Ofisa wa Ethiopia apongeza kampuni za China kwa kutekeleza majukumu ya kijamii

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,000
1,019
Serikali ya Ethiopia imepongeza kampuni za China kwa juhudi zao za kutekeleza majukumu ya kijamii nchini humo.

Taarifa hiyo imetolewa na naibu meya wa Addis Ababa Bw. Yasmin Wohabrebbi kwenye hafla ya kukamilika kwa ujenzi wa barabara ya Mekanisa Abo. Mradi huu umefadhiliwa na kujengwa na kampuni ya CCECC ya China, ukiwa sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake ya kijamii.

Bw. Wohabrebbi amesema, hatua hiyo ikiwa sehemu ya utekelezaji wa majukumu ya kijamii ya kampuni ya kimataifa kama CCECC ni jambo linalopongezwa na serikali, kwa kuwa maendeleo yote hayawezi kusimamiwa tu na serikali.

Pia amesema, serikali inatia moyo sekta binafsi na kampuni za kimataifa kushiriki kwenye shughuli zinazofanana na hiyo, kwa sababu zitasaidia kuhimiza maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya nchi hiyo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom