Ofisi ya Bunge yatoa taarifa juu ya habari iliyochapishwa na gazeti Mtanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ofisi ya Bunge yatoa taarifa juu ya habari iliyochapishwa na gazeti Mtanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by EMT, Jun 21, 2011.

 1. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #1
  Jun 21, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  YAH: TAARIFA POTOFU YA GAZETI LA DIRA YA MTANZANIA TOLEO LA JUMATATU, 20 – 26 JUNI, 2011 ' SAKATA LA POSHO ZA WABUNGE' SPIKA MAKINDA MBUMBUMBU ‘Utafiti wabainianasimamia asichokijua magwiji wa Bunge washangaa tamko lake'.

  1.0 UTANGULIZI

  Ofisi ya Bunge laJamhuri ya Muungano wa Tanzania imesikitishwa sana na habari potofu na yenye dharau iliyochapishwa na gazeti la Dira ya Mtanzania, lenye usajili ISSN No.1821-641, Toleo Namba 89 la Jumanne Juni 20 -26, 2011 lenye kichwa cha habari'SAKATA LA POSHO ZA WABUNGE' SPIKA MAKINDA MBUMBUMBU pamoja na vichwa vidogovya habari vyenye kusomeka ‘Utafiti wabaini anasimamia asichokijua' magwiji waBunge washangaa tamko lake' nk katika ukurasa wake wa kwanza na iliyoendeleapia katika Ukurasa wa 2.

  Pamoja na Vichwa vyahabari hiyo, Katika taarifa hiyo Mwandishi wa gazeti hilo amedai kuwa;

  i. Spika wa Bunge, Anne Makinda hana uelewa wa kutosha wa jinsi mbunge anavyoweza kupoteza wadhifa wake

  ii. Pia Spika wa Bunge haelewi mfumo wa malipo ya Posho za Wabunge.
  iii. Spika hana mamlaka ya kumfukuza Mbunge yeyote anayekataa kusaini Fomu za kuchukua posho ya kikao.

  2.0 MAJIBU YA HOJA POTOFUZILIZOTOLEWA

  Ofisi ya Bunge ingependa kuwaarifu wananchi kwamba habari hiyo iliyoandikwa na gazeti la Diraya Mtanzania ni ya dharau na haina ukweli wowote na imeandikwa kwa nia mbaya yauchochezi na kuharibu sifa aliyo nayo Mhe. Spika Bungeni na kwa Watanzania kwaujumla.

  Ili kuondoa upotofu wa taarifa iliyotolewa na gazeti hili, Ofisi ya Bunge ingependa kutoa ufafanuzi wa hoja zilizotolewa kama ifuatavyo;

  i. Sio kweli kwamba Mhe. Anne Makinda hana uelewa kuhusu uendeshaji wa shughuli za Bunge. Mhe.Makinda amekuwa mbunge kwa zaidi ya miaka 30 Bungeni na kwa kipindi hicho chote ameshika nyadhifa mbalimbali Bungeni na Serikalini. Aidha akiwa Naibu Spika ameongoza kamati ya Bunge iliyoshiriki marekebisho ya Kanuni za Kudumu za Bungetoleo la 2007.

  Kwa mantiki hiyo anazifahamu vyema Kanuni za Bunge na ana uzoefu na uendeshaji wa shughuli za Bunge kwa muda mrefu kuliko hata idadi kubwa ya wabunge wapya waliopo Bungeni. Katika utendaji wake, hafanyi kazi kwa kuvutwa na hisia bali husimamia uendeshaji wa Bunge kwa Mujibu wa Kanuni za Bunge ambazo tuna shaka hata kama mwandishi wa gazeti hili anazifahamu vyema.

  Ni kwa kuzingatia hilo aliwaeleza bayana Waandishi wa habari siku alipofanya nao mahojiano ambapo mwandishi wa gazeti hili pia hakuwepo, kuwa taratibu la kuchukua posho kwaMbunge huenda sanjali na kusaini mahudhurio Bungeni (Mbunge anayehudhuria Bungendiye anayelipwa posho), kwa maana huwezi kumlipa posho Mbunge asiyekuwepo Bungeni. Mahudhurio ya Mbunge ni pale anaposaini fomu ya Mahudhurio. Kwa mantiki hii, kanuni zinamtaka bayana kila mbunge kuhudhuria vikao vya Bunge.


  Kanuni ya 143 inatamka kuwa:
  (1) kuhudhuria vikao vya Bunge na kamati ni wajibu wa kwanza wa kila mbunge.
  (2) Mbunge yeyote atakaeshindwa kuhudhuria mikutano ya Bunge mitatu mfululizo bila ruhusa ya Spika iliyotolewa kwa maandishi, atapoteza Ubunge wake kwa mujibu wa ibara ya 7 (1) ya katiba na Spika ataiarifu Tume ya Uchaguzi.
  (3) Mbunge atakapokosa kuhudhuria nusu ya vikao vya Mkutano mmoja bila ya sababu ya msingi atapewa onyo.
  Hivyo basi kwa mantiki hiyo, Mbunge atakayeshindwa kusaini fomu za mahudhurio kwa mtiririko huo hapo juu atakuwa amepoteza sifa zake za kuwa Mbunge kwa mujibu wa Kanuni.

  ii. Aidha ni kwa uvivu wa kufikiri au kwa makusudi kabisa, mwandishi wa gazeti hili ameandika yale aliyohisi ni sahihi na kufanya utafiti katika kiwango ambacho hajaeleza nikwa kutumia vigezo gani bila hata kujaribu kuuliza misingi halisi aliyoizungumzia Mhe. Spika kuhusu uhalali wa mahudhurio ya Mbunge sanjali na ulipwaji wake posho awapo kazini.

  Hivyo madai ya kuwa Spika hana madaraka ya kumfukuza Mbunge Bungeni hayana mantiki na wala madaraka ya Spika kuhusu kumfukuza Mbunge hayakuwa sehemu ya mahojiano na waandishi na Spika wa Bunge kama anavyodai, na Kanuni zimeeleza bayana kazi za Spika Bungeni. Kumbuka madaraka ya Spika, wajibu wa Wabunge na hata Miongozo mingine Bungeni huratibiwa kwa mujibu wa kanuni za Kudumu za Bunge.

  Hatujui lengo la mwandishi ni lipi hasa kwa kuweza kutoa taarifa zenye upotoshaji mkubwa kwaumma na zenye kuleta dharau kwa kiongozi wa Bunge na Bunge kwa ujumla kwa kuzingatia kuwa kiongozi huyu amechaguliwa na Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano.

  3.0 HITIMISHO

  Ofisi ya Bunge inapenda kuwaarifu wanahabari wote kuwa Idara yake ya Habari imekuwa ikitoa ushirikiano wa kutosha kuwaarifu waandishi kwa taarifa zozote wanazohitaji na inasikitishwakwa kiasi kikubwa na uandishi unaojali hisia na wenye kulenga uchochezi badala ya kuelemisha.

  Licha ya mwandishi wahabari hii kutokuwepo Dodoma na wala hakushiriki mahojiano hayo na Mhe. Spika, habari husika iliyoandikwa imelenga kutoa taarifa potofu bila kushirikisha hata upande wa pili kwa ufafanuzi. Kwa kuzingatia hilo Ofisi ya Bungeina mtaka Mhariri wa Gazeti la Dira ya Mtanzania kuomba radhi kwa uzito ule ule waliotoa habari yao ya kupotosha umma.

  Deogratios Egidio
  Kny: KATIBU WA BUNGE
  21 Juni, 2011

  NB: Kumradhi kwenye heading ya thread inatakiwa kuwa gazeti la Dira ya Tanzania.

   
 2. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #2
  Jun 21, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  hawajui namna kuweka paragraph kwenye kuandika basua au ndio u=kuumizana macho?
   
 3. M

  Marytina JF-Expert Member

  #3
  Jun 21, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  MAKINDA ni mbumbumbu kweli Mtanzania halijakosea[HR][/HR]
   
 4. mfereji maringo

  mfereji maringo JF-Expert Member

  #4
  Jun 21, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 1,003
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  miaka thelathini aliyotumikia bi kiroboto alikuwa anawaongoza vilaza wa magamba ambao siku zote walikuwa wanapitisha kila kilicholetwa bungeni na serikali, sasa mziki wa chadema hauwezi na kama nyie mnamuona yuko fair basi si hivyo tunavyomuona huku site, tunawasubiri 2015 tuendelee kuwapunguza pengine hiyo ndiyo itakuwa dawa ya kuibeba serikali badala ya kuisimamia.
   
 5. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #5
  Jun 21, 2011
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 520
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Sasa wanasema anajua wakati kila mtu anamjua ni mbumbumbu? Alinivunja mbavu wakati aliposema yeye ni mtaalam wa sheria eti kwa sababu alisoma course ya business Law, wakati akisoma uhasibu pale TIA!
   
 6. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #6
  Jun 21, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,791
  Likes Received: 2,399
  Trophy Points: 280
  Mbona haijatoa siku za kuomba radhi?asipoomba radhi hatua gani zitachukuliwa?
   
 7. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #7
  Jun 21, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  [​IMG]

  YAH: TAARIFA POTOFU YA GAZETI LA DIRA YA MTANZANIA TOLEO LA JUMATATU, 20 – 26 JUNI, 2011 ‘ SAKATA LA POSHO ZA WABUNGE’ SPIKA MAKINDA MBUMBUMBU ‘Utafiti wabaini anasimamia asichokijua magwiji wa Bunge washangaa tamko lake’.

  1.0UTANGULIZI
  Ofisi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesikitishwa sana na habari potofu na yenye dharau iliyochapishwa na gazeti la Dira ya Mtanzania, lenye usajili ISSN No. 1821-641, Toleo Namba 89 la Jumanne Juni 20 -26, 2011 lenye kichwa cha habari ’SAKATA LA POSHO ZA WABUNGE’ SPIKA MAKINDA MBUMBUMBU pamoja na vichwa vidogo vya habari vyenye kusomeka ‘Utafiti wabaini anasimamia asichokijua’ magwiji wa Bunge washangaa tamko lake’ nk katika ukurasa wake wa kwanza na iliyoendelea pia katika Ukurasa wa 2.
  Pamoja na Vichwa vya habari hiyo, Katika taarifa hiyo Mwandishi wa gazeti hilo amedai kuwa;

  i.Spika wa Bunge, Anne Makinda hana uelewa wa kutosha wa jinsi mbunge anavyoweza kupoteza wadhifa wake

  ii.Pia Spika wa Bunge haelewi mfumo wa malipo ya Posho za Wabunge

  iii.Spika hana mamlaka ya kumfukuza Mbunge yeyote anayekataa kusaini Fomu za kuchukua posho ya kikao.

  2.0MAJIBU YA HOJA POTOFU ZILIZOTOLEWA
  Ofisi ya Bunge ingependa kuwaarifu wananchi kwamba habari hiyo iliyoandikwa na gazeti la Dira ya Mtanzania ni ya dharau na haina ukweli wowote na imeandikwa kwa nia mbaya ya uchochezi na kuharibu sifa aliyonayo Mhe. Spika Bungeni na kwa watanzania kwa ujumla.
  Ili kuondoa upotofu wa taarifa iliyotolewa na gazeti hili, Ofisi ya Bunge ingependa kutoa ufafanuzi wa hoja zilizotolewa kama ifuatavyo;

  i. Sio kweli kwamba Mhe. Anne Makinda hana uelewa kuhusu uendeshaji wa shughuli za Bunge. Mhe. Makinda amekuwa mbunge kwa zaidi ya miaka 30 Bungeni na kwa kipindi hicho chote ameshika nyadhifa mbalimbali Bungeni na Serikalini. Aidha akiwa Naibu Spika ameongoza kamati ya Bunge iliyoshiriki marekebisho ya Kanuni za Kudumu za Bunge toleo la 2007.

  Kwa mantiki hiyo anazifahamu vyema Kanuni za Bunge na ana uzoefu na uendeshaji wa shughuli za Bunge kwa muda mrefu kuliko hata idadi kubwa ya wabunge wapya waliopo Bungeni. Katika utendaji wake, hafanyi kazi kwa kuvutwa na hisia bali husimamia uendeshaji wa Bunge kwa Mujibu wa Kanuni za Bunge ambazo tunashaka hata kama mwandishi wa gazeti hili anazifahamu vyema.

  Ni kwa kuzingatia hilo aliwaeleza bayana Waandishi wa habari siku alipofanya nao mahojiano ambapo mwandishi wa gazeti hili pia hakuwepo, kuwa taratibu la kuchukua posho kwa Mbunge huenda sanjali na kusaini mahudhurio Bungeni (Mbunge anayehudhuria Bunge ndiye anayelipwa posho), kwa maana huwezi kumlipa posho Mbunge asiyekuwepo Bungeni.

  Mahudhurio ya Mbunge ni pale anaposaini fomu ya Mahudhurio. Kwa mantiki hii, kanuni zinamtaka bayana kila mbunge kuhudhuria vikao vya Bunge.

  Kanuni ya 143 inatamka kuwa:

  (1) kuhudhuria vikao vya Bunge na kamati ni wajibu wa kwanza wa kila mbunge.

  (2) Mbunge yeyote atakaeshindwa kuhudhuria mikutano ya Bunge mitatu mfululizo bila ruhusa ya Spika iliyotolewa kwa maandishi, atapoteza Ubunge wake kwa mujibu wa ibara ya 71 (1) ya katiba na Spika ataiarifu Tume ya Uchaguzi.

  (3) Mbunge atakapokosa kuhudhuria nusu ya vikao vya Mkutano mmoja bila ya sababu ya msingi atapewa onyo.

  Hivyo basi kwa mantiki hiyo, Mbunge atakayeshindwa kusaini fomu za mahudhurio kwa mtiririko huo hapo juu atakuwa amepoteza sifa zake za kuwa Mbunge kwa mujibu wa Kanuni.
  ii. Aidha ni kwa uvivu wa kufikiri au kwa makusudi kabisa, mwandishi wa gazeti hili ameandika yale aliyohisi ni sahihi na kufanya utafiti katika kiwango ambacho hajaeleza ni kwa kutumia vigezo gani bila hata kujaribu kuuliza misingi halisi aliyoizungumzia Mhe. Spika kuhusu uhalali wa mahudhurio ya Mbunge sanjali na ulipwaji wake posho awapo kazini.

  Hivyo madai ya kuwa Spika hana madaraka ya kumfukuza Mbunge Bungeni hayana mantiki na wala madaraka ya Spika kuhusu kumfukuza Mbunge hayakuwa sehemu ya mahojiano na waandishi na Spika wa Bunge kama anavyodai, na Kanuni zimeeleza bayana kazi za Spika Bungeni. Kumbuka madaraka ya Spika, wajibu wa Wabunge na hata Miongozo mingine Bungeni huratibiwa kwa mujibu wa kanuni za Kudumu za Bunge.

  Hatujui lengo la mwandishi ni lipi hasa kwa kuweza kutoa taarifa zenye upotoshaji mkubwa kwa umma na zenye kuleta dharau kwa kiongozi wa Bunge na Bunge kwa ujumla kwa kuzingatia kuwa kiongozi huyu amechaguliwa na Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano.

  3.0 HITIMISHO
  Ofisi ya Bunge inapenda kuwaarifu wanahabari wote kuwa Idara yake ya Habari imekuwa ikitoa ushirikiano wa kutosha kuwaarifu waandishi kwa taarifa zozote wanazohitaji na inasikitishwa kwa kiasi kikubwa na uandishi unaojali hisia na wenye kulenga uchochezi badala ya kuelemisha.

  Licha ya mwandishi wa habari hii kutokuwepo Dodoma na wala hakushiriki mahojiano hayo na Mhe. Spika, habari husika iliyoandikwa imelenga kutoa taarifa potofu bila kushirikisha hata upande wa pili kwa ufafanuzi. Kwa kuzingatia hilo Ofisi ya Bunge inamtaka Mhariri wa Gazeti la Dira ya Mtanzania kuomba radhi kwa uzito ule ule waliotoa habari yao ya kupotosha umma.

  Deogratios Egidio
  Kny: KATIBU WA BUNGE
  21 Juni, 2011
   
 8. Mkuu wa chuo

  Mkuu wa chuo JF-Expert Member

  #8
  Jun 21, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,255
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Eti kuharibu sifa nzuri ya spika!!! Kwani spika wa kwanza mwanamke ana sifa gani nzuri aliyojijengea hakuna kitu kama hicho, wasitake kutudanganya!
   
 9. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #9
  Jun 21, 2011
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  MY TAKE: Dada Makinda hana uelewa wa namna mbunge anavyoweza kupoteza ubunge wake, na pili ofisi ya katibu wa bunge nayo haina uelewa kwa namna ambavyo mbunge anavyoweza kupoteza ubunge wake, kwa hiyo basi Speaker na katibu wote wawili hawana uelewa na kulifanya bunge zima wanaloliongoza liongozwe kwa hisia zaidi kuliko kufuata kanuni. Nasema hiyo kwasababu kanuni waliyoiquote imetamka wazi kama Mbunge atakayeshindwa kuhudhuria mikutano 3 mfululizo bila ruhusa ya maandishi ya spika atapoteza nafasi yake ya ubunge. Kanuni haijasema kuwa mbunge atathibitishwa kuwa ameshiriki au kutoshiriki kikao au mikutao ya bunge kwa kusaini daftari la mahudhurio. Daftari la mahudhurio ni utaratibu uliowekwa bila kanuni yoyote ya bunge hivyo kutosaini katika daftari la mahudhurio hutakuwa umevunja kanuni yoyote ya bunge. Utaratibu wa daftari la mahudhurio umewekwa na katibu w abunge kw aridhaa yake mwenyewe kumrahisishia kuratibu shughuri za malipo ya posho za wabunge. Kwa maana hiyo Anna Makinda ameonyesha umbumbu wa wazi wazi wa hata kanuni inayosemeka na kujieleza vizuri kirahisi kwa kiswahili rahisi. Kama mtu atakuwa ameshindwa kuhudhuria mikutano ya bunge 3 na haijasemwa kuwa kuhudhuria kutathibitishwa na daftari la mahudhurio.
   
 10. M

  Mghaka JF-Expert Member

  #10
  Jun 21, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 320
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Anaweza kukanusha ya kwenye gazeti lakini hawezi kufuta vichwani mwa watanzania juu ya kushindwa kumudu kazi kwa` spika wa bunge la jamhuri ya muungano. Makinda amepata usipika lakini nafasi ya usipika haijapata mwenyewe. Jadili mtakavyo na mpendavyo ukweli wa nafasi ya spika umeandikwa kwenye miyo ya watanzania
   
 11. L

  Lufu lwa ndama New Member

  #11
  Jun 21, 2011
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mahudhurio ya Mbunge ni pale anaposaini fomu ya Mahudhurio. Kwa mantiki hii, kanuni zinamtaka bayana kila mbunge kuhudhuria vikao vya Bunge.
  Kanuni ya 143 inatamka kuwa:

  (1) kuhudhuria vikao vya Bunge na kamati ni wajibu wa kwanza wa kila mbunge.

  (2) Mbunge yeyote atakaeshindwa kuhudhuria mikutano ya Bunge mitatu mfululizo bila ruhusa ya Spika iliyotolewa kwa maandishi, atapoteza Ubunge wake kwa mujibu wa ibara ya 71 (1) ya katiba na Spika ataiarifu Tume ya Uchaguzi.

  (3) Mbunge atakapokosa kuhudhuria nusu ya vikao vya Mkutano mmoja bila ya sababu ya msingi atapewa onyo.

  Ukiisoma hii kanuni ya 143 kama ilivyonukuliwa hapo juu sioni sehemu yoyote inayotaka mbunge asign form ya mahudhurio labda mi mwenzenu nina makengeza!!.Pia sidhani kama uthibitisho wa mbunge kuwepo kiakoni ni kusign form!!je mbunge atakayeingia kikaoni bila hata kujaza hizo form zao na kushuhudiwa na watu kuwa alikuwepo au kwa upande mwingine aliweza hata kuchangia hoja je, mbunge huyu ataadhibiwa kuwa hakuwepo?pia kama wanavyotuambia siku hizi kuwa wabunge wanaingia kwa kadi maalumu milangoni hasa kuingia ukumbi wa bunge ina maana taarifa za kadi za wabunge husika si zinakuwepo sasa kwa nini hili la form linang'ang'aniwa sana!!!
   
 12. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #12
  Jun 21, 2011
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,992
  Likes Received: 3,741
  Trophy Points: 280
  Kama nukuu ya kanuni 143 hapo juu imekamilika jinsi inavyoonekana, basi ni kanuni KIMEO......

  Imetamka lazima wabunge wahudhurie vikao lakini haisemi lazima wa-SIGN IN!

  So Zitto & co wanaweza kuhudhuria vikao bila kulazimika kujiorodhesha kwani evidence ya physical presence yao bungeni tayari itakuwa ipo captured kwenye ELECTRONIC MEDIA!

  Huyu bibi atajiua kwa pressure bure!!
   
 13. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #13
  Jun 21, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,496
  Likes Received: 19,901
  Trophy Points: 280
  wanatapatapa
   
 14. c

  chelenje JF-Expert Member

  #14
  Jun 21, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 554
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wakuu, bi kiroboto ndo nani?????
   
 15. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #15
  Jun 21, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,249
  Likes Received: 3,836
  Trophy Points: 280
  Hakika kabisa!!
   
 16. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #16
  Jun 21, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Kwa mantiki hii basi, hata huyu anastahili posho kwa kusaini na kwenda kupiga mbonji. Huyu ana tofauti gani na asiyekuja bungeni kabisa?

  [​IMG]
   
 17. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #17
  Jun 21, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Daaa.....wamekanusha kwa nguvu zooote.......lakini kwakweli bi mkubwa AMEPWAYA
   
 18. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #18
  Jun 21, 2011
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Kumbe kanuni zimewekwa kulazimisha posho! Ningetegemea kanuni inayolazimisha Mbunge kushiriki ktk mijadala kwa dhati na kutoa mchango wake kama mwananchi anavyotegemea .....
   
 19. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #19
  Jun 21, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Hapo kwenye RED Hilo Gazeti hawajakosea ni ukweli walichokiandika
   
 20. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #20
  Jun 21, 2011
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,992
  Likes Received: 3,741
  Trophy Points: 280
  Taratibu mkuu.....hivi unajua huyu bibi anatokea lile kabila la watani wangu ambao kujining'iniza ni kitu rahisi sana?? Ohooo!
   
Loading...