha hapa. Hakukuwa na tuhuma zozote za ubadhirifu na ufisadi dhidi yake.

Kwa hali iliyopo sasa mustakabali wa nchi upo hatarini, mgawanyo wa rasilimali haupo sawa then unasema unasema wapinzani wanahatarisha utangamano wa nchi, hapana, ninyi mafisadi ndo mnahatarisha amani ya nchi.

ACHENI UFISADI MTAANGAMIZA NCHI.
 
Kama mpendwa wa Mwalimu (RIP) bwana Mkapa aliweza kuwaonyeshea wenzake mfano wa namna ya kuwa wajasiriamali na kuigeuza nyumba kuu ya Taifa pale Magogono pango lake la biashara,na mdogo wake ndugu kikwete kutamka bayana tena hadharani kuwa hawezi kuwachunguza viongozi wastaafu,mnategemea kina Karamagi,Mramba,Chenge,Mgonja,Rutabanzibwa,Balali,Lowassa,Simbakalia, waziheshimu ofisi zao?
 
Hivi kile kipindi cha Wosia wa baba pale redio tanzania bado kipo?

Na jinsi watu wanavyomkubali mwalimu(RIP)..hIki kipindi si kinaweza kwenda against maslahi ya kisiasa ya baadhi ya wakubwa.
kutokana na ujumbe mzito wa Mwalimu?

ndo maana nauliza hiki kipindi bado kinarushwa?
 
Niliangalia kipindi kile,

Hawa jamaa walifanikisha kuingiza serikali madarakani kwa fedha yao, unategemea hela yao itarudi vipi? Ni lazima wafanye biashara ndani ya ofisi na kutumia madaraka yao kurejesha hiyo fedha.

Hii ni hatari kwa mstakabali wa nchi, amani iliyopo tuelewe msingi wake nini, sio kusema ni SISIEM tu kirahisirahisi hivi. Mwangalieni mwalimu Nyerere aliyefanikisha hili aliishi vipi na hadi akatufikisha hapa. Hakukuwa na tuhuma zozote za ubadhirifu na ufisadi dhidi yake.

Kwa hali iliyopo sasa mustakabali wa nchi upo hatarini, mgawanyo wa rasilimali haupo sawa then unasema unasema wapinzani wanahatarisha utangamano wa nchi, hapana, ninyi mafisadi ndo mnahatarisha amani ya nchi.

ACHENI UFISADI MTAANGAMIZA NCHI.

Msee,
Naona leo hutaki mchezo yaani....nakuchungulia sasa thread kama ya tatu hivi, una-indict na kutoa verdict hapo hapo!!! tuna hitaji wengiwengi kama wewe,kazi nzuri sana.
 
Back
Top Bottom