Ofisi ya DC Arusha yakosa choo,kilichopo chaziba na kutapakaza vinyesi na harufu kali.

Arusha Leo

Senior Member
Mar 12, 2012
122
72
Ofisi ya mkuu wa wilaya ya Arusha imekumbwa na aibu ya mwaka baada ya uongozi kushindwa kukarabati choo cha jengo hilo kilichoziba kwa muda mrefu ,ambapo kwa sasa kimefurika maji machafu na kinyesi na kutiririsha eneo la ofisi hiyo na kuwafanya watumishi wa jengo hilo akiwemo DC, Raymond Mushi kuingia ofisini akiwa ameziba mdomo na kitambaa huku wakikanyaka maji machafu yaliyotapakaa kila pembe.
 
Inaelekea fedha za matengenezo walisaidia wilaya jirani ya Arumeru kwenye uchaguzi,tukiwaambia hawawezi kazi wanasema kauli za uchochezi,DC mzima anakalia mavi halafu huyo useme atasimamia usafi wa manispaa ya Arusha kweli DC Raymond Mushi HOVYOOOO
 
Nafikiri swala la vyoo kufurika hapa A.town ni fashion mpya ya meya kaja nayo kwani karibu mji mzima vyoo vimefurika na hamna anayejali labda viongozi wa manispaa wanapenda hiyo harufu.
 
Back
Top Bottom