Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa wawaambia CHADEMA kuweka picha ya Rais katika ofisi zao

Pich ya Mwenyekiti wa CCM ndani ya ofisi ya chama cha upinzani!
 
Nukuu:

(na pia wameanza kutumia bajeti ambayo wameiandaa lakini haijaidhinishwa na kamati kuu kama katiba yao inavyotaka.) Halafu wanataka katiba mpya
...Hilo ni dogo...( kama ni kweli),_ Msajili..m...rema..Yaani Mapungufu madogo no.01.ni Picha 02.Matumizi mabaya ya Bajeti..!!!
 
Nukuu:

(na pia wameanza kutumia bajeti ambayo wameiandaa lakini haijaidhinishwa na kamati kuu kama katiba yao inavyotaka.) Halafu wanataka katiba mpya
Nani wa kulaumiwa kama CCM wanaogoga vikao vya ndani vya CHADEMA.😂😂
Katiba mpya ni lazima ili kuwe na usawa. acha kujitia upunguani
 
..Ni ofisi ya CHAMA sio ofisi ya umma.

..Ningependa kusikia Msajili anataja na SHERIA inayolazimisha chama cha siasa kuweka picha ya Raisi ktk ofisi zao.

..Msajili ana mambo fulani ya kishamba sana. Hiyo yote ni kujaribu kuwa-provoke Chadema.
Nami ningependa ufafanuzi wa Msajili juu ya kuweka picha ya Mwenyekiti wa chama kingine kwenye ofisi ya chama pinzani.

Hii haiko sawa hata kidogo.
 
Dar es Salaam.

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imeishauri Chadema kuweka picha ya Rais katika ofisi za viongozi wa chama hicho kwa sababu hiyo ni taasisi ya umma.

Ushauri huo umetolewa leo Ijumaa Septemba 10, 2021 na Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza wakati wakifanya ukaguzi wa chama hicho katika utekelezaji wa Sheria ya Vyama vya Siasa na Sheria ya Gharama za Uchaguzi.

Amesema ofisi za vyama vya siasa ni ofisi za umma hivyo ni vizuri wakaendeleza utamaduni wa kuwa na picha ya Rais kwenye taasisi za umma.

"Hii ni ofisi ya umma, ni vizuri kukawa na picha ya Rais ukutani, siyo unaweka picha ya katibu mkuu. Huu ni ushauri tumewapa, tutapita Januari kuona kama wamelifanyia kazi," amesema Nyahoza.

Akizungumzia suala hilo, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema - Zanzibar, Salum Mwalimu amesema Msajili amekuta mambo yamekaa vizuri ndiyo maana akagundua hakuna picha ya Rais.

"Tumempokea Msajili, wamepitia taarifa zote walizozihitaji wamekuta mambo yako vizuri, ni masuala madogo madogo ndiyo yanahitaji kufanyiwa kazi. Kama angekuta mambo makubwa, asingekumbuka kuangalia picha ya Rais," amesema Mwalimu.

Ofisi ya Msajili inaendelea na ukaguzi wa vyama vya siasa na leo walikuwa wakikagua Chadema ambapo Nyahoza amesema wamefurahishwa na mfumo mzuri wa uwekaji kumbukumbu za fedha na wana mfumo mzuri wa utawala.

Hata hivyo, amesema wamebaini mapungufu kadhaa ikiwemo uwekaji kumbukumbu kwenye mali za chama na pia wameanza kutumia bajeti ambayo wameiandaa lakini haijaidhinishwa na kamati kuu kama katiba yao inavyotaka.
Project waliyopewa ya kuua cdm imebuma
 
Kuna mambo mengi ya msingi wanashindwa kuyashughulikia wanaongelea picha ya mdemko
 
Ni kweli Chadema ni taasisi ya umma kuweka picha ni lazima au waweke picha ya Kenyata utaweza kujua kuwa serikali ipo au haipo.
 
Dar es Salaam.

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imeishauri Chadema kuweka picha ya Rais katika ofisi za viongozi wa chama hicho kwa sababu hiyo ni taasisi ya umma.

Ushauri huo umetolewa leo Ijumaa Septemba 10, 2021 na Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza wakati wakifanya ukaguzi wa chama hicho katika utekelezaji wa Sheria ya Vyama vya Siasa na Sheria ya Gharama za Uchaguzi.

Amesema ofisi za vyama vya siasa ni ofisi za umma hivyo ni vizuri wakaendeleza utamaduni wa kuwa na picha ya Rais kwenye taasisi za umma.

"Hii ni ofisi ya umma, ni vizuri kukawa na picha ya Rais ukutani, siyo unaweka picha ya katibu mkuu. Huu ni ushauri tumewapa, tutapita Januari kuona kama wamelifanyia kazi," amesema Nyahoza.

Akizungumzia suala hilo, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema - Zanzibar, Salum Mwalimu amesema Msajili amekuta mambo yamekaa vizuri ndiyo maana akagundua hakuna picha ya Rais.

"Tumempokea Msajili, wamepitia taarifa zote walizozihitaji wamekuta mambo yako vizuri, ni masuala madogo madogo ndiyo yanahitaji kufanyiwa kazi. Kama angekuta mambo makubwa, asingekumbuka kuangalia picha ya Rais," amesema Mwalimu.

Ofisi ya Msajili inaendelea na ukaguzi wa vyama vya siasa na leo walikuwa wakikagua Chadema ambapo Nyahoza amesema wamefurahishwa na mfumo mzuri wa uwekaji kumbukumbu za fedha na wana mfumo mzuri wa utawala.

Hata hivyo, amesema wamebaini mapungufu kadhaa ikiwemo uwekaji kumbukumbu kwenye mali za chama na pia wameanza kutumia bajeti ambayo wameiandaa lakini haijaidhinishwa na kamati kuu kama katiba yao inavyotaka.

CDM hautambui utawala dharimu wa ccm hivyo sioni sababu ya kuwa na kijipicha cha raisi?
 
TJNATAKA tamko la chama litueleze kwa nini wanatumia bajeti ambayo haijapitishwa na kamati kuu kama katiba ya CHADEMA inavyotutaka, kwa mujibu wa msajili wa vyama.

Haya si ndio yale yale tuliyomlaani Magufuli kuanzisha miradi ya miundombinu ma trilioni ambayo hayajapitishwa bungeni?

Tunataka majibu!
 
..Ni ofisi ya CHAMA sio ofisi ya umma.

..Ningependa kusikia Msajili anataja na SHERIA inayolazimisha chama cha siasa kuweka picha ya Raisi ktk ofisi zao.

..Msajili ana mambo fulani ya kishamba sana. Hiyo yote ni kujaribu kuwa-provoke Chadema.
Kwani ofisi za umma huwa ninapigwa mabomu! Ofisi za umma zinavunjwa milango kuvamia mikutano ya ndani! Msajili wa vyama, only in Tanzania.
 
Dar es Salaam.

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imeishauri Chadema kuweka picha ya Rais katika ofisi za viongozi wa chama hicho kwa sababu hiyo ni taasisi ya umma.

Ushauri huo umetolewa leo Ijumaa Septemba 10, 2021 na Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza wakati wakifanya ukaguzi wa chama hicho katika utekelezaji wa Sheria ya Vyama vya Siasa na Sheria ya Gharama za Uchaguzi.

Amesema ofisi za vyama vya siasa ni ofisi za umma hivyo ni vizuri wakaendeleza utamaduni wa kuwa na picha ya Rais kwenye taasisi za umma.

"Hii ni ofisi ya umma, ni vizuri kukawa na picha ya Rais ukutani, siyo unaweka picha ya katibu mkuu. Huu ni ushauri tumewapa, tutapita Januari kuona kama wamelifanyia kazi," amesema Nyahoza.

Akizungumzia suala hilo, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema - Zanzibar, Salum Mwalimu amesema Msajili amekuta mambo yamekaa vizuri ndiyo maana akagundua hakuna picha ya Rais.

"Tumempokea Msajili, wamepitia taarifa zote walizozihitaji wamekuta mambo yako vizuri, ni masuala madogo madogo ndiyo yanahitaji kufanyiwa kazi. Kama angekuta mambo makubwa, asingekumbuka kuangalia picha ya Rais," amesema Mwalimu.

Ofisi ya Msajili inaendelea na ukaguzi wa vyama vya siasa na leo walikuwa wakikagua Chadema ambapo Nyahoza amesema wamefurahishwa na mfumo mzuri wa uwekaji kumbukumbu za fedha na wana mfumo mzuri wa utawala.

Hata hivyo, amesema wamebaini mapungufu kadhaa ikiwemo uwekaji kumbukumbu kwenye mali za chama na pia wameanza kutumia bajeti ambayo wameiandaa lakini haijaidhinishwa na kamati kuu kama katiba yao inavyotaka.
Hii imenikumbusha tabia ya mama yangu nikiwa mdogo. Akikukuta umerelax unaangalia Tv atakuuliza kazi hii umefanya? Kazi ile umefanya sasa akikuta umeshafanya zoote yupo radhi akutume hata dukani ilimradi tu apate sababu ya kukutoa😄
 
Siku Rais akiwa mwingine na mwenyekiti mwingine chadema ndo wataweka hiyo picha ya rais, kwa sasa wakiweka itaonekana picha ni ya mwenyekiti wa ccm sio rais
 
Back
Top Bottom