Uzalendo wa Kitanzania
JF-Expert Member
- Mar 8, 2020
- 2,156
- 4,510
Weledi, Uchapakazi na Uzalendo
Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali ya Awamu ya Tano imeokoa Tsh Trilioni 11.4 baada ya kushinda kesi mbalimbali zilizofunguliwa ndani na nje ya Nchi dhidi ya Serikali ya Tanzania.
Aidha Ofisi hiyo imefanikiwa kurejesha Serikalini mali mbalimbali zilizochukuliwa kwa njia zisizo halali ikiwemo mashamba 106, Viwanja, Hoteli na nyumba mbalimbali ikiwemo Hoteli ya Mbeya.
Gabriel Malata - Wakili Mkuu wa Serikali
======
WAKILI Mkuu wa Serikali, Gabriel Malata amesema serikali imefanikiwa kuokoa zaidi ya Sh trilioni 11.4 kwa miaka miwili kutokana na uendeshaji madhubuti wa mashauri ndani na nje ya nchi.
Malata amesema hayo leo wakati akitoa taarifa kwa Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Mwigulu Nchemba aliyetembelea ofisi yake.
Wakili huyo mkuu amesema miongoni mwa mafanikio yametokana na kushinda kesi zilizofunguliwa nchini Afrika Kusini na Canada.
Amesema fedha hizo zingeweza kulipwa kwa watu wasiostahili.
CHANZO: Habari Leo (August 2020)