Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi Online, Profesa Lipumba naye amechaguwa wajumbe wa Bodi. Mkutano huo walialikwa muwakilishi kutoka RITA na OFISI YA MSAJILI amethibitisha kuwa walihudhuria.
Aidha Profesa Lipumba anasema Upande wa maalim Seif hauna Baraza Kuu na yeye ndie mwenye Baraza kuu.
Nimetafakari kidogo ushiriki wa Ofisi ya Msajili na RITA kweli wamejiridhisha na huo Uhalali wa kikao cha baraza kuu la Lipumba upo kihalali au ndio ule mwendelezo wa kujichora kwa kuchagua upande?
Hivi Baraza kuu la CUF linachaguliwa na nani kwa mujibu wa katiba yao ? Jee hili RITA na MSAJILI wamejiridhisha?
Vipi ikiwa Baraza kuu ndilo lililomfukuza Lipumba na hakuna kumbukumbu ya kumrejesha leo wametowa mamlaka wapi ya kumfanya Lipumba awe Mwenyekiti wake tena na kuchaguwa wajumbe wa bodi?
Vipi kuhusu akidi ya wajumbe wa kikao imezingatiwa kwa wajumbe halali wa Baraza kuu. Jee RITA NA MSAJILI wamejiridhisha hayo ?
Nadhani busara ingeelekezwa kwanza kutaka KUJUWA UHALALI WA UENYEKITI WA LIPUMBA KWANZA AMBAPO MATARAJIO NI KESI KUSOMWA KESHO. JEE HAPA RITA NA MSAJILI WATAEPUKANA VIPI NA TUHUMA ZA RUSHWA KWA JAJI IKIWA MAHAKAMA ITAMTAMBUWA LIPUMBA?
Kwa sababu inakuwaje wawe na uthubutu wa kushirikiana na upande ule ule ulitenguliwa wajumbe wake wa bodi kwa kutofuatwa sheria leo tena ofisi hizi za umma zikapata uthubutu wa kujiingiza tena kwenye sintofahamu hii na kuwa tayari kujidhalilisha kwa kiasi hiki ikiwa kweli hawajui maamuzi ya kesi hii.
Jee RITA NA MSAJILI wamesukumwa na nini kujiiingiza kwenye mgogoro huu ? tukisema wanatumika kisiasa tutakosea ?
Wameshindwa nini walau kusubiri hukumu ya kesi ya uhalali wa uenyekiti wa lipumba ikasomwa?
Hapa ndipo RITA na Ofisi ya msajili inavyojichora kwenye mgogoro huu wa CUF.
Kishada