Ofisi ya mkuu inapotumika kumnyanyasa aliyekuwa mfanyakazi wake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ofisi ya mkuu inapotumika kumnyanyasa aliyekuwa mfanyakazi wake

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Nam..., Nov 16, 2011.

 1. N

  Nam... Member

  #1
  Nov 16, 2011
  Joined: Nov 11, 2011
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mfanyakazi mmoja katika kituo kimoja cha redio ya kiongozi mmoja serikalini, anaendelea kunyanyasika kwa kuchukuliwa vitu vyake vya ndani katika nyumba aliyokuwa akiishi kabla ya kufiwa na mkewe na kusafiri kwenda Dar kwa mazishi.

  Wakati akiwa msibani inasemekana baadhi ya wafanyakazi wenzake walibeba mizigo yote iliyokuwa ndani ya nyumba hiyo ambayo mfanyakazi huyo alikuwa akiishi na mfanyakazi mwingine ambaye hata hivyo alifariki mapema mwezi wa tisa hivyo vifaa vyake pamoja na vya mlalamikaji vyote vilikuwa ndani ya nyumba hiyo yenye zaidi ya vyumba vitatu.

  Ukweli wa kunyanyasika mfanyakazi huyu ni kwamba; alipelekwa Bukoba kufanya kama meneja masoko wa kituo cha redio, lakini baadaye maelewano ya aliyempeleka kwa nduguzetu hao yakawa madogo na akapendekeza kumtimua, lakini kabla hajamtimua ikabidi amwondoe kwenye mshahara na akaendelea kumlipa posho baada ya kuleta matangazo.

  Baadaye aliyekuwa kiongozi wa chombo hicho aliondoka na kuwaachia ngazi vijana ambao bado wanachapa mzigo redioni hapo bila kuwa na maelewano na mfanyakazi huyo anayenyanyaswa kwasababu yeye akipeleka matangazo pale anapata commision ya 10% jambo ambalo wadau wanaona vijana wanaomwonea fitna wanahisi wanazikosa kwa ajili yake.

  Baada ya vitu vyake kuondolewa ndani jamaa alilalamika kwamba akikuta kuna kilichopungua lazima afungue kesi, dada kutokana na uhoga wa waliohamisha vitu wamehamua kumfanyia mbinu ya kusema kuwa ofisi haimtambui wala hawajui alikuwa akiishi wapi, lakini ukweli ni kwamba huyu jamaa alianzia nyamkazi akiwa sambamba na mfanyakazi mwingine aliyefariki baadaye wakahamishiwa kashai na wakilipiwa pango, iweje ofisi ya kiongozi huyo haimtambui.

  Polisi Bukoba imesema kesi iliyofunguliwa na ndugu wa karibu wa mfanyakazi huyo, haina vigezo vya kwenda mahakamani kwasababu wanajua ikifika mahakamani watashindwa kwakufanya kazi na mtu kwa muda wa miaka3 bila mikataba ya kazi lakini pia wanajihisi kuwa na kosa la kuvunja nyumba na kuhamisha vitu. Je ni sahihi vitendo vinavyofanywa na wafanyakazi katika ofisi ya mkuu huyo? J e wizara ya kazi ikowapi kutokagua mikataba ya wafanyakazi?????????
   
 2. JamboJema

  JamboJema JF-Expert Member

  #2
  Nov 16, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,148
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Unasema mfanyakazi wa Redio ya Kagasheki?
   
Loading...