Ofisi ya msajili wa vyama: Imeshindwa kazi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ofisi ya msajili wa vyama: Imeshindwa kazi!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MWANAWAVITTO, Jun 27, 2012.

 1. MWANAWAVITTO

  MWANAWAVITTO Senior Member

  #1
  Jun 27, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 185
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 45
  Ofisi ya msajili wa vyama ni ofisi inayoshughulika na kazi ya usajili wa vyama vya siasa visivyo na mirengo ya kidini au kikabila kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na sheria zake.

  Baadhi ya kazi za ofisi hii ni pamoja na kusimamia ukuaji ulio bora wa demokrasia katika nyanja ya siasa, kusimamia vyama katika mienendo yake ya kila siku kwa maana ya kuvilinda katika kutekeleza majukumu yake kisheria, kulinda misingi ya nchi kidemokrasia ili isivamiwe na siasa za kibaguzi kama vile udini na ukabila.

  Kanuni, shughuli na taratibu za ofisi hii zinapaswa kuendeshwa bila ya ubaguzi wala upendeleo na woga kwa mtu yeyote wala chama chochote kile cha siasa, kama ambavyo kanuni za ofisi zinaelekeza na jinsi yalivyo matakwa ya katiba ya nchi.

  Mwaka wa 2005 wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa Tanzania, JESHI LA POLISI lilijitokeza na kudai kuwa kuna chama cha siasa kimegeuka na kuwa kundi la WAISLAMU WENYE MSIMAMO MKALI NA LENYE MRENGOWA KIGAIDI, hayo yalielezwa na aliyekuwa mkuu wa Jeshi hilo IGP Omary Mahita.

  Kauli hiyo ya jeshi iliambatana na na kuonyeshwa kwa kontena lililosheni silaha zenye nembo za chama cha CUF[Civil United Front] kilichopata usajili wa kuwa chamacha siasa kwa mujibu wa taratibu za nchi na siyo chama cha kigaidi au kidini.

  Kwa vyovyote vile taarifa hizo ziliwashtua wengi na kuwaacha wakiwa na maswali yasiyo na majibu na hata kukifanya chama hicho kupoteza wanachama na wafuasi wengi jambo ambalo lilikinyima kura nyingi chama hicho na kuathiri maana nzima ya SIASA ZA VYAMA VINGI.

  Wakati hayo yakiendelea kuelekeauchaguzi mkuu wa mwaka 2010 yakaibuka mengine, zilizuka taarifa zilizoambatana na jumbe fupi kwenye simu za mkononi [MESSAGE ] pamoja na nyaraka zinazotaja chama cha CHADEMA [Chama cha Demokrasia na Maendeleo] ambacho kina usajili wa ofisi hii kuwa ni chama cha KIKABILA na KIKATOLIKI.

  Kwa mara nyingine tena wapiga kura wakaachwa njia panda wasijue cha kufanya, jambo ambalo liliathiri upigaji kura kidemokrasia na kuharibu maana nzima ya MFUMO WA SIASA ZA VYAMA VINGI.

  Ofisi hii ndiyo ilipaswa kutoa tamko juu ya madai haya kwamba:

  1-Haijawahi kusajili vyama vyenye mirengo ya kidini na kikabila, hivyo kukemea uzushi huo,
  2-au Ikiri kuwa inasajili vyama vyenye mielekeo tajwa, na iseme NI LINI ILIANZA USAJILI WA VYAMA VYA KIDINI NA KIKABILA katika ardhi yetu.

  Jambo la kustaajabisha ni kuwa ofisi hii imekaa kimya na kuacha Watanzania wasijue wala kuelewaukweli ni upi na nini maana halisi ya mfumo wa vyama vingi hivyo kuathiri demokrasia ya nchi yetu ambapo madhara yake ni makubwa kuliko tunavyoweza kufikiri,
  Ukimya wa ofisi hii una maana ya kuwa; kuna uzembe uliokubuhu ndani ya ofisi hii hivyo kuifanya kushindwa kutekeleza majukumu yake na kuicha DEMOKRASIA YA NCHI YETU na SIASA ZA NCHI YETU zikichafuliwa na WAHUNI wasiotutakia mema.

  Hivyo basi;
  -Sekretareti nzima ya ofisi hii inapaswa kujiuzulu kwani imeshindwa kazi ya kulinda siasa za nchi yetu pamoja na demokrasia kwa njia ya kuhifadhi na kuitetea katiba yetu kwa kuwaeleza Watanzania ukweli na kutoa ufafanuzi wa mambo husika,
  - Kama sekretareti hii haitataka kujiuzulu basi itumbiye sababu za kukaa kimya na kuliacha TAIFA likigawanyika katika misingi ya KIDINI na KIKABILA wakati tulishawapa rungu la kutulinda.
  - Itueleze pia kwanini ofisi hiyo inatukanwa na ipo kimya jambo ambalo linawafanya wengi waamini uzushi na propaganda za kidini na kikabila.


  MWANAWAVITTO KIRARO.
   
 2. Nzenzu

  Nzenzu JF-Expert Member

  #2
  Jun 27, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 859
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Bwana Tendwe yuko bize na kuandaa mikakati ya 2015... Kazi ipo!
   
 3. B

  Bob G JF Bronze Member

  #3
  Jun 27, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Msajili kawekwa 2 na ccm alinde ccm umesahau Liundi alipostaafu 2 katangaza kugombea ubunge kupitia ccm,
   
 4. MWANAWAVITTO

  MWANAWAVITTO Senior Member

  #4
  Aug 12, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 185
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 45
  si ajabu huyu nae akafuata nyayo
   
Loading...