VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,802
Hebu tazama kuhusu Kabendera na wengineo:
Kwanza, watu 'wasiojulikana na wasiotaka kujitambulisha' wanafika nyumbani kwa anayetaka kukamatwa. Wananchi wakisogea na kutaka kujua kulikoni, watu hao hudai ni polisi.
Pili, Mkamatwaji hufikishwa Polisi na mahojiano hufanyika. Huhojiwa kwa mambo mbalimbali ynayodhaniwa kutendwa au kushiriki kwa Mkamatwaji. Mahojiano huambatana na Mkamatwaji kuwekwa mahabusu.
Kabrasha lenye nyaraka za taratibu zote zilizofuatwa kuanzia kukamatwa hadi kuhojiwa kwa Mkamatwaji hupelekwa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini almaarufu kama DPP. Mkuu huyo hupaswa kulipitia kabrasha hilo na kuona kama kuna kosa au makossa yaliyotendwa.
Ofisini kwa DPP, kulingana na nyaraka za mahojiano ya Polisi na Mkamatwaji, huandaliwa Hati ya Mashtaka yenye shtaka au mashtaka kadhaa. IELEWEKE KUWA mashtaka huchipukia kwenye malalamiko ya Mlalamikaji aliyefungua malalamiko Polisi na maelezo aliyoyatoa Mkamatwaji wakati akihojiwa na Polisi. Si chini wala zaidi ya hapo.
Wananchi wanapenda wakosaji wapelekwe Mahakamani na sharia kuchukua mkondo wake. Lakini, hawaridhishwi na namna Mkamatwaji anavyokamatwa, kuwekwa mahabusu na kuhojiwa.Tena wananchi hawaridhishwi na ama na aina ya mashtaka wanayoburuzwa nayo mahakamani Wakamatwaji. Mashtaka hutofautiana na mahojiano ya Polisi na Mkamatwaji.
Vile vile, mashtaka ya sasa kutoka kwa DPP 'huonwa na kuaminiwa' na wananchi kama makossa ya kukomoana. Imekuwa kawaida hivisasa Wakamatwaji kushtakiwa kwa makossa yasiyo na dhamana kama uhujumu uchumi, utakatishaji fedha na ugaidi.
Kutokana na malalamiko ya wananchi, ambao ndiyo hasa wateja wa Mkurugenzi wa Mashtaka na Polisi, Ofisi hizi zinapaswa kujitafakari na kujirekebisha. Si vyema vyombo vinavyopaswa kuaminika na kuwa kimbilio la wananchi wanyonge kutiliwa shaka kila dakika. Watanzania sio wajinga!
Makosa yasiyo na dhamana yasiwe kichaka cha mateso ya kisheria!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Muleba, Kagera)