Elections 2010 Ofisi ya Mbunge wa Nyamagana

Hassan J. Mosoka

JF-Expert Member
Oct 26, 2010
682
323
Ndugu zangu nimepatwa na mshangao mkubwa kuona aliyekuwa WAZIRI WA MAMBO YA NDANI (USALAMA WA RAIA) na mwanasheria kwa taaluma kuondoka na samani za OFISI YA MBUNGE WA BUNGE LA JMT.
Naomba kusaidiwa tu kujua je amechukuliwa hatua gani na serikali kwa kupora mali ya Umma? CCM kama chama wamemchukulia hatua gani kwa aibu aliyokiletea chama?
Kama huyu ndiye alikuwa analinda usalama na mali zetu Je tuna hakika gani kuwa ametuacha salama kama taifa?,
Naomba mnisaidie kuelewa hayo tu kwa leo
 
Kwa Kuwa ni wa CCM hahuna kosa, inguwe vinginevyo unge juaaaaa serikali ilivyo
 
we hujui nini? hii ni tz zaidi uijuavyo
ukimwuliza chiligati ama makamba utasikia "eeeeh bwana anahaki ya kuchikuwa hizo samani ni zake tatizo watanzania tunatumia vifaa vya ofisini kimazoea" hayo ndiyo majibu yao

sasa awe ni mbunge wa upande wa pili utasikia tume zikiundwa na mapolisi wanavyohangaika na issue.ila kwa hiii ya masha na mbeya wala kimyaaaaaaaaa

mapinduziiiii daimaaaaaa
 
Na hawa ndio walikua viongozi kwaajili ya taifa, shame on them, inamaana public office wao walikua wanaleta vitu kutoka majumbani kwao? Katiba mpya muhimu tuwajibishane.
 
hii ni tabia ya wanafunzi kuondoka na mali yao wamalizapo shule. haingii akilini mtu mzima kubeba hata kitasa!!!!
 
Hivi hizo thamani za ofisi zilinunuliwa na pesa ya CCM au ni kodi za wananchi walala hoi? Shame on you Masha!! Such a low move, that grounded you to the floor!!
 
Nahisi Masha anaweza hata kuondoka na salio la hela la wizara yake Benk ili waziri mpya aanzie kwenye sifuri. Dah hii kali.

Sasa kitasa kibovu na picha ya kikwete kachukua vya nini?
 
And someone tells me that Mr Masha is eduacted person with such a kind of misleading action. Watu hawajielewi tatizo Tanzania yetu hii, unakuta mtu anaenda tu bila kukutana na tatizo toka azaliwe na wala hataki kujifunza kutoka kwa wenye matatizo matokeo yake anakuwa kama chizi akikutana na negativity kama hizi.
He is still young, he has to learn how to live with other people, kwani hao hao anaowaona hawafai ndo siku yake ya mwisho watamsindikiza tena bila kukumbuka matendo yake kwa saana.
 
Aisee huyo jamaa ni mwizi kinoma halafu hana uvumilivu wa kisiasa,
mfano hivi karibuni katwangwa mangumi na kudondosha meno kadhaa.
Nawasilisha.
 
mbona mnamsakama sana huyu mkuu! hujawahi kuwa na demu halafu mkiachana unadai vitu vyako ulivyo mhonga
 
Nyamagana sasa anzeni kazi ya kujenga jimbo. Acheni porojo za hapa na pale. Wenzenu Arusha wameanza kazi, Ubungo tumepata vipaumbele vyao. Nyinyi mnagombania furniture. Mbunge mpya unatia aibu.
 
Nyamagana sasa anzeni kazi ya kujenga jimbo. Acheni porojo za hapa na pale. Wenzenu Arusha wameanza kazi, Ubungo tumepata vipaumbele vyao. Nyinyi mnagombania furniture. Mbunge mpya unatia aibu.
Mheshimiwa hapa hoja sio kugombania furniture na kama unadhani kauli hii itaufuta ukweli wa aibu inayofanywa na wana ccm hauipenda ccm na tena unaisaliti. Hawa watu wamezidi kukipotezea chama credibility mzee. Kuna jambo muhimu sana hapa. Who is the owner of the MP's offices in Tanzania?? NI muhimu kujua Mbunge sio Masha Wenje wala Mbega, Mbunge ni title inayoshemiwa na inayolinda maslahi ya umma. Hatutarajii Title hii iwe mali ya mtu kama unavyotaka kutuaminisha. Title hii ina ofisi na budget yake. Masha kwa kitendo chake ni zaidi ya mwizi ni mhaini wa nyaraka za nchi,
 
mbona mnamsakama sana huyu mkuu! hujawahi kuwa na demu halafu mkiachana unadai vitu vyako ulivyo mhonga
Demu ni suala la binafsi ingawa pia watu wastarabu hawadai kitu unaishia kimya kimya. OFISI YA MBUNGE NI MALI YA UMMA WA WATU INAYOLINDA MASLAHI YA UMMA. Kama kila mbunge akinunua furniture zake na kuondoka nazo then Ubunge hautakuwa na maana yoyote katika taifa
 
Aibu!! Sijui anavipeleka wapi.....
<br />
<br />
Nahisi atakuwa anapeleka nyumbani kwake akaanziye maisha mapya bila uheshimiwa. Duh! Afrika ya kina Nkwame, Nyerere, Patrick, Nkeni Salawiwa, sijui imepotezwa na nani, na ni jinsi gani tunaweza kuirejesha, kama hali ndo hiiiiiiiiiiiiiii
 
Ndugu zangu nimepatwa na mshangao mkubwa kuona aliyekuwa WAZIRI WA MAMBO YA NDANI (USALAMA WA RAIA) na mwanasheria kwa taaluma kuondoka na samani za OFISI YA MBUNGE WA BUNGE LA JMT.
Naomba kusaidiwa tu kujua je amechukuliwa hatua gani na serikali kwa kupora mali ya Umma? CCM kama chama wamemchukulia hatua gani kwa aibu aliyokiletea chama?
Kama huyu ndiye alikuwa analinda usalama na mali zetu Je tuna hakika gani kuwa ametuacha salama kama taifa?,
Naomba mnisaidie kuelewa hayo tu kwa leo

Alisema alivinunua kwa pesa zake, case closed!
 
Back
Top Bottom