Ofisi ya Msajili wa vyama na RITA wanavyozidi kujichora mgogoro wa CUF.

KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,088
2,000
Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi Online, Profesa Lipumba naye amechaguwa wajumbe wa Bodi. Mkutano huo walialikwa muwakilishi kutoka RITA na OFISI YA MSAJILI amethibitisha kuwa walihudhuria.

Aidha Profesa Lipumba anasema Upande wa maalim Seif hauna Baraza Kuu na yeye ndie mwenye Baraza kuu.

Nimetafakari kidogo ushiriki wa Ofisi ya Msajili na RITA kweli wamejiridhisha na huo Uhalali wa kikao cha baraza kuu la Lipumba upo kihalali au ndio ule mwendelezo wa kujichora kwa kuchagua upande?

Hivi Baraza kuu la CUF linachaguliwa na nani kwa mujibu wa katiba yao ? Jee hili RITA na MSAJILI wamejiridhisha?

Vipi ikiwa Baraza kuu ndilo lililomfukuza Lipumba na hakuna kumbukumbu ya kumrejesha leo wametowa mamlaka wapi ya kumfanya Lipumba awe Mwenyekiti wake tena na kuchaguwa wajumbe wa bodi?

Vipi kuhusu akidi ya wajumbe wa kikao imezingatiwa kwa wajumbe halali wa Baraza kuu. Jee RITA NA MSAJILI wamejiridhisha hayo ?

Nadhani busara ingeelekezwa kwanza kutaka KUJUWA UHALALI WA UENYEKITI WA LIPUMBA KWANZA AMBAPO MATARAJIO NI KESI KUSOMWA KESHO. JEE HAPA RITA NA MSAJILI WATAEPUKANA VIPI NA TUHUMA ZA RUSHWA KWA JAJI IKIWA MAHAKAMA ITAMTAMBUWA LIPUMBA?

Kwa sababu inakuwaje wawe na uthubutu wa kushirikiana na upande ule ule ulitenguliwa wajumbe wake wa bodi kwa kutofuatwa sheria leo tena ofisi hizi za umma zikapata uthubutu wa kujiingiza tena kwenye sintofahamu hii na kuwa tayari kujidhalilisha kwa kiasi hiki ikiwa kweli hawajui maamuzi ya kesi hii.

Jee RITA NA MSAJILI wamesukumwa na nini kujiiingiza kwenye mgogoro huu ? tukisema wanatumika kisiasa tutakosea ?

Wameshindwa nini walau kusubiri hukumu ya kesi ya uhalali wa uenyekiti wa lipumba ikasomwa?

Hapa ndipo RITA na Ofisi ya msajili inavyojichora kwenye mgogoro huu wa CUF.Kishada
 
Kifaurongo

JF-Expert Member
Jan 18, 2010
3,766
2,000
Ndio madhara ya kuandika katiba na kisha kushindwa kufanya maamuzi kulngana na katiba. Maalim kwa sababu zake mwenyewe hakuishughulikia kikatiba barua ya kujiudhuru Lipumba naye akatumia mwanya huo kurudi madarakani. Kwa kukurupuka akataka kutumia mkutano mkuu kumchomoa katika ndoano aliyoirusha majini mwenyewe hali kuwa kishachelewa (Kikatiba).
 
Umkilo

JF-Expert Member
Jan 24, 2018
471
500

Sijui sana mambo ya cuf lkn nilisikia Seif pia amechagua bodi yake na amepeleka majina RITA swali mbona yeye hakusubiri kesi ya uenyekiti wa Lipumba kwanini Lipumba pekee ndie anapaswa kusubiri?
 
MAGALEMWA

JF-Expert Member
Jul 8, 2015
6,024

Kuwa mkweli haya yanaratiwa kiuangalifu na kwa gharama yo yote ile kusiwe na CUF. Nimemsikia Lipumba akitoa hoja ya kufutwa CUF kwa sababu ya Maalim Sefu. Ukweli yeye ndiye wakala wa kuifuta CUF. Ila mola ajuaye yote atatuvusha atakako.
 
Hivi Maalimu angewasilisha barua kwenye vikao husika na kuitolea maamuzi, mara tu baada ya kuipokea, haya yangetokea? Amekaa nayo mfukoni karibu mwaka anakuja kusituka amekaliwa vibaya!!!??
 
dmketo

JF-Expert Member
Aug 10, 2015
498
1,000
Sijui sana mambo ya cuf lkn nilisikia Seif pia amechagua bodi yake na amepeleka majina RITA swali mbona yeye hakusubiri kesi ya uenyekiti wa Lipumba kwanini Lipumba pekee ndie anapaswa kusubiri?
Kwa jinsi nilivyomuelewa mleta hoja, yeye akujikita kwenye hizi pande kinzani kuchagua wajumbe, bali hoja yake ameielekeza kwenye kutoa angalizo kwa hizi taasisi za umma kujichagulia upande wa kushirikiana nao wakati dhahiri uelekeo wa kesi unaweza kuupa haki upande wa pili. Kwa mujibu wake ikitokea hivyo, itaichafua Serikali kuonekana ilikuwa na mkono wake kwenye mgogoro huu.
 
KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,088
2,000
Sijui sana mambo ya cuf lkn nilisikia Seif pia amechagua bodi yake na amepeleka majina RITA swali mbona yeye hakusubiri kesi ya uenyekiti wa Lipumba kwanini Lipumba pekee ndie anapaswa kusubiri?
Tatizo hapa sio Seif kuteuwa. Tunaizungumzia RITA na OFISI YA MSAJILI KUJIINGIZA KWENYE MGOGORO HUU licha ya Mahakama kutenguwa uamuzi ambao awali ulipata Baraka za RITA na Ofisi ya Msajili.
 
mmh

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
2,082
2,000
Maalimu kazidi naye sasa kakutana na profesa ngunguli ataomba poo mwenyewe, kama namuona akikatwa ugombea wa Zanzibar, yetu macho
 
Umkilo

JF-Expert Member
Jan 24, 2018
471
500
Kwa jinsi nilivyomuelewa mleta hoja, yeye akujikita kwenye hizi pande kinzani kuchagua wajumbe, bali hoja yake ameielekeza kwenye kutoa angalizo kwa hizi taasisi za umma kujichagulia upande wa kushirikiana nao wakati dhahiri uelekeo wa kesi unaweza kuupa haki upande wa pili. Kwa mujibu wake ikitokea hivyo, itaichafua Serikali kuonekana ilikuwa na mkono wake kwenye mgogoro huu.
Anataka tuone hivyo lkn shida yake ni kuonyesha kuwa upande wa Lipumba unabebwa lkn hauna uharali, lkn anasahau Seif hakuwaita na hata hakufuata utaratibu wa kuwachangua, wala hakuwaita hao Rita ofisi ya msajiri
 
Umkilo

JF-Expert Member
Jan 24, 2018
471
500
Tatizo hapa sio Seif kuteuwa. Tunaizungumzia RITA na OFISI YA MSAJILI KUJIINGIZA KWENYE MGOGORO HUU licha ya Mahakama kutenguwa uamuzi ambao awali ulipata Baraka za RITA na Ofisi ya Msajili.
Ukialikwa usiende? Kwa nini?
 
KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,088
2,000
Hivi Maalimu angewasilisha barua kwenye vikao husika na kuitolea maamuzi, mara tu baada ya kuipokea, haya yangetokea? Amekaa nayo mfukoni karibu mwaka anakuja kusituka amekaliwa vibaya!!!??
Kuna mambo mengine ni siri juu ya siri bora unyamaze. Ni huo wakati vile vile iliarifiwa kuwa intelijensia imebaini CUF ingevurugwa wakati ule ule ikiwa hicho kikao cha Mkutano mkuu kingeitishwa kabla ya uchaguzi. Nadhani wazee wanabusara zao kusubiri uchaguzi upite. Hata hivyo nafikiri ulikiona kilichotokea mkutano ulipoitishwa pale Lipumba alipvamia mkutano akisema kapigiwa simu na baadhi ya wanacha,ma na namna alivyoingia na walinzi.
 
KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,088
2,000
Anataka tuone hivyo lkn shida yake ni kuonyesha kuwa upande wa Lipumba unabebwa lkn hauna uharali, lkn anasahau Seif hakuwaita na hata hakufuata utaratibu wa kuwachangua, wala hakuwaita hao Rita ofisi ya msajiri
Hapana. RITA walipelekewa awali wakakataa kwa kisingizio kuwa Msajili wa vyama anamtambuwa Lipumba bila kujali sheria yao inasimamia nini. Ndio maana Maalim Seif amekialika chombo chengine cha Serikali ( Government Authority) kushuhudia.

Hoja hapa kwa NINI RITA NA MSAJILI wameshirikiana tena na LIPUMBA wakati wanajuwa sheria zimekiukwa?
 
Kifaurongo

JF-Expert Member
Jan 18, 2010
3,766
2,000
Kuna mambo mengine ni siri juu ya siri bora unyamaze. Ni huo wakati vile vile iliarifiwa kuwa intelijensia imebaini CUF ingevurugwa wakati ule ule ikiwa hicho kikao cha Mkutano mkuu kingeitishwa kabla ya uchaguzi. Nadhani wazee wanabusara zao kusubiri uchaguzi upite. Hata hivyo nafikiri ulikiona kilichotokea mkutano ulipoitishwa pale Lipumba alipvamia mkutano akisema kapigiwa simu na baadhi ya wanacha,ma na namna alivyoingia na walinzi.
Ndio kosa la kiufundi, kikao kiliitishwa baada ya Lipumba kubatilisha maamuzi kujiuzuru na kikawa kikwazo kwa Maalim kutoa majibu. kikao kilikua kikao mkakati na angekuwa mnyonge asiyejua sheria na katiba, Lipumba angeng'oka!!
 
KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,088
2,000
Ndio kosa la kiufundi, kikao kiliitishwa baada ya Lipumba kubatilisha maamuzi kujiuzuru na kikawa kikwazo kwa Maalim kutoa majibu. kikao kilikua kikao mkakati na angekuwa mnyonge asiyejua sheria na katiba, Lipumba angeng'oka!!
Itategemea tafsiri ya sheria kutoka mahakamani. Kwa kadiri nilivyofuatilia mgogoro huu, Katiba ya CUF haina kipengele cha kujiuzulu halafu ukajirejesha. Aidha wanasema wanasheria kwamba kujizulu ni PROCESS kwenye katiba ya CUf , haishii kujiuzulu na kujirejesha tu lakini LAZIMA UTHIBITISHWE NA MKUTANO MKUU hata kama mkutano umechelewa. PROCESS inaishia kuthibitishwa na mkutano mkuu ambao ulisharidhia kujizulu kwa Lipumba. Hayo mengine ni mikakati tu ya kuivuruga CUF.

Hapa inazungumzwa KATIBA YA CUF na sio MSAJILI.
 
mtanzania1989

JF-Expert Member
May 20, 2010
3,164
2,000
Kwa jinsi nilivyomuelewa mleta hoja, yeye akujikita kwenye hizi pande kinzani kuchagua wajumbe, bali hoja yake ameielekeza kwenye kutoa angalizo kwa hizi taasisi za umma kujichagulia upande wa kushirikiana nao wakati dhahiri uelekeo wa kesi unaweza kuupa haki upande wa pili. Kwa mujibu wake ikitokea hivyo, itaichafua Serikali kuonekana ilikuwa na mkono wake kwenye mgogoro huu.
Kwa sasa serikali inamtambua Lipumba kama mwenyekiti rasmi, watafanya naye kazi labda hadi mahakama itamke vinginevyo. Maalim ameenda kuishia kumualiza Boniface Jacob, meya mimashavu kama mwakilishi wa serikali, hivi kweli hizi ni akili timamu?
 
kandamatope

JF-Expert Member
May 19, 2018
471
500
Itategemea tafsiri ya sheria kutoka mahakamani. Kwa kadiri nilivyofuatilia mgogoro huu, Katiba ya CUF haina kipengele cha kujiuzulu halafu ukajirejesha. Aidha wanasema wanasheria kwamba kujizulu ni PROCESS kwenye katiba ya CUf , haishii kujiuzulu na kujirejesha tu lakini LAZIMA UTHIBITISHWE NA MKUTANO MKUU hata kama mkutano umechelewa. PROCESS inaishia kuthibitishwa na mkutano mkuu ambao ulisharidhia kujizulu kwa Lipumba. Hayo mengine ni mikakati tu ya kuivuruga CUF.

Hapa inazungumzwa KATIBA YA CUF na sio MSAJILI.
Unaongea maneno ya kurishwa na mitandao
Kwa mujibu wa katiba ya cuf
Mwenyekiti na katibu mkuu wataondolewa na wajumbe wa mkutano mkuu
Ili mwenyekiti aondolewe katika nafasi hama kwa kufukuzwa au kujiuzulu

Wajumbe wa mkutano mkuu watapiga kura ya siri ( sio ya kidole juu

Wajumbe wa mkutano mkuu wa upande wa bara kwanza watahesabiwa kama koram imetimia wanatakiwa wapige kura ya theluthi 2

Vili vile na wajumbe kutoka upande wa kisiwani Zanzibar nao watahesabiwa kama koram imetimia watapiga kura ya siri kwa mtindo ule ule wa theluthi 2

hiyo ndio katiba ya cuf inavyotaka pale ubungo plaza ulifanyika uhuni
Ndio maana msajili akashauri kwa mujibu wa katiba yenu ya cuf profesa lipumba bado mwenyekiti harali

Kuhusu kesi ya kesho kesi inamuhusu msajili Maalim seif na kundi lake linamtuhumu msajili kuingilia mambo ya ndani ya cuf kesho hakuna kesi dhidi ya lipumba
Ukisikia kesho kuna kesi dhidi ya lipumba elewa tu hayo ni Matango pori..
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom