Ofisi ya Ardhi Jiji la Dodoma imezidiwa na wateja au kuna uzembe?

Chendembe

JF-Expert Member
Oct 20, 2019
416
462
Wanabodi, napenda kupata uzoefu kwenu kuhusu hali ya msongamano wa watu wa kila siku za kazi za juma katika Idara hii ya Ardhi Jijini Dodoma ambayo haipunguwi kama wagonjwa wanaokwenda kutibiwa hospitali wakati wa mlipuko.

Nimekuwa mhanga pia wa kuhudhulia katika ofisi hiyo kwa Jambo moja kushindwa kuona faili la kiwanja changu ambacho nimekilipia mwanzoni mwa 2020 lakini Hadi naandika hapa, sijapata barua na viambatisho vya kupeleka kwa kamishina wa Ardhi.

Kwakweli ni kero. Hali siyo shwari katika idara hiyo.
 
Kimsingi Dodoma hawakustahili kuwa na Jiji. Wangebakia tu kuwa Manispaa, labda mpaka baada ya miaka 10 mbele ndiyo wangepewa hadhi ya kuwa Jiji!😇
 
Dodoma wamepima maelf ya viwanja na wakalipa kidogo wakasepa...sasa wanahangaika kuwasaka walipe hela.
Walionunua walijua watauza baadae ila biashara imebuma
 
Dodoma wamepima maelf ya viwanja na wakalipa kidogo wakasepa...sasa wanahangaika kuwasaka walipe hela.
Walionunua walijua watauza baadae ila biashara imebuma
Hilo tuliliona hapo awali. Mwaka huo Jiji lilikusanya mapato mengi na kupewa sifa kedekede. Ila tulisema hii biashara baada ya muda itakosa wateja. Kwa sasa uie moto wa kuhamia Dodoma umeanza kufifia. Na hivyo mararajio ya wengi ya kuweza kupiga pesa kwa kuwalangua wahamiaji tarajiwa yakayeyuka kama theluji.
 
Yeah kuna tatizo na ule mfumo wao wa kuwahi vikadi, kutibiwa kwa foleni kwa maana ya kadi zikiisha hakuna huduma, wahi kesho upange foleni ya kadi au walinzi wakusaidie kuingia ndani na hii ina pelekea mambo ya kitu kidogo...

Uviko nayo imekuja na mengi
 
Back
Top Bottom