Benny Haraba
JF-Expert Member
- Dec 7, 2012
- 8,385
- 6,350
Ukweli utabaki kuwa kweli tu ''when you leave in a glass house do not throw stones''
tupinge mara ngapi ?Hapa ndio naiona kazi ya sheria ya takwimu waziwazi,sasa pinga kinachosemwa uone kazi
Mnataka sema kuwa Serikalini haijapungua ila Kwetu ndio zimepungua. Mkisema walioajiriwa ni 22mil maana yake Nusu ya Watanzania wameajiriwa....
Hamjui Nusu ya Watanzania karibia 25mil ni under 18?
Hamjui kuwa wazee 55 na kuendelea ni zaidi ya 10mil
Kwanini ikiguswa serikali mnakuwa wakali sana?
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUKANUSHA HABARI ILIYOSAMBAZWA KATIKA MITANDAO YA KIJAMII YA KUPUNGUA KWA AJIRA SERIKALINI
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) inakanusha habari iliyosambazwa katika baadhi ya mitandao ya kijamii hususan Jamii Forum yenye kichwa cha habari “NBS yakiri ajira sekta binafsi zimepungua kwa 42.6%, Serikalini zimepungua kwa 78.1% ndani ya mwaka mmoja."
Habari hii imepotosha kuhusu kupungua kwa ajira Serikalini na hivyo jamii inaombwa kuipuuza kwa kuwa haina ukweli wowote.
Ifahamike kwamba, wakati NBS ikijiandaa kufanya utafiti wa Watu wenye Uwezo wa Kufanya Kazi (Intergrated Labour Force Survey) utakaofanyika mwaka 2019/20, ilifanya maoteo mwaka 2018 (projections) ya mwenendo wa hali ya Soko la Ajira Nchini ambayo yanabainisha mabadiliko yaliyotokea katika soko la ajira tangu mwaka 2014 hadi mwaka 2018. Taarifa hii inapatikana kwenye tovuti ya NBS (www.nbs.go.tz - Tanzania in Figures 2018 Uk. 40).
Maoteo ya takwimu hizo yanaonesha kuwa, idadi ya watu walio na ajira imeongezeka kutoka milioni 20.0 mwaka 2014 hadi milioni 22.0 mwaka 2018.
Aidha, takwimu zilizowekwa kwenye Tanzania in Figure 2018 Uk. 41 zinazotokana na taarifa za kiutawala (administrative records) ambazo zinasaidia kupata takwimu za ajira ambazo hazikusanywi kwenye tafiti za kawaida. Takwimu hizi hutumika pia kama kigezo cha kufanya maoteo ya hali ya ajira (proxy indicators) katika vipindi ambavyo hakuna tafiti zilizofanyika ili kutoa hali ya soko la ajira katika vipindi vifupi vifupi na vya kati.
Tafsiri halisi ya Jedwali lililopo uk. 41 wa Tanzania in Figures ni kwamba, mwaka 2017/18 kulikuwa na jumla ya ajira 552,063 zilizozalishwa nchini ikilinganishwa na ajira 453,466 kwa mwaka 2016/17. Hili ni ongezeko la ajira 98,597 sawa na asilimia 21.7 kati ya mwaka 2016/17 na mwaka 2017/18.
Kati ya ajira 552,063 zilizozalishwa nchini mwaka 2017/18, ajira 415,009 sawa na asilimia 75.0 zilikuwa ni ajira kutoka Serikalini; ajira hizi zinajumuisha ajira 18,000 kutoka Serikali Kuu na ajira 397,009 kutoka katika miradi ya maendeleo kupitia Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2016/17 hadi 2020/21.
Hali hii inatokana na ukweli kuwa, wananchi wengi huajiriwa kwenye miradi ya kimkakati ya maendeleo inayoendelea hapa nchini ambapo Serikali imejikita kwa dhati kuitekeleza kwa ajili ya kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 na kupunguza umaskini.
Kwa upande mwingine, ajira 137,054 sawa na asilimia 25.0 ya ajira zote zilizozalishwa na Sekta Binafsi zimepungua kutoka ajira 239,017 mwaka 2016/17 hadi ajira 137,054.
Hivyo, hali halisi kwa jedwali hilo ni kuongezeka kwa ajira Serikalini kutoka 214,449 mwaka 2016/17 hadi 415,009 mwaka 2017/18 sawa na ongezeko la ajira 200,560 (asilimia 94) ya ajira zilizozalishwa mwaka 2016/17.
Ikumbukwe kwamba, Ofisi ya Taifa ya Takwimu hutumia taarifa za kiutawala za ajira kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu; Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu kubaini kiwango cha ajira zilizozalishwa kwa kila mwaka. Huu ndio uzoefu wa nchi nyingi duniani hususan nchi za Afrika.
Utafiti wa Watu wenye Uwezo wa Kufanya Kazi hufanyika kila baada ya miaka mitano ambapo kwa mara ya mwisho ulifanyika mwaka 2014 wakati Utafiti wa Ajira na Mapato katika Sekta Rasmi hufanyika kila mwaka na kwa mara ya mwisho ulifanyika mwaka 2016.
Takwimu hizi za ajira hukusanywa na viashiria mbalimbali vya ajira (Labour Market Indicators) na hutolewa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na Shirika la Kazi Duniani (ILO) zikiwa na lengo la kufuatilia na kutathmini sera zilizowekwa na Serikali katika Soko la Ajira.
Mwisho, Ofisi ya Taifa ya Takwimu inausisitiza Umma kupuuza habari hiyo potofu ya kupungua kwa ajira Serikalini na inatoa wito kwa wananchi kuendelea kufanya kazi kwa bidii na maarifa zaidi ili kuunga mkono juhudi zinazoendelea za kujenga uchumi. Aidha, NBS inawaasa wachambuzi wote kufuata matakwa ya Sheria ya Takwimu ya mwaka 2015 kila wanapofanya uchambuzi wa takwimu mbalimbali.
Imetolewa na:
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS),
DODOMA
14 Agosti 2019
View attachment 1181119
View attachment 1181120
Kuhusu habari inayolalamikiwa, soma:
Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS) yakiri ajira sekta binafsi zimepungua kwa 42.6%, serikalini zimepungua kwa 78.1% ndani ya mwaka mmoja
NBS Report “Tanzania in Figure 2018” Agosti 10, 2019 Kwa kifupi. Ajira rasmi zilizotengenezwa na sekta binafsi zimepungua kutoka 239,017 mwaka 2016/2017 hadi kufikia ajira 137,054 mwaka 2017/2018. Pia ajira rasmi zilizotengenezwa na Serikali zilipungua kutoa 82,302 hadi 18,000 ikiwa ni sawa na...www.jamiiforums.com
Wapumbavu sana, eti Watanzania 22m wameajiliwa. Tena ni Mashetani wa kufa mtu. Mimi hata kama sina utafiti nakuambia waalimu wako laki 7, polisi laki 8, JW wako milioni 1, magereza wako laki 3, manesi wauguzi na madokta laki 6, wafanyakazi wengine wote laki 7. Haya jumla inakuwa 4.1m. ukija sekata binafsi utakuta wako 3m hapo jumla unapata 7.1m. Wapumbavu hao eti milioni 22, hata uongo hawawezi. Na hapo nimekupa idadi kabla ya vyeti feki kupita. Ukiweka vyeti feki basi watabaki jumla 3m walioajiliwa serikalini.
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUKANUSHA HABARI ILIYOSAMBAZWA KATIKA MITANDAO YA KIJAMII YA KUPUNGUA KWA AJIRA SERIKALINI
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) inakanusha habari iliyosambazwa katika baadhi ya mitandao ya kijamii hususan Jamii Forum yenye kichwa cha habari “NBS yakiri ajira sekta binafsi zimepungua kwa 42.6%, Serikalini zimepungua kwa 78.1% ndani ya mwaka mmoja."
Habari hii imepotosha kuhusu kupungua kwa ajira Serikalini na hivyo jamii inaombwa kuipuuza kwa kuwa haina ukweli wowote.
Ifahamike kwamba, wakati NBS ikijiandaa kufanya utafiti wa Watu wenye Uwezo wa Kufanya Kazi (Intergrated Labour Force Survey) utakaofanyika mwaka 2019/20, ilifanya maoteo mwaka 2018 (projections) ya mwenendo wa hali ya Soko la Ajira Nchini ambayo yanabainisha mabadiliko yaliyotokea katika soko la ajira tangu mwaka 2014 hadi mwaka 2018. Taarifa hii inapatikana kwenye tovuti ya NBS (www.nbs.go.tz - Tanzania in Figures 2018 Uk. 40).
Maoteo ya takwimu hizo yanaonesha kuwa, idadi ya watu walio na ajira imeongezeka kutoka milioni 20.0 mwaka 2014 hadi milioni 22.0 mwaka 2018.
Aidha, takwimu zilizowekwa kwenye Tanzania in Figure 2018 Uk. 41 zinazotokana na taarifa za kiutawala (administrative records) ambazo zinasaidia kupata takwimu za ajira ambazo hazikusanywi kwenye tafiti za kawaida. Takwimu hizi hutumika pia kama kigezo cha kufanya maoteo ya hali ya ajira (proxy indicators) katika vipindi ambavyo hakuna tafiti zilizofanyika ili kutoa hali ya soko la ajira katika vipindi vifupi vifupi na vya kati.
Tafsiri halisi ya Jedwali lililopo uk. 41 wa Tanzania in Figures ni kwamba, mwaka 2017/18 kulikuwa na jumla ya ajira 552,063 zilizozalishwa nchini ikilinganishwa na ajira 453,466 kwa mwaka 2016/17. Hili ni ongezeko la ajira 98,597 sawa na asilimia 21.7 kati ya mwaka 2016/17 na mwaka 2017/18.
Kati ya ajira 552,063 zilizozalishwa nchini mwaka 2017/18, ajira 415,009 sawa na asilimia 75.0 zilikuwa ni ajira kutoka Serikalini; ajira hizi zinajumuisha ajira 18,000 kutoka Serikali Kuu na ajira 397,009 kutoka katika miradi ya maendeleo kupitia Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2016/17 hadi 2020/21.
Hali hii inatokana na ukweli kuwa, wananchi wengi huajiriwa kwenye miradi ya kimkakati ya maendeleo inayoendelea hapa nchini ambapo Serikali imejikita kwa dhati kuitekeleza kwa ajili ya kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 na kupunguza umaskini.
Kwa upande mwingine, ajira 137,054 sawa na asilimia 25.0 ya ajira zote zilizozalishwa na Sekta Binafsi zimepungua kutoka ajira 239,017 mwaka 2016/17 hadi ajira 137,054.
Hivyo, hali halisi kwa jedwali hilo ni kuongezeka kwa ajira Serikalini kutoka 214,449 mwaka 2016/17 hadi 415,009 mwaka 2017/18 sawa na ongezeko la ajira 200,560 (asilimia 94) ya ajira zilizozalishwa mwaka 2016/17.
Ikumbukwe kwamba, Ofisi ya Taifa ya Takwimu hutumia taarifa za kiutawala za ajira kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu; Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu kubaini kiwango cha ajira zilizozalishwa kwa kila mwaka. Huu ndio uzoefu wa nchi nyingi duniani hususan nchi za Afrika.
Utafiti wa Watu wenye Uwezo wa Kufanya Kazi hufanyika kila baada ya miaka mitano ambapo kwa mara ya mwisho ulifanyika mwaka 2014 wakati Utafiti wa Ajira na Mapato katika Sekta Rasmi hufanyika kila mwaka na kwa mara ya mwisho ulifanyika mwaka 2016.
Takwimu hizi za ajira hukusanywa na viashiria mbalimbali vya ajira (Labour Market Indicators) na hutolewa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na Shirika la Kazi Duniani (ILO) zikiwa na lengo la kufuatilia na kutathmini sera zilizowekwa na Serikali katika Soko la Ajira.
Mwisho, Ofisi ya Taifa ya Takwimu inausisitiza Umma kupuuza habari hiyo potofu ya kupungua kwa ajira Serikalini na inatoa wito kwa wananchi kuendelea kufanya kazi kwa bidii na maarifa zaidi ili kuunga mkono juhudi zinazoendelea za kujenga uchumi. Aidha, NBS inawaasa wachambuzi wote kufuata matakwa ya Sheria ya Takwimu ya mwaka 2015 kila wanapofanya uchambuzi wa takwimu mbalimbali.
Imetolewa na:
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS),
DODOMA
14 Agosti 2019
View attachment 1181119
View attachment 1181120
Kuhusu habari inayolalamikiwa, soma:
Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS) yakiri ajira sekta binafsi zimepungua kwa 42.6%, serikalini zimepungua kwa 78.1% ndani ya mwaka mmoja
NBS Report “Tanzania in Figure 2018” Agosti 10, 2019 Kwa kifupi. Ajira rasmi zilizotengenezwa na sekta binafsi zimepungua kutoka 239,017 mwaka 2016/2017 hadi kufikia ajira 137,054 mwaka 2017/2018. Pia ajira rasmi zilizotengenezwa na Serikali zilipungua kutoa 82,302 hadi 18,000 ikiwa ni sawa na...www.jamiiforums.com
yaani wanatuona mabwege sana ! hivi hii ndio ajira kweli ?Kwamba 2017/2018 kulikua na ajira 400,000 za seeikali hahahah hawa jamaa bila shaka watakua wamejumuisha wamachinga, mama ntilie, yani hata upikeje data huwezi pata hizo ajira 400,000+ kwa mwaka huo
Hata mtoto wa form one anajua ile point ya "lack of employment"
Andiko la Quinine hapa ukumbini kuhusu kupungua ajira serikalini na sekta binafsi lilizua mjadala mrefu hadi ikalazimu NBS kukanusha maelezo ya Quinine kwa kueleza kuwa ametafsiri vibaya takwimu zilichapishwa katika kitabu cha Tanzania in Figures cha mwaka 2018. Lakini hata pale NBS ilipotoa ufafanuzi bado mjadala unaendelea. Sasa Quinine imekuwa kama vile Cloroquine yaani kila mgonjwa anapopata nafuu ya ugonjwa wa malaria ndivyo mwili unavyozidi kuwasha! Maana naona mjadala hausimami lakini zaidi hofu yangu unakwenda arijojo.TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUKANUSHA HABARI ILIYOSAMBAZWA KATIKA MITANDAO YA KIJAMII YA KUPUNGUA KWA AJIRA SERIKALINI