Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS) yaikana ripoti ya Twaweza; wadai haiwatambui na tafiti zao hivyo sio halali

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imekana kushirikishwa katika ufanyaji wa utafiti unaodaiwa kufanywa na Twaweza hivyo haiutambui.

Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Kijamii wa NBS, Ephraim Kwesigabo amesema, ofisi yake haikushirikishwa kwa namna yoyote kuhusu utafiti huo sheria inavyotaka.

“Hatujatoa kibali cha utolewaji wa hizo takwimu na hakuna mahala ambapo tumeshirikishwa kuhusu utafiti huo,” amesema.

Sheria ya Takwimu inatoa mamlaka kwa NBS pekee kusimamia masuala yote ya takwimu rasmi nchini na imeipa uwezo wa kuzipa taasisi, NGO na wakala nyingine, uwezo wa kufanya tafiti za takwimu rasmi kwa kufuata vigezo ilivyoweka
 
Mkuu yani kabisa ulitegemea Mama Dr. ALBINA Chuwa na ile ongea yake taasisi anayoiongoza iseme tofauti na hili? Hahahahhaa acha utani
 
Back
Top Bottom