G.MWAKASEGE
Senior Member
- Jun 29, 2007
- 153
- 15
Zaidi ya asilimia 90 ya mawaziri wanatumia ofisi zao kama `vijiwe` lakini muda wao mwingi wanautumia kufanya shughuli zao binafsi zikiwemo za biashara badala ya zile walizoajiriwa kuzifanya.
Maoni hayo yalitolewa juzi usiku na Profesa Mwesiga Baregu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alipokuwa akichangia mada katika kipindi cha `Jenerali on Monday` kinachorushwa na kituo cha televisheni cha Channel Ten.
Profesa Baregu alisema, hali hiyo inasababisha mawaziri wengi kushindwa kutekeleza majukumu yao ya kuwahudumia wananchi.
`Watu wanajua mawaziri wengi wa serikali hii ni wafanyabiashara hivyo ofisi kwao ni kama `kijiwe` kwa ajili ya kufanikisha shughuli zao binafsi` alisema.
Aidha, katika kipindi hicho watu mbalimbali walitoa maoni yao juu ya utendaji wa serikali ya awamu ya nne.
Baadhi yao walisema, hakuna dalili zozote za kutekeleza ahadi ya serikali ya awamu ya nne ya kuwaletea wananchi maisha bora.
Akichangia mada katika kipindi hicho, Bw. Abdalah kutoka Tanga alisema, hali ya maisha kwa wananchi wa kawaida inazidi kuwa ngumu kuliko kipindi chochote katika historia ya nchi hii.
Naye mchangiaji mwingine Bw. Benny kutoka Mwanza alisema, viongozi wengi wa serikali hivi sasa wanachukua raslimali za taifa bila huruma na kuzifanya mali zao.
Alisema watendaji wengi wa serikali hasa ngazi za juu hawajali wananchi wala hawafuati sheria zinazolinda maadili ya viongozi wa umma.
Aidha katika mjadala huo baadhi ya wachangiaji walisema, tabia ya ufisadi iliyopo hivi sasa inatokana na viongozi wengi kipindi cha nyuma kufuata falsafa ya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kwa unafiki.
Walisema Mwalimu Nyerere alikuwa na falsafa ya `Ujamaa na Kujitegemea` kwa kuwa aliamini kwamba hiyo ndiyo ilikuwa njia pekee ya kuwafanya watu wawe wamoja.
Walitoa mfano kwa marehemu Oscar Kambona ndiye kiongozi pekee aliyeweza kumpinga Mwalimu juu ya falsafa hiyo lakini wengine walimkubalia kwa unafiki.
Naye muongozaji wa kipindi hicho Bw. Generali Ulimwengu alisema, kama leo Mwalimu Nyerere angefufuka akaona ufisadi unaofanyika ndani ya serikali angekufa mara ya pili.
Alisema ni bora mawaziri wakatangaza kwamba wao ni wafanyabiashara na ikajulikana hivyo badala ya kuendelea kutumia nafasi walizonazo ili kufanikisha biashara zao.
Aliongeza kuwa viongozi wa sasa wanafanya ufisadi huu bila ya uoga kwa kuwa wanajua ifikapo mwaka 2010 kwenye uchaguzi watanunua kura kwa kilo moja ya sukari na kipande cha kanga.
SOURCE: Nipashe