Ofisi ya Msajili wa Vyama ya Siasa 2014: CHADEMA iliwapelekea kumbukumbu ya Mkutano Mkuu 2006 lakini hakuna kipengele kilichoondoa ukomo wa uongozi.

Mgambilwa ni mntu

JF-Expert Member
May 30, 2017
2,869
3,188
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ilitoa taarifa wakati wa Mkutano Mkuu wa CHADEMA mwaka 2014 kuwa, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu Wilbroad Slaa, hawakuwa tena na sifa za Uongozi ndani ya Chama hicho kwa kuwa wanabanwa na Katiba yao.
Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa nchini, Sisty Nyahoza alisema kuwa, walipata malalamiko na kuyafanyia kazi, ikiwa ni pamoja na kupitia kumbukumbu walizonazo na kubaini kuwa, kipengele cha ukomo wa uongozi kiliondolewa kinyemela katika Katiba ya CHADEMA.
Nyahoza alieleza kuwa, kwa kawaida Vyama vyote vinapofanya mkutano huwapelekea mihtasari hivyo, CHADEMA nao waliwapelekea kumbukumbu ya Mkutano Mkuu wa 2006 lakini hakuna sehemu yoyote iliyoondoa ukomo wa uongozi.
Labda kwa lengo la kuendelea kuwa madarakani, waliona wakiondoe kipengele hicho kwa njia ya kuwavuruga wapinzani wao kwenye nyadhifa hizo. Fikiria akina Wilbroad Kaborou, Chacha Wangwe, Zitto Kabwe na Mwita Waitara - possibly the list will keep growing!!
Je, ni wakati sasa, CHADEMA kujitokeza hadharani kufafanua juu ya tuhuma hizi kutoka kwa Ofisi ya Msajili wa Vyama? Ama Demokrasia kwa CHADEMA ni kuichachamalia CCM na Serikali yake bila kujitathimini kwenye nendo zao. Tofauti ya CCM na CHADEMA kwenye Demokrasia iko wapi?
IMG_5959.JPG
 
Tofauti ya CCM na Chadema ipo kubwa sana

CCM hakuna uchaguzi wa kidemokrasia unayemuweka mwenyekiti wake madarakani, uliona wapi mwenyekiti anashindanishwa na kivuli chake! CCM hawaruhusu nafasi ya uenyekiti kushindaniwa, hivyo mfumo unaomuweka madarakani ni mfumo wa kidikteta

Chadema hufanya uchaguzi wa mwenyekiti kwa njia ya kidemokrasia kwa kushindanishwa na yeyote yule anayojitokeza kugombea, hivyo misingi ya kidemokrasia hushika mkondo wake
 
Back
Top Bottom