Ofisi Ya Pinda Yakanusha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ofisi Ya Pinda Yakanusha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mpita Njia, Apr 11, 2008.

 1. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #1
  Apr 11, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda hajasema kuwa Tanzania iko tayari kupeleka jeshi Zimbabwe kama ilivyoandikwa kwa makosa katika gazeti la kila siku la Kiingereza linalochapishwa Dar es Salaam THE CITIZEN toleo la leo (Ijumaa Apr. 11, 200.

  Alichosema Waziri Mkuu katika Bunge mjini Dodoma jana (Alhamisi Apr. 10, 200 asubuhi wakati wa kipindi cha Maswali kwa Waziri Mkuu kujibu swali la Mbunge Zitto Kabwe (Chadema) ni kwamba kama ni kupeleka jeshi Zimbabwe basi uamuzi huo utakuwa wa Umoja wa Afrika (AU).

  "Kama ni lazima kupeleka jeshi mimi nasema kama ni lazima AU nina hakika itakaa chini itatazama what to do (nini cha kufanya) na kama hapana budi watafanya hivyo," alisema.

  Katika swali lake kuhusu hali ya Zimbabwe, Mbunge Kabwe aliuliza kutaka kujua kuwa endapo Jumuiya ya Uchumi ya Kusini mwa Afrika (SADC) iliyotakiwa ikutane kujadili suala la Zimbabwe itaamua kupeleka jeshi la kulinda amani nchini humo kufuatia utata katika matokeo ya uchaguzi, Tanzania itakuwa tayari kupeleka jeshi kama ilivyopeleka Comoro.

  Katika gazeti hilo la THE CITIZEN, kwenye habari ya ukurasa wa kwanza, iliandikwa kwa kichwa cha maneno "Dar ready for military action in Zimbabwe", ikimaanisha kuwa Tanzania iko tayari kuchukua hatua za kijeshi Zimbabwe, jambo ambalo kamwe halikuzungumzwa na Waziri na Waziri Mkuu Pinda.

  Swali la Mbunge Kabwe na majibu ya Waziri Mkuu, kama yalivyonakiliwa kama yalivyo, katika taarifa rasmi ya Bunge ambayo hupatikana Ofisi ya Bunge ni kama ifuatavyo:-

  "MHE. KABWE ZUBERI ZITTO: Mheshimiwa Waziri Mkuu kuhusu Zimbabwe. Mheshimiwa Waziri Mkuu (nchi) yetu imekuwa katika juhudi mbalimbali za kimataifa za kuleta amani, leo tunavyozungumza ni wiki ya pili toka uchaguzi ufanyike Zimbabwe matokeo hayajatangazwa na kuna juhudi dhahiri kabisa Chama cha ZANU-PF ambacho ni marfiki wa chama chako kukataa kukubaliana na matokeo yatakavyokuwa. Serikali ya Tanzania inasemaje kuhusiana na uchaguzi wa Zimbabwe?

  WAZIRI MKUU: Haya ningekuwa na uwezo wa kukuuliza na mimi ningesema Kabwe unanishauri nini? Tuseme nini wote (Kicheko/Makofi).

  Mheshimiwa Spika, suala la Zimbabwe ni kitendawili si kwa Serikali ya Tanzania lakini ninaweza kusema kwa Afrika yote na ninaweza kusema hata kwa International Community yote, si jambo linalopendeza hata kidogo yaani halipendezi hata kidogo. Na unapokwenda kumsaidia mtu si lazima aonyeshe dalili za kukuomba kwamba Mzee njoo unisaidie kama hujaombwa unaweza ukainuka tu akakwambia nani kakutuma?

  Kwa hiyo, unalolisema ni concern (kuhusika) kwa kila mtu sisi wote hapa we are very much concerned (tunahusika sana) lakini aah! mimi nasema ngoja tungoje tuone litakalotokea ni nini.

  Tunaye Mwenyekiti wa Nchi za SADC (Jumuiya ya Uchumi ya Nchi za Kusini mwa Afrika) kwa hiyo nadhani pengine inaweza ikawa ni kiungo cha karibu zaidi kuliko pengine hata Chairman (Mwenyekiti) wa AU (Umoja wa Afrika). Lakini ni kweli Tanzania sisi tume play role (shiriki) kubwa sana kwa uhuru wa Zimbabwe aah! sasa tungoje tuone litatokea nini maana mimi sina jibu la harakaharaka kwenye eneo hili hata kidogo. (Makofi)

  MHE. KABWE ZUBERI ZITTO: Mheshimiwa Spika, mara nyingi tumekuwa tukingoja matokeo yake maafa yanatokea na hiyo huo ni mfano ambao ulitokea Kenya.

  Lakini Mheshimiwa Waziri Mkuu keshokutwa SADC wanakutana iwapo SADC wataamua kupeleka jeshi Zimbabwe kwa ajili ya kuhakikisha kwamba tunaweka amani na aliyeshinda uchaguzi anapewa haki yake ya kushinda. Tanzania itakuwa tayari kupeleka Jeshi kama ilivyopeleka Comoro? (Kicheko).

  WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, bahati nzuri umeliweka vizuri kwamba je kama itaonekana kwamba aliyeshinda uchaguzi na Serikali inaombwa kwenda kuhakikisha huyo aliyeshinda na mifumo mingine inaendelea kazi zake kwa salama bila ya matatizo je Serikali itakuwa tayari kuridhia jambo hili.

  Kwa sababu msingi wake mkubwa unanzia hapo lakini so far (mpaka sasa) hatujui nani mshindi lakini tuna taarifa za juu juu tu juu ya jambo hili kwa hiyo mimi nadhani tungoje International Pressure (shinikizo la kimataifa) na mimi najua ipo kubwa, tutakapopata a breakthrough (ufumbuzi) na kwa kweli kama ni lazima kupeleka jeshi nasema kama ni lazima AU nina hakika itakaa chini itatazama what to do (nini cha kufanya) na kama hapana budi watafanya hivyo. (Makofi)"

  (mwisho)

  Imetolewa na:

  Ofisi ya Waziri Mkuu,

  S.L.P. 3021,

  DAR ES SALAAM

  Ijumaa Apr. 11, 2008
   
 2. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #2
  Apr 11, 2008
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Bora maana wengine tulianza kuogopa kwamba yaani PM wetu anaweza akawa mtupu kiasi hicho!!?
   
 3. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #3
  Apr 11, 2008
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Huyu Pinda naye utamweza?

  Mimi hapa nilishanawa mikono siku nyingi sana? Hata hivyo bado nitamkaribisha kwenye babikyu akija marekani!
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Apr 11, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Ndiyo haya yaliyosemwa Rais kasema "Sitovunja Baraza la Mawaziri" wakati hakusema; kule KLH tuliripoti correctly kutoka vyanzo hivyo hivyo vya habari kuwa "Tusubiri kitakachotokea Zimbabwe" - Pinda

  Nadhani wakati mwingine tunasoma zaidi ya kilichosemwa na ili kupata catchy phrase basi tunaandika tu.

  Jukumu la kwanza ni kujua kinadharia; Waziri Mkuu hawezi kuzungumzia deployment ya majeshi yetu mahali popote with authority. Hivyo kusema Tanzania iko tayari kupeleka majeshi halafu unamnukuu Waziri Mkuu ni kuonesha hujui majukumu na nguvu za Waziri Mkuu.
   
 5. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #5
  Apr 11, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Na wengi wetu humu hatuhoji mengi tunayosikia kutoka kwenye vyombo vyetu vya habari na tunakimbilia kumshambulia mtu na kumuita kila aina ya majina.
   
 6. J

  JokaKuu Platinum Member

  #6
  Apr 11, 2008
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,782
  Likes Received: 5,022
  Trophy Points: 280
  ..mimi ni mmoja wa waliomshambulia Waziri Mkuu Pinda kwa kauli ambayo nimekuja kugundua hakuitoa.

  ..naamini ilikuwa ni makosa kwa upande wangu kutoa shutuma zile.
   
 7. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #7
  Apr 11, 2008
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  kama alivyosema JK, makanjanja wako wengi.. hata Bungeni wapo pia... suala ni kuchambua, unatoa chuya unabakiza mchele!
   
 8. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #8
  Apr 11, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  The real problem is that our politicians speculate too much.You cannot speculate in international diplomacy.

  Pinda kasema

  Katika international diplomacy kwenye siasa na spin za kila aina mtu anayesema hivi anaonyesha uvivu wa kufikiri na kukosa umakini.Huwezi kusema "kama" na "ikiwa" na kutoa misimamo ya nchi wakati kitu hakijawa. You just open yourself to misinterpretations, deliberate or unintentional.Muulize John McCain alivyokuwa quoted out of context swala la kukaa Iraq miaka 100, muulize Barack Obama kuhusu kukutana na Ahmadinejad au kutumia nuclear Pakistan. Speculation breeds misinterpretations, spins and more speculations.

  Kuna watu wengine wanaweza kusema Tanzania kama mwenyekiti wa AU inaanza kutoa signal AU ipeleke majeshi Zimbabwe.Siwezi kulaumu waliom misquote Pinda (kama kweli wame m misquote) ikiwa wamem misquote makusudi au hawakumuelewa.

  Alichotakiwa kusema ni kitu kidogo tu.Tanzania inangojea tamko la vikao vya AU na siwezi kusema lolote kabla hatujakaa na wenzetu kujadili.Kwisha kazi.

  Ila hatujui kusema "no comments" "I do not have the facts right now" "mshindi wa uchaguzi hajatangazwa" na mambo mengine central kama hayo halafu kuishia hapo, sio unasema "matokeo ya uchaguzi hayajatangazwa" halafu unaenda ku speculate military intervention bila hata kujua nani atakuwa mshindi.

  We want facts, cold facts, not speculations.Sasa Kama PM ana speculate akiletewa maneno ya speculation kwamba Tanzania inataka kuvamia Zimbabwe atakuwa na moral higher ground kukemea speculations?
   
 9. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #9
  Apr 11, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Na sisi "wajuzi" wa mambo humu tumezidi....muda wote "tuko" tumekaa chonjo tukisubiri tu pale viongozi wetu watakapoteleza ulimi na sisi hao...vroom...hatukawii kushambulia. Wakati mwingine inakuwa kama vile "tunawaombea" wakosee kitu fulani ili tupate cha kulalamikia na kuongelea.....
   
 10. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #10
  Apr 11, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Hakuna kuombea negative Mkuu, mimi kila siku naombea tupate ma leaders smart ambao watanifanya proud kuwataja kama "So and so is the president of Tanzania"

  Ingawa Nyerere alikuwa na matatizo yake, alikuwa anaweza kupanga point.Kuna watu mpaka leo wanajadili (ona hapa) exchanges za Nyerere, Reagan, Trudeau na Thatcher Cancun Mexico 1981 kuhusu mambo ya subsidies za serikali kwa wakulima nchi tajiri zinavyoharibu hali za wakulima wa nchi masikini, au crusade yake kuhusu kufutwa madeni ya South South

  Mkapa fisadi na alikuwa anamtetea demagogue Mugabe Australia CHOGM 2000, lakini kina Tony Blair wote walizima fegi na kisha ya hapo wakamtumia katika kazi zao.

  Sasa kiongozi hujui kuongoza, sawa, unashindwa hata ku fake authority na smartness? Unashindwa hata rhetoric?

  Sasa Pinda anajigonga gonga kuongea na waandishi wa bongo (simsingizii, kasema mwenyewe, ona hapa) ataweza kukaa ma Cancun na ma Paris Club kukata issue? Ku demand deni lifutwe? Kutetea wakulima wetu against US government subsidized farm products? Miaka 20 baada ya Pinda na Kikwete kustaafu watu wa kimataifa wanaweza kuwa quote kama figures fulani zilizofanya mambo ya kuweza kusomwa? Au watakuwa nondescript leaders tu?

  I seriously doubt optimism here.

  On a lighter note nasikia jamaa kashajikwapulia 17,000 hectares za game reserve huko South, ona hapa
   
 11. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #11
  Apr 11, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Nyani Ngabu;
  Huu mtazamo wa kuangalia vitu kivyako, bila kukubali mara moja kinachosemwa na wengi, ikiwa ni pamoja na yale yasemwayo hapa JF, ni kitu cha kipekee. Lakini unapokuja kwenye hii dunia kuwa tayari kuchukuliwa kama '**** kama jiwe' na wale watakaokushangaa.

  Nimefurahia - na sikutegemea - tundiko lako hilo, na nakuunga mkono 100%. Pia, naomba katika mahojiano yetu ya mbele usisite kuendelea kuniita vile utakavyo nidhania kila utaponiona '**** kama jiwe.'
   
 12. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #12
  Apr 11, 2008
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  makanjanja mwaka huu, watazidi kuumbuka
   
 13. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #13
  Apr 11, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mimi bado nasimama na kauli ya mwanzo .JK alikuwa akitoa matamshi siku za nyuma na baada ya siku moja yanapingwa .Leo imeanza kwa waziri mkuu .Kwa nini akaririwe akisema kwamba majeshi yataenda ? Ina maana mwandishi huyu atakywa kilaza na kuku kiasi gani ? Tunarudia hadithi za Ikulu kudai inabambikizwa lakini mwishowe kuna ukweli ndani yake .I am skeptical.
   
 14. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #14
  Apr 11, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Pundit, sidhani watu wanakuelewa na hizo ishu.

  Kitu kikubwa nitakacho mshukuru Mkapa milele ni kumpiga Kikwete brashi kwa kumuweka wizara ya nje miaka kumi. Yani aliona mbali ile mbaya! Na bado anaharibu. Itakuwa Pinda!
   
 15. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #15
  Apr 11, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mimi naamini kukataa bado ni spinning .Pinda alikuwa LIVE na alikaririwa akiwa LIVE .Hebu mliosikiliza na kuona LIVE semeni tusikie
   
 16. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #16
  Apr 11, 2008
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Lunyungu nakubaliana nawe hapa!

  Pinda alijikanganya mwenyewe kwa kutoa mawazo yanayojichanganya. Kwa nini aanze kulaumu watu kwa kutafsiri kile alichosema kwa namna aliyoisema!?

  Huyu Pinda nimesema hapa kila siku kuwa atajikuta anafungwa na haya maneno yake yanayochanganya kila siku. Kila mara anasema vitu na watu wakimuuliza anadai kuwa wametafsiri kinyume.

  Kila kitu kiko open kwa tafsiri ya msikilizaji. Hata Lowasa alisema the same thing pale Mkjj alivyomwandika kuhusu hotuba yake ya ndege inayopaa au kasungura ka bungeni!
   
 17. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #17
  Apr 11, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Nakubaliana na wewe mkuu, labda hukunielewa. Pinda kaharibu.

  Tokea kwenye risala yake ya kupokea madaraka Pinda alianza kuharibu. Siku ya kwanza alisema moja ya upekee wake ni kuwa mtoto wa mkulima, ambayo sio upekee kwa kizazi chake, na Mawaziri karibu wote katika historia. Siku ya pili, kuhusu soo la Lowassa akasema tugange yajayo, yaliyo pita si ndwele. Siku ya tatu akasema ataanza kufuatilia hii ishu, na mapendekezo ya Tume. Ni mchemkaji Pinda, na tulishamshtukia siku ya kwanza.
   
 18. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #18
  Apr 11, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Kuna mtu humu ndani wakati Pinda kateuliwa kuwa waziri mkuu alisema Pinda anaonekana kuwa mzungumzaji mzuri.....sijui huyu mtu alikuwa anamaanisha nini
   
 19. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #19
  Apr 11, 2008
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mhh,

  Naona unatafuta ugomvi sasa ... kwi kwi kwi kwi kwi ...
   
 20. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #20
  Apr 11, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Bebi wako yuko wapi leo...?
   
Loading...