Ofisi ya Waziri Mkuu yakanusha habari ya Tanzania Daima | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ofisi ya Waziri Mkuu yakanusha habari ya Tanzania Daima

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Msanii, Jan 28, 2012.

 1. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #1
  Jan 28, 2012
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  KUKANUSHA TAARIFA ZA UPOTOSHAJI ZA
  GAZETI LA TANZANIA DAIMA


  OFISI YA WAZIRI MKUU imesikitishwa na habari iliyochapishwa na gazeti la TANZANIA DAIMA toleo namba 2610 la Alhamisi, Januari 26, 2012, kwenye ukurasa wake wa kwanza yenye kichwa cha habari:
  “Dk. Mwakyembe aipasua Serikali”
  · Pinda amtaka azungumzie hali yake
  · Aunga mkono posho za Wabunge kupanda
  · Adai wanaosaka Urais hawana akili nzuri

  Kwenye habari hiyo iliyopewa uzito wa juu kwenye ukurasa wa kwanza na kuendelea ukurasa wa pili kuna taarifa inayosema kwamba Waziri Mkuu amedai kuwa wanaowania kugombea urais mwaka 2015 hawana akili nzuri.

  Gazeti la Tanzania Daima liliandika: “Mimi nimeshasema sitagombea ubunge, wala urais mwaka 2015, lakini mtu anayehaha kuutaka urais hawezi kuwa na akili nzuri hasa kama kweli anajua Ikulu anakwenda kufanya nini”.

  Habari hii haina ukweli wowote kwani Waziri Mkuu Mizengo Pinda alisema wanaoutaka urais hawajui ugumu wa kazi hiyo. Alichosema Waziri Mkuu ni hiki: “Wanaotaka urais hawajui urais ni kitu gani, waendelee nao, lakini mimi naona hapa (Ikulu) ni kazi ngumu tu kwa sababu hulali… napajua hapa, nimetumia sehemu kubwa ya maisha yangu ya utumishi nikiwa Ikulu.

  “Haiwezekani mtu ukautaka urais, isipokuwa kama unachofuata State House ni mazingira yake ama kujinufaisha na siyo kubebeshwa mzigo wa kusaidia Watanzania…”

  Katika habari hiyohiyo, mwandishi wa Tanzania Daima alimnukuu Waziri Mkuu akisema kwamba alikutana na Mhe. John Malecela na kumwambia kwamba anajiona ameutua mzigo mzito. Alichoandika mwandishi huyo:

  “Wakati Mwalimu Julius Nyerere anang’atuka siku moja tulikwenda nyumbani kwake Msasani. Tukiwa tumekaa naye, alikuwa anamtania John Malecela, akamwambia: ‘John, hapa nilipo naona kama kuna kitu kikubwa kimetoka mwilini mwangu, najiona mwepesi sana.’

  Katika mkutano wake na Wahariri wa vyombo vya habari, Jumatano, (Januari 25, 2012) hakumtaja kabisa Bw. John Malecela bali alimtaja Mama Joan Wickens ambaye alikuwa Msaidizi wa Mwalimu Nyerere (Personal Assistant) wakati huo.

  Alichosema Waziri Mkuu: “Labda niwape mfano, siku Rais Nyerere anang’atuka, alipotoka Uwanja wa Taifa kuagwa rasmi, alifika nyumbani akapanda juu, alipoteremka akatukuta watu watatu, mimi, Mzee Batao na Mama Joan Wickens. Mimi nilikuwa kijana wakati huo (1985), natumwa tu hamisha faili peleka hili pale…”

  “Mwalimu alimwambia msaidizi wake, Joan Wickens (marehemu), kwamba anajisikia faraja kama mtu aliyeondokewa na kitu fulani mwilini. Alionekana kama katua mzigo mzito uliokuwa unamwelemea…”

  Ofisi ya Waziri Mkuu inasikitishwa na taarifa hizo za uchochezi na upotoshaji. Ni vema mwandishi angeuliza kupata ufafanuzi na kupata usahihi wa majina yaliyotumiwa kabla ya kuchapisha habari hizo. Kama gazeti, Tanzania Daima lilipaswa lijiridhishe na usahihi wa habari zake kabla ya kuzichapisha kama inavyoelekeza misingi mikuu ya uandishi wa habari na weledi wa kazi hiyo.

  Uandishi wa habari za uongo hauna maana, unaleta hofu na unaweza kuchochea hisia ambazo hazipo bila sababu za msingi miongoni mwa wananchi. Na hiyo siyo kazi ya uandishi wa habari.

  (mwisho)

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  S. L. P. 3021,
  DAR ES SALAAM.
  IJUMAA, JANUARI 27, 2012
   
 2. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #2
  Jan 28, 2012
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,453
  Likes Received: 7,217
  Trophy Points: 280
  Hawa Tanzania Daima hawafai,juzi wametudanganya Raisi kaenda Sweden,kumbe Raisi alikwenda Suisse
   
 3. MAFILILI

  MAFILILI JF-Expert Member

  #3
  Jan 28, 2012
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,916
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Serikali hii imezidi uvumilivu, HIKI CHOMBO CHA CDM kipigwe marufuku kimezidi kuleta majungu kati ya wananchi na serikali halali iliyopo madarakani
   
 4. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #4
  Jan 28, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Kazi ya hizi kurugenzi za habari imekuwa ni kukanusha habari mahsusi, wala si kutoa habari, ukiangalia kanusho la habari mbili, moja tu inaweza kuwa imekosewa jina la muhusika, pinda anaposema wanaotaka urais hawajui......., amemaanisha kwa suala hilo ni wajinga!!!!!! tanzania daima liko sahihi 97%. Pinda punguza mikogo unapohutubu.
   
 5. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #5
  Jan 28, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135


  gazeti hili linapaswa kujirekebisha matatizo haya haya madogo mwisho wa siku yatakuwa makubwa Waandishi wawe makini na wanacho kiandika kwani si mara ya kwanza kulalamikiwa Hata Zitto alilalamika alipo kuwa India
   
 6. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #6
  Jan 28, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  Wanakimbizana na kivuli chao hao....badala kuhangaikia na kumtaka PM aende kuongea madaktari yeye anahangaika kupambana na media....aende akaongee na madaktari maana anaonekana hana uwezo kuendesha nchi au kutoa maamuzi magumu na mazito...hadi "raisi atue" ni ajabu sana kiongozi alie kulia ikulu na kuzeekea hapo anashindwa kuwa mamauzi sahihi hadi "rais atue"....ni aibu sana sana haina maana ya "Delegation of Authority"aliyopewa!!!!sijui kama hata anaelewa anachokifanya!!piga porojo tu
   
 7. J

  JokaKuu Platinum Member

  #7
  Jan 28, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,786
  Likes Received: 5,037
  Trophy Points: 280
  ..hao ni waandishi wanaolipualipua.

  ..kama mwandishi hakupata kumjua Mama Joan Wickens[r.i.p] alipaswa kuuliza habari zake, badala ya kupachika jina la Mzee Cygwiyemwisi John Malecela?
   
 8. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #8
  Jan 28, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Serikali iliyo nje ya madaraka inaheshimiwa na wananchi kuliko iliyoko madarakani. huwazuia wanaodai haki kwa mabom, maji ya kuwasha, virungu n.k, wawapelekee mabomu madaktari tuone!!!!
   
 9. F

  FJM JF-Expert Member

  #9
  Jan 28, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Alichosema Waziri Mkuu ni hiki: “Wanaotaka urais hawajui urais ni kitu gani, waendelee nao, lakini mimi naona hapa (Ikulu) ni kazi ngumu tu kwa sababu hulali… napajua hapa, nimetumia sehemu kubwa ya maisha yangu ya utumishi nikiwa Ikulu.

  “Haiwezekani mtu ukautaka urais, isipokuwa kama unachofuata State House ni mazingira yake ama kujinufaisha na siyo kubebeshwa mzigo wa kusaidia Watanzania…”

  Ofisi ya Waziri mkuu waache kulia kulia. Wajifunze siasa za ushindani na siku nyingine waziri mkuu achague maneno ya kusema kama hataki habari ipotoshwe. Ukisoma hapo kwenye red sijui anakanusha nini au alitaka mwandishi wa Tanzania Daima aandike 'neno kwa neno? Kama ndio next time atoe taarifa kama tangazo kwenye magazeti, hakuna atakaye 'potosha'.
   
 10. KIGENE

  KIGENE JF-Expert Member

  #10
  Jan 28, 2012
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 1,068
  Likes Received: 205
  Trophy Points: 160
  Haya anayokanusha Pinda ni vijimambo tu ngoma iko Muhimbili na kwinginelo ambako watu wanakufa kwa kukosa huduma lakini haya ya mtu kakosea spelling sijui kani misquote inamuathili nini Mtanzania ambaye hata hilo gazeti hataliona wala hana hata redio yakusikiliza nani kasema nini

  Hapa hakuna ubishi hafai kuwa Waziri Mkuu hachilia mbali urais kakiri mwenyewe kuwa hawezi lakini hata bila kusema maamuzi yake huwa yanadhihirisha uwezo wake ulivyo mdogo

  Sikumuelewa anaposema wanaowania urais ni wajinga je wasipojitokeza nchi itatawaliwa na nani je na huyo aliyemteua kwenye nafasi yake alikuwa mjinga kuwania urais na yeye Pinda alipoteuliwa uwaziri mkuu mbona hakuukataa au ni kazi isiyokuwa na majukumu yanayokaribiana na ya urais

  Ama kweli taifa limekosa viongozi wenye kuwajibika kujiamini na kulitumikia taifa letu Hivi marehemu Sokoine angeweza kutoa taarifa au mahojiano kama haya kwa vyombo vya habari Mungu ibariki Tanzania
   
 11. k

  kiche JF-Expert Member

  #11
  Jan 28, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 456
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  wepesi huu wa kupambana/kukanusha magazetini ungetumika pia kutoa maelezo ya maazimio 13 ya bunge yaliyobaki kuhusu richmond,rada,epa,meremeta na mengine yanayokera wananchi.
  Nyerere aliwai kusema kuwa serikali corrupt haiwezi kukusanya kodi itabaki kufukuzana na vibaiskeli mabarabarani huyu mzee alikuwa na uwezo wa kujua akili za watu! nami nimeamini kuwa serikali fisadi itakimbizana na kukanusha mambo madogo madogo kwenye magazeti na kuacha kushughulikia mambo ya msingi,kama si uwendawazimu kwa sasa ni lipi la kushughulikia udaku wa gazeti la tanzania daima au mgomo wa madaktari???
   
 12. M

  Mkwe21 JF-Expert Member

  #12
  Jan 28, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,852
  Likes Received: 492
  Trophy Points: 180
  Eeeh Mungu Tusaidie!! Why People Fighting with small issues and Not Big Ones??
   
 13. M

  Mkandara Verified User

  #13
  Jan 28, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Laaah mada hii imenipa somo la huyu mama JOAN WICKEN...Ni Watanzania wachache sana tunatambua mchango wake ktk ujenzi wa taifa letu..Naomba mjadala juu ya huyu mama kuwa PS wa mwalimu toka Uhuru hadi amefariki dunia..
   
 14. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #14
  Jan 28, 2012
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Katika gazeti lile la Tanzania Daima alichokosea mwandishi sio yale yaliyotamkwa na Pinda bali majina ya wahusika badala ya Joan Wickens ambaye nadhani hawa waandishi vijana hawakumfahamu ndio maana ikawa rahisi wao kudhani alimtaja John Malecela!! The problem with the article was name changes and not substance; Pinda is trying to jump the gun kwani alikuwa amekanyaga pabaya kuwaita wakina SITTA,EL ect wajinga!!
   
 15. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #15
  Jan 28, 2012
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mh Pinda shughulika na issue za taifa mf migomo ya madaktari
   
 16. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #16
  Jan 28, 2012
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Mimi naona ilikuwa ni ujinga wa viongozi wa mwanzo wa kiAfrika kupenda wanawake wa kizungu. Katika nchi zilizokuwa makoloni ya kifransa, viongozi walioa wazungu. Katika makoloni ya mwingereza waliwachukua kama sekritari, mfano ni Kwame na Nyerere.
   
 17. kaburungu

  kaburungu JF-Expert Member

  #17
  Jan 28, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 1,603
  Likes Received: 2,458
  Trophy Points: 280
  Yeah...uko sahihi kabisa Nyerere alikuwa kiongozi mwenye upeo mkubwa.. Nchi iko ICU wao wanakimblia mambo madogomadogo, wapi maisha bora kwa kila mtz..,wapi amani na utulivu wakati sina uhakika wa hata wa koroboi moja ya mafuta ya kula kwenye mchicha wangu, nauliza iwapi amani wakati watanzania tunanyanyaswa na mwekezaji mzungu anaelindwa na serikali... Waje kutolea ufafafanuzi wa mambo ka haya na sio hizo blabla zao.
   
 18. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #18
  Jan 28, 2012
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Tangu mhariri wao atinge mahakamani mambo yamekuwa ovyo.
   
 19. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #19
  Jan 28, 2012
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Tatizo la serikali yetu ni kutaka kuonekana iko safi sana wakati ilishachafuka kitambo!!
   
 20. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #20
  Jan 28, 2012
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Je Nyerere alikuwa anajua kukusanya kodi? Katika enzi zake migomo ilikuwa marufuku. Kulikuwa hakuna vyombo vya habari binafsi.

  Kama angekuwa kiongozi jasiri, angeruhusu migomo, uhuru wa vyombo vya habari, na baadaye angetuachia mifano ya kutatua matatizo.
   
Loading...