Ofisi ya Rais-Utumishi kutekeleza kwa wakati maelekezo ya Rais ya kupandisha mishahara ya watumishi

Monica Mgeni

Member
Oct 7, 2021
82
134
OFISI YA RAIS-UTUMISHI KUTEKELEZA KWA WAKATI MAELEKEZO YA MHE. RAIS YA KUPANDISHA MISHAHARA YA WATUMISHI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Jenista Mhagama amesema ofisi yake imejipanga kupandisha mishahara ya Watumishi wa Umma kwa wakati kama alivyoelekeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani 2022 yaliyofanyika kitaifa jijini Dodoma.

Akizungumzia utekelezaji wa maelekezo ya kuwapandisha mishahara Watumishi wa Umma, Mhe. Jenista amesema ofisi yake itafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha ifikapo Julai, 2022 kila mtumishi wa umma anapata mshahara mpya. Hivyo amewataka watumishi wa umma kuwa watulivu wakati zoezi hili likiendelea kushughulikiwa na Serikali.

“Mimi na watendaji wangu tumeanza kupitia taarifa za Watumishi katika Mfumo wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara ili kushirikiana na Wizara ya Fedha katika kukamilisha zoezi la kupandisha mishahara ya Watumishi wa Umma, itakapofika Julai 2022 kila mtumishi atakuwa amepata mshahara mpya kama ilivyoelekezwa na Mhe. Rais,” Mhe. Jenista amesisitiza.

Mhe. Jenista ameongeza kuwa ahadi ambazo Mhe. Rais amekuwa akizitoa kwa watumishi wa umma zimekuwa zikitekelezwa kwa wakati, hivyo jambo hili la mishahara litatekelezwa kama alivyokusudia.

Katika kuhakikisha mishahara ya watumishi wa umma inapanda kwa mujibu wa maelekezo ya Mhe. Rais, Waziri Jenista amewataka Maafisa Utumishi wote katika taasisi za umma nchini kuhakikisha wanatekeleza ipasavyo kila mwongozo utakaotolewa na ofisi yake kwa lengo la kukamilisha zoezi la upandishaji wa mishahara ya watumishi.

“Maafisa Utumishi hakikisheni mnatekeleza maelekezo yatakayotolewa na ofisi yangu kwa uzalendo na uadilifu wa hali ya juu kwani atakayekwenda kinyume hatua kali zitachukuliwa dhidi yake kwa kukiuka maelekezo halali ya Mhe. Rais,” Mhe. Jenista ameongeza.

Akizungumzia utekelezaji wa maelekezo mengine aliyoyatoa Mhe. Rais likiwemo la watumishi walioondolewa kutokana na vyeti vya kughushi, Mhe. Jenista amesema wameshafanya mawasiliano na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii
 
Tuendelee kulipana tu maana nchi nyingine nazo wanatusubiri kwenye issue za maendeleo.

Tutapitwa mpaka na Burundi sisi tumekalia siasa tu kila kitu.
 
Uzuri hajasema atapandisha Kwa asilimia ngapi. Tufanye kwamba atapandisha 20% na makofi yatapigwa kama Wakenya walivyofurahi. Mwenye gross ya 1,000,000 atapandishwa hadi 1,200,000. Sasa Anza makato ya PAYE, NSSF, NHIF, n.k ndo ujiandae kisaikolojia.
 
Shame on you! KWANINI UMEKOP ANDIKO LA MR. Q? Ama kweli wewe ni MASKINI wa fikra!
 
Waseme hadharani watapandisha kwa % ngapi! Nje ya hapo ni siasa tu.
 
Kazi inaendelea 👇

Screenshot_20220511-082210.png
 
Uzuri hajasema atapandisha Kwa asilimia ngapi. Tufanye kwamba atapandisha 20% na makofi yatapigwa kama Wakenya walivyofurahi. Mwenye gross ya 1,000,000 atapandishwa hadi 1,200,000. Sasa Anza makato ya PAYE, NSSF, NHIF, n.k ndo ujiandae kisaikolojia.

Kwani hayo makato hayakuwepo kabla?
 
Mh. Mhagama, achana na issue ya kupanda mwa mishahara uangalie Ile sheria Yako kandamizi ya mafao ya wastaafu kulipwa mafao Yao Kwa 25% ambayo Magufuli aliahirisha utekelezaji wake Hadi 2023.
Na hata juzi mh. Rais aliwarai muiangalie ili angalau iwe 33%.
Binafsi siuoni umuhimu wa sheria ili zaidi ya ubatili wake. Kwanini ninyi wanasiasa mnapomaliza session moja ya binge mnalipwa mafao yote bila kubaniwa? Iweje linalowezekana Kwa wabunge lishindwe Kwa wastaafu wa kada nyingine?
Hiyo fedha mnayobaki nayo mtakuwa mnawalipa na riba yake?
Nikushauri TU Kwa manufaa mapana ya wastaafu watarajiwa hebu peleka mswada wa marekebisho ya sheria hiyo na ikiwapendeza wabunge waifutilie mbali kwani ipo kinyume kabisa na haki za binadamu.
 
Umeongea point
 
OFISI YA RAIS-UTUMISHI KUTEKELEZA KWA WAKATI MAELEKEZO YA MHE. RAIS YA KUPANDISHA MISHAHARA YA WATUMISHI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Jenista Mhagama amesema ofisi yake imejipanga kupandisha mishahara ya Watumishi wa Umma kwa wakati kama alivyoelekeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani 2022 yaliyofanyika kitaifa jijini Dodoma.

Akizungumzia utekelezaji wa maelekezo ya kuwapandisha mishahara Watumishi wa Umma, Mhe. Jenista amesema ofisi yake itafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha ifikapo Julai, 2022 kila mtumishi wa umma anapata mshahara mpya. Hivyo amewataka watumishi wa umma kuwa watulivu wakati zoezi hili likiendelea kushughulikiwa na Serikali.

“Mimi na watendaji wangu tumeanza kupitia taarifa za Watumishi katika Mfumo wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara ili kushirikiana na Wizara ya Fedha katika kukamilisha zoezi la kupandisha mishahara ya Watumishi wa Umma, itakapofika Julai 2022 kila mtumishi atakuwa amepata mshahara mpya kama ilivyoelekezwa na Mhe. Rais,” Mhe. Jenista amesisitiza.

Mhe. Jenista ameongeza kuwa ahadi ambazo Mhe. Rais amekuwa akizitoa kwa watumishi wa umma zimekuwa zikitekelezwa kwa wakati, hivyo jambo hili la mishahara litatekelezwa kama alivyokusudia.

Katika kuhakikisha mishahara ya watumishi wa umma inapanda kwa mujibu wa maelekezo ya Mhe. Rais, Waziri Jenista amewataka Maafisa Utumishi wote katika taasisi za umma nchini kuhakikisha wanatekeleza ipasavyo kila mwongozo utakaotolewa na ofisi yake kwa lengo la kukamilisha zoezi la upandishaji wa mishahara ya watumishi.

“Maafisa Utumishi hakikisheni mnatekeleza maelekezo yatakayotolewa na ofisi yangu kwa uzalendo na uadilifu wa hali ya juu kwani atakayekwenda kinyume hatua kali zitachukuliwa dhidi yake kwa kukiuka maelekezo halali ya Mhe. Rais,” Mhe. Jenista ameongeza.

Akizungumzia utekelezaji wa maelekezo mengine aliyoyatoa Mhe. Rais likiwemo la watumishi walioondolewa kutokana na vyeti vya kughushi, Mhe. Jenista amesema wameshafanya mawasiliano na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii
Naona hapa mchumi namba moja hakushirikishwa kama kwenye mafuta na tozo. Mambo yakaenda sawa.
 
Hongereni watumishi, hiyo nyongeza tunaisubiri mtaani tuile wote
 
Back
Top Bottom