mwanamichakato
JF-Expert Member
- Mar 20, 2015
- 1,169
- 1,073
Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi imekuwa ikifanya kazi nzuri sana ya kuhakikisha wananchi wa Tanzania na mali za watanzania vipo salama lakini zaidi amani,usalama,utulivu vikiendelea kila iitwapo leo kupitia taasisi zake kama Jeshi La Polisi,Jeshi la Magereza,Idara ya wakimbizi,Jeshi/Idara ya Uhamiaji,Jeshi la zimamoto na uokoaji.Pamoja na taasisi tajwa Wizara ya hii ndio yenye jukumu la kusajiri vyama vya kijamii zikiwemo taasisi za dini {makanisa,Huduma za kiroho,Misikiti,vyama vya kidini na madhehebu}.
Taasisi nyingi za kidini zimekuwa na mchango mkubwa katika kuijenga jamii bora ya Watanzania na wasio watanzania.Kumekuwepo na ukengeufu mkubwa wa misingi ya uanzishwaji {usajiri} wa taasisi nyingi hasa mapato na mali vinapoongezeka { kupitia sadaka na matoleo ya waumini au waaminio}kwa baadhi ya waanzirishi kutoka nje ya msingi,makusudi na makusudio hivyo kuibua migogoro inayokuwa na lengo la kujinufaisha ama kukidhi matakwa nje ya mapenzi ya Mungu.
Usumbufu mkubwa sana umekuwa ukitokea na kuwakumba waumini wa madhehebu husika katika taasisi za dini zenye migogoro na hasa wanapokuwa wamejitoa kwa hali,mali,fedha,dhahabu,Vito vya thamani kupitia sadaka,dhaka,fungu la kumi,malimbuko n.k
Ni kweli kumekuwepo na migogoro mingi ndani ya taasisi za kidini makanisa yakiwemo.Ukifuatilia utavumbua ya kuwa mingi ya migogoro chanzo chake ni tamaa ya madaraka,tamaa ya mali,tamaa za miili .Hivyo ni wazi migogoro,mitafaruku husika imekuwa ikisababishwa na wacha Mungu wa kweli dhidi ya wacha Mungu wenye kiu ya utajiri/anasa/matumizi mabaya ya rasilimali zinazopatikana kwa mgongo wa dini,dhehebu,kanisa,msikiti...n.k
Migogoro inapoibuka katika taasisi za dini {Misikiti,makanisa,madhehebu,Huduma} ofisi ya msajiri wa vyama vya kijamii iliopo chini ya kurugenzi ya Sheria katika Wizara ya Mambo ya ndani imekuwa ikihusishwa katika kutafsiri katiba za taasisi husika,Kupatanisha pande husika,kushauri pande husika,na kwa ujumla kutatua figisufigisu na migogoro kwa maslahi ya amani,usalama na mshikamano katika nchi.
Kwa muda mrefu sana kumekuwepo na tuhuma lukuki zinazoelekezwa kwenye ofisi hii zikihusisha matumizi mabaya ya madaraka kwa baadhi ya maofisa katika kushughulikia kero,malalamiko,migogoro kwa kuegemea upande mmoja pasipo haki/kweli na uzingatiaji wa sheria,kanuni,mila,desturi na hekima kwa sababu ya rushwa {Mfano wa viwango vya rushwa zinazosemekana kutolewa ni kuanzia milioni 10,20,30,50,60,70,100,150,200 n.k kutegemeana na ukwasi wa taasisi/pande husika} na ukosefu wa maadiri.
Maamuzi yasio ya haki na ukweli yamekuwa na athari kubwa kwenye taasisi za dini {makanisa/huduma} hivyo kuhatarisha kwa kiwango kikubwa amani na usalama kwa watanzania wenye kuguswa /kuumizwa/kuteswa/kuibiwa/kugandamizwa /huduma na baadhi ya viongozi matumizi ya rushwa kubwa na ndogo ambazo msingi wake ni sadaka,matoleo,dhaka zitolewazo na waumini.Mfano wa Migogoro inayogusa maamuzi ya taasisi tajwa ni Mgogoro wa msikiti wa Mwembechai,Kanisa la Moravian,Assemblies of God,Anglican Church,FGBFC,na mengineo mingi inayoendelea sasa chini kwa chini.
Ni wito wangu kwa Wizara na taasisi mtambuka kufuatilia hili kwa karibu sana na kupata ukweli kisha kuchukua hatua stahiki kwa wahusika wenye kutumia madaraka yao vibaya .Pia kuchukua hatua stahiki dhidi ya viongozi wa taasisi za kidini wenye kujinufaisha binafsi kwa mgongo wa kunyonya,kudanganya,kutapeli waumini wenye kiu ya kumtafuta Mungu.Ifike wakati taasisi hizi za kidini ziundiwe sheria nzuri ya udhibiti inayoweza kuepusha matumizi mabaya ya madaraka yasio na tija kwa waumini {itakayolinda zaidi maslahi/matakwa ya waumini/wanachama dhidi ya waanzirishi hasa wanapopotoka au wanapopotosha maslahi ya taifa na wengi dhidi ya maslahi binafsi.