Ofisi ya CCM yafungwa na kugeuzwa ya CHADEMA:CCM yapoteza Mali na wanachama

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Katika tukio ambalo halikutarajiwa na la kushangaza vijana zaidi ya 50 waliokuwa wanachama wa CCM Tawi la Cairo mjini Mererani wilayani Simanjiro mkoani Manyara wameishusha bendera ya Tawi hilo na kuipandisha ya CHADEMA huku kila kitu ikiwemo ofisi,samani na wanachama wote kuhamia CHADEMA.

Wanachama hao wamesema wameamua kufanya tukio hilo la kushangaza kutokana na kudai kwamba CCm imepoteza dira na mwelekeo hadi kusababisha maisha kuzidi kuwa magumu na mfumuko wa bei.Pia wamesema wameamua kumuunga mkono aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Arusha James Ole Millya aliyejiondoa CCM na kujiunga na CHADEMA mwezi uliopita.

Akizungumzia tukio hilo kiongozi wa CCM kata hiyo Sifael Saitore mbali ya kushtushwa na tukio hilo aliahidi kutafuta kiwanja sehemu nyingine kwa ajili ya kujenga ofisi mpya ya Tawi kwani awali Tawi hilo lililojiunga na CHADEMA halikuwa katika eneo linalomilikiwa na CCM.

Source:Mwananchi Ijumaa Uk.10
 
Ndicho CCM walichotaka.Wameshindwa kabisa kusoma alama za nyakati hata baada ya watu kutoa ushauri mwingi wa bure.Ni watu wa ajabu sana,maana hata sasa bado hawajastuka,it's business as usual.
Katika tukio ambalo halikutarajiwa na la kushangaza vijana zaidi ya 50 waliokuwa wanachama wa CCM Tawi la Cairo mjini Mererani wilayani Simanjiro mkoani Manyara wameishusha bendera ya Tawi hilo na kuipandisha ya CHADEMA huku kila kitu ikiwemo ofisi,samani na wanachama wote kuhamia CHADEMA.
Wanachama hao wamesema wameamua kufanya tukio hilo la kushangaza kutokana na kudai kwamba CCm imepoteza dira na mwelekeo hadi kusababisha maisha kuzidi kuwa magumu na mfumuko wa bei.Pia wamesema wameamua kumuunga mkono aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Arusha James Ole Millya aliyejiondoa CCM na kujiunga na CHADEMA mwezi uliopita.
Akizungumzia tukio hilo kiongozi wa CCM kata hiyo Sifael Saitore mbali ya kushtushwa na tukio hilo aliahidi kutafuta kiwanja sehemu nyingine kwa ajili ya kujenga ofisi mpya ya Tawi kwani awali Tawi hilo lililojiunga na CHADEMA halikuwa katika eneo linalomilikiwa na CCM.

Source:Mwananchi Ijumaa Uk.10
 
Watu wa Mererani walikuwa mtaji mkubwa wa CCM. Sasa kama na ofisi imehamishiwa CHADEMA CCM bye bye!

Msako Unaendelea
 
sasa hatuwanyatii tena na wala hatuwafukuzi kimya kimya,hiki ndicho kimbunga lichosema Mheshimiwa Sugu,baada ya hiyo ofisi tutafuatia viwanja vyote vya michezo virudishwe serikalini iweje wajenge wote leo waseme vyao
 
Ndiyo maana hata kiongozi wa ccm wa kata amekiri kushtushwa na tukio hilo
 
Back
Top Bottom