Ofisa Usalama wa Taifa atumbukia ufisadi BoT | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ofisa Usalama wa Taifa atumbukia ufisadi BoT

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Feb 3, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Feb 3, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,759
  Likes Received: 82,735
  Trophy Points: 280

  Ofisa Usalama wa Taifa atumbukia ufisadi BoT
  Waandishi Wetu, Dodoma
  Daily News; Saturday,February 02, 2008 @19:01

  KAMPUNI mbili ambazo zimetumiwa kuchota mabilioni Benki Kuu (BoT) zimegundulika kuwa zinamilikiwa na Ofisa wa Idara ya Usalama wa Taifa mwenye cheo cha juu kabisa. Kampuni hizo ni Clayton Marketing Ltd na Excellent Services Ltd ambazo ni miongoni mwa kampuni 22 zilizotumiwa kuiba Sh bilioni 133 za BoT kupitia Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA).

  Habari zimeeleza kuwa ofisa mmoja wa ngazi ya juu ndani ya idara hiyo ndiye anatajwa kama mmoja wa wakurugenzi. Habari za uhakika ambazo gazeti hili limezipata zinaeleza kuwa kampuni hizo zilitumiwa kuchota kiasi kikubwa cha fedha kwa kisingizio cha kazi maalumu ya kitaifa.

  Kampuni ya Clayton inatajwa kuchota kwa wakati mmoja dola za Marekani 500,000 kutoka Benki Kuu. "Nyaraka tu iliandikwa kwenda Benki Kuu kwamba tafadhali lipa hizo pesa kwa kazi maalumu, unajua wakati huo hatukujua hizo fedha zinakwenda wapi, sasa tunafahamu," kilidokeza chanzo kimoja cha habari.

  Kampuni hizo mbili ni miongoni mwa kampuni zilizolipwa Sh bilioni 42.9 na hakuna nyaraka yoyote iliyowasilishwa kuthibitisha malipo hayo. Kampuni zingine katika kundi hilo ni G&T International Ltd, Mibale Farm, Liquidity Service Ltd, M/S Rashtas (T) Ltd, Kiloloma and Brothers, Karnel Ltd na Malegesi Law Chambers (Advocates) inayomilikiwa na Bedery Malegesi.

  Pia gazeti hili limebaini kuwa ofisa huyo kutokana na nafasi yake, ni miongoni mwa watu ambao idara yake imehusishwa katika kuundwa kwa tume maalumu iliyoundwa na Rais Jakaya Kikwete kuchunguza tuhuma hizo. "Kwa kazi yake yeye ni mtu mkubwa katika kamati ile kwani ndiye anayeshughulikia masuala yote ya kigaidi, kiuhalifu wa kimataifa ndani ya Idara ya Usalama wa Taifa," kilidokeza chanzo chetu cha habari.

  Mwenyekiti wa kuchunguza ufisadi huo, John Mwanyika alipofuatwa na gazeti hili mjini Dodoma aeleze uhusiano wa Ofisa huyo wa Usalama wa Ikulu na kamati yake alisema kwamba hamfahamu huyo mtu na kamati yake inahusisha watu watatu na wala haihusishi watu wa Usalama wa Taifa.

  "Sina taarifa za hizo kampuni unazoniuliza na wala huyo mtu simfahamu," alisema Mwanyika wakati akizungumza na gazeti hili ambalo lilitaka ufafanuzi kama ofisa huyo anahusika kwenye kamati yake. Tume ya kuchunguza suala hilo inaongozwa na Mwanasheria Mkuu kwa kushirikiana na Mkuu wa Polisi na Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa.

  Lakini vyanzo vya habari vilithibitisha kuwa Ofisi ya Usalama wa Taifa imeombwa kuhusishwa katika kuchunguza suala hilo kama ambavyo imekuwa inashiriki katika matukio mengine ya uhalifu. Kampuni ya Excellent Service Ltd ambayo imesajiliwa kama inashughulika na masuala ya upokeaji na usafirishaji wa mizigo, wakurugenzi wake wakati huo walimiki asilimia 100 kila mmoja akiwamo Ofisa Usalama huyo.

  Kampuni hiyo ofisi zake zinaelezwa kuwa ziko Mtaa wa Sokoine kitalu namba 11649. Oktoba 5, 2004 mwenzake alijiuzulu na akateuliwa mtu anayeitwa Massimo Fanneli kuwa Mkurugenzi. Hisa za Sabbas ambazo ni 100 zilihamishiwa kwa Fannel baada ya kulipwa Sh milioni 5. Kampuni hiyo hadi kufikia Desemba 19 mtaji wake uliongezeka kutoka 500,000 hadi kufikia milioni 5.

  Alipotakiwa kuzungumzia kama kampuni zilizoanzishwa na Ofisa Usalama huyo zilikuwa ni kwa ajili ya shughuli za Serikali, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Philip Marmo alisema jana kuwa Serikali haijafikia hatua ya kuanzisha kampuni katika idara yake nyeti ya kama ya Usalama wa Taifa.

  Alisema kutokana na hali hiyo ni wazi kuwa kampuni anazodaiwa kuanzisha ofisa huyo mwandamizi zilizotajwa katika ubadhirifu wa Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) hazihusiani na Idara ya Usalama wa Taifa.

  "Mimi sifahamu kama ana kampuni lakini kwa mujibu wa Azimio la Zanzibar, anaruhusiwa kuwa na kampuni, lakini zisiingiliane na nafasi yake kwa maana asitumie nafasi yake katika uendeshaji wa kampuni zake. Sasa hivi suala hilo la kampuni zilizohusika na ubadhirifu linashughulikiwa na vyombo vya sheria, mimi siwezi ku comment kitu hapo, tusubiri sheria ifanye kazi," alisema.
   
 2. Kafara

  Kafara JF-Expert Member

  #2
  Feb 3, 2008
  Joined: Feb 17, 2007
  Messages: 1,392
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  afisa usalama, mtu huyo nk. hana jina?

  kama magazeti yanashindwa kutaja moja kwa moja
  si waende brela na kuchukua orodha na kumwaga
  majina ya wahusika bila kuonyesha yupi na afisa
  usalama. ninahakika wakuu wa kumkoma nyani giladi
  watamuumbua tuu hapa jf.
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Feb 3, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  sasa kama habari hizi ni za uhakika na vyanzo vyake vimethibitishwa si wangemtaja. Vinginevyo naomba hilo jina mimi nitamtaja. Pleaaase.. but you better back up with some data!
   
 4. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #4
  Feb 3, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Azimio la Arusha lilileta haya ya kuwa na makampuni na huku unatumia Serikali sasa JK kaja na Azimio la Kikwete . Sina uhakika linataka kufanya nini but I think is another hoax.
   
 5. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #5
  Feb 3, 2008
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Ningependa kufahamu jina lake.Ningependa kujua uhusiano waKe na Apson Mwang'onda.Mwenye Data anitumie katika PM na mie nitamuanika hadharani.
   
 6. m

  mwana siasa Senior Member

  #6
  Feb 3, 2008
  Joined: Aug 28, 2007
  Messages: 119
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  ninahisi atakuwa ali siwa, mana huyu bwana ndo alikuwa anahusika na uhalifu.ni hisia tu
   
 7. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #7
  Feb 3, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Majina yote yanatajwa hapa chini:

  Uchunguzi wa gazeti hili unaonyesha kuwa kampuni za Bencom International Ltd, B. V Holdings Ltd, Venus Hotels Ltd, V.B Associates Company Ltd, Bina Rosort Lt na Bora Hotels & Apartment zote zilisajiliwa kwa siku moja.


  Jayantkumar Patel na Devendra Vinodbahi Patel wanatajwa kama wakurugenzi wa kampuni hizo ambazo ziliandikishwa Aprili 4, 2005 zote zikiwa na malengo yanayofanana ya kuagiza na kusafirisha bidhaa mbalimbali nje ya nchi.


  Kampuni zote hizo kila moja imeandikishwa kwa mtaji wa Sh milioni 1, kila kampuni ina hisa 100 ambazo zina thamani ya Sh 10,000 kwa kila hisa moja. Kiasi cha Sh bilioni 133 zimechotwa BoT kwa kutumia kampuni 22 ambazo zililipwa kwa kutumia nyaraka bandia.


  Patel peke yake anamiliki kampuni nyingine tatu hivyo kufanya aongoze katika wizi wa fedha hizo za umma. Katika mwaka 2005, kampuni nyingi zilizotajwa kuchota mabilioni ziliandikishwa na kusajiliwa.


  Kuna kampuni ya Mibale Farms iliandikishwa Septemba 6, 2005, wakurugenzi wake wanatajwa kuwa ni Kiza Selemani na Farijara Hussein, Clayton Marketing Ltd inayomilikiwa na Edwin Mtoi na Elisifu Ngowi na iliandikishwa Juni 6, 2005.


  Mwaka huo huo pia kampuni ya Kiloloma and Brothers iliandikishwa Aprili 14. Mkurugenzi wake anatajwa kuwa ni Charles Kissa. Money Planners & Consultants nayo iliandikishwa Machi 24, 2005 na wakurugenzi wake wanatajwa kuwa ni Paul Nyingo na Fundi Kitunga.


  Lakini kampuni hizo mbili ni za mtu mmoja maana zinatumia ofisi iliyoko mtaa wa Iramba nyumba namba 7 Magomeni, Dar es Salaam ingawa zilisajiliwa kwa makusudi tofauti.


  Moja imesajiliwa kama inashughulika na usambazaji wa vifaa vya ofisini wakati nyingine shughuli yake ni ukusanyaji wa madeni. Mwaka huo wa 2005 kampuni ya Kagoda Agriculture Ltd pia iliandikishwa Septemba 29 na wakurugenzi wake wanatajwa kuwa ni John Kyamuhendo na Francis William.


  Kampuni zingine anazomiliki Patel alizoandikisha miaka ya nyuma ambazo nazo amezitumia kuibia Benki Kuu ni Maltan Mining Company ambayo iliandikishwa Machi 1995. Katika kampuni hiyo Patel aliandikisha kampuni hiyo akiwa na mwanahisa mwingine aliyemtaja kwa jina la Haharier Radhakrishnan.


  Lakini Agosti 29, mwaka huo huo, Patel akabadilisha jina la kampuni hiyo na kuiita Noble Maltan. Hata hivyo, tangu iandikishwe mwaka huo hakuwahi kuwasilisha taarifa ya mizania BRELA kama sheria inavyomtaka hali iliyosababisha msajili huyo kumwandikia barua kumtaka awasilishe mizania hiyo.


  Patel pia ana kampuni nyingine ya Ndovu Soaps Ltd aliyoiandikisha Februari 18, 1992 na tangu wakati huo hakuwahi kuwasilisha wala kulipia taarifa ya mizania. BRELA pia ilimwandikia barua mwaka jana kumtaka awasilishe na kulipia taarifa hiyo muhimu la sivyo angechukuliwa hatua za kisheria.


  Kwa mujibu wa Sheria ya Makampuni kifungu 108, mtu anayeandikisha kampuni anatakiwa kuwasilisha taarifa za mizania kila mwaka (Annual Returns Report). Katika taarifa hiyo lazima uonyeshe wakurugenzi waliopo, mtaji wa kampuni na shughuli inayoshughulika nazo.


  Kampuni yake nyingine ni Navy Cut Tobacco Tanzania Ltd ambayo aliiandikisha Oktoba 12, 1995 kwa ajili ya kusafirisha nje Tumbaku na bidhaa nyingine inayohusiana na tumbaku. Lakini pia hakuwahi kufanya malipo yoyote ya taarifa ya mizania.


  Kampuni ya Liquidity Services Ltd inayomilikiwa na Thabit Katunda na Rajab Maranda iliandikishwa Desemba 17, 2004, Njake Hotel & Tours inayomilikiwa na familia ya Japhet Lema iliandikishwa Aprili 10, 2003 na ilianzishwa kwa mtaji wa milioni 200.


  Lakini Mei 13, 2005 ilibadilishwa jina na kuitwa Njake Tours & Safaris Ltd. Baadaye mtaji wake uliongezeka ghafla na kufikia Sh bilioni nane. Kampuni ya Excellent Services Ltd iliandikishwa 2004 na wakurugenzi wake walikuwa ni Emil Sabbas na Elisifa Ngowi.


  Kampuni hiyo ilianzishwa kwa mtaji wa Sh 500,000, lakini baadaye Sabbas alijiuzulu na kumuuzia hisa zake Massimo Fanneli Desemba 19, 2005. Ghafla mtaji wa kampuni hiyo uliongezeka hadi kufikia Sh milioni 50.


  Karnel Ltd ambayo shughuli zake ni usambazaji wa vifaa vya kuzimia moto ilianzishwa Agosti 4, 1998 kwa mtaji wa Sh milioni moja; lakini kufikia Desemba 15 mtaji wake uliongozeka hadi kufikia Sh bilioni 10. Wakati kampuni ya Uwakili ya Malegesi yenyewe imesajiliwa tangu mwaka 2001 na inaongozwa na Bedery Malegesi. Nayo inatajwa katika ufisadi huo wa BoT.
   
 8. m

  mabangi Member

  #8
  Feb 3, 2008
  Joined: Feb 1, 2008
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  iri ribubu ha sirierewi. kama uritaka kureta miapari si ingriireta tu. hujuigi kusema na maububu yako hayo si ujuwege hata kuandikaga. sasa rihapari rote hiro harafu hata rijina ra hiro riusarama ra taifa hurijuwi, harafu rimkapa riripopondaga mianikaji ya hapari ya tanzania mukariona rimkapa rijinga. nani nirijinga kwa miapari namuna hii. si hii mianikaji hapari ndio mijinga.
   
 9. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #9
  Feb 3, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Gembe kuwa mpole mzee hapa hadi kujua majina basi itakuwa baada ya kila kitu kufichwa .Mwanamtandao huwa hatajwi kwa uharaka ila ukiwa nje ndiyo utamsikia Meghji anasema alidanganywa .
   
 10. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #10
  Feb 3, 2008
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Lakini vyanzo vya habari vilithibitisha kuwa Ofisi ya Usalama wa Taifa anayeitwa ALI SIWA imeombwa kuhusishwa katika kuchunguza suala hilo kama ambavyo imekuwa inashiriki katika matukio mengine ya uhalifu. Kampuni ya Excellent Service Ltd ambayo imesajiliwa kama inashughulika na masuala ya upokeaji na usafirishaji wa mizigo, wakurugenzi wake wakati huo walimiki asilimia 100 kila mmoja akiwamo Ofisa Usalama huyo.
   
 11. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #11
  Feb 3, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Kulingana na habari hapo juu, jina linalotokea kwenye kampuni hizo zote mbili ni la Elisifa Ngowi, je huyu ni usalama wa taifa?
   
 12. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #12
  Feb 3, 2008
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  kichefuchefu kam cha uja uzito vile. ina maana hawa tunaowaamini kuwa wanalinda usalama wa taifa letu nao wanahusika kuiporomosha nchi?? sasa uzalendo upo wapi?? maana kama uzalendo utaisha ktk mioyo ya watanzania sisi basi hawa usalama ndiyo mioyo ya uzalendo yenyewe. wanakosa nini mpaka wachote hela zote hizo?? au ndo zile enzi za undugunaizesheni ktk kujiunga na kitengo hicho??

  naamini kuwa sio usalama wa taifa wote wameoza ila wapo walio wasafi na sijui wata deal vipi na ishu hii.

  Nauliza hiviii.... zaidi ya kuweka kura sandukuni, sisi wananchi tunanafasi ipi tena kidemokrasia (i dont believe in it) kuondoa utata huu??? maana kuwazomea hakutoshi, ni budi tuwavue cyupi na tuwatandike viboko hadharani.... (nina hasira sio siri)
   
 13. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #13
  Feb 3, 2008
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Ahsante Mtanzania, ila hawa Habari Leo ni wa ajabu sana. Hii habari hapa chini iliandikwa na habari leo Ijumaa iliyopita na The Citizen wakaandika Jumamosi iliyofuatia bila majina (Jumamosi ya wiki iliyopita) lakini cha ajabu ni kwamba habari ya The Citizen iliwekwa hapa JF na majina tukayaanika. Pia katika ile thread ya Ufisadi Usalama wa Taifa, kuna mtu aliweka data hapa na kuonyesha kwa data za JF hii habari ya Habari Leo si ya leo, ila naambiwa walisubiri kuomba kibali kwa JK na wamepata. Waliongea mpaka na RI. JF walitangulia zamaaani!!. Ajabu lEo watu wamesahau. JF NI KOBOKO.

  http://www.jamboforums.com/showthread.php?p=128217

  http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=9182&page=2

  http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=9252&page=2

  http://www.jamboforums.com/showthread.php?p=132715   
 14. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #14
  Feb 3, 2008
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Mtanzania, si tu kwamba ni Ofisa Usalama, naambiwa ndiye aliyechukua nafasi ya Siwa, katika Kurugenzi ya Usalama wa Ndani, awali alikua akifanya kazi chini ya Siwa, lakini alikua na nguvu kubwa kutokana na kuwa mtu wa DG aliyeondoka. Mkuu Mambo ni mazito kuliko yanavyoonekana.
   
 15. m

  mabangi Member

  #15
  Feb 3, 2008
  Joined: Feb 1, 2008
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  huierewi mijitu humu inchanganyaga mimbo siyo imesahaugi ni mijinga haina miakiri.inajinyaga mijanja kumbe inareta miapari ya kure kare. miapari ya zamani.
   
 16. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #16
  Feb 3, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mkuu Halisi,
  Nilipoona watu wanashangaa majina hayajatajwa nikashangaa maana mimi nimeyaona hapa mara nyingi kama ulivyosema hapo juu. Nikaamua kutumia search engine na ndio nikaipata hiyo habari tena toka kwenye threads za JF.

  Labda watu wanasoma haraka haraka na kusahau, Mimi sisomi threads zote ila nikiamua kujibu kitu basi inabidi nisome kila kitu toka mwanzo ili kutojichanganya.

  Asante kwa taarifa mkuu. Inaelekea mikono ya Apson na Mkapa imetapakaa kila sehemu. Hii ngoma ni nzito mno. Mpaka sasa nimeshindwa kupata sababu za JK kumteua Mwang'onda kuwa mbunge, je alikuwa analipa fadhila za babake? Au basi tu ni kwasababu alikuwa kijana wa Mtandao?

  Sijui kama tutajua ukweli wote kuhusu BOT maana inaelekea watu wengi mno walikuwa wanaogelea hapo.
   
 17. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #17
  Feb 3, 2008
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Ukisoma kwa makini habari hii pia utaona mambo yalikwisha kuandikwa.

   
 18. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #18
  Feb 3, 2008
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  kazi ipo
  na hili la sitta kumzuia makinda asijadili BOT na Richmond, si inaonesha dhahiri kuwa kuna jambo linachukuliwa kwa tahadhari sana hapo?? Na ikichukuliwa baadhi ya wahusika wametajwa dhahiri ila wale mbegu halisi hawajatajwa hadi sasa. Ninapata shaka kama hiyo ripoti kamili itatolewa kwa bunge kuijadili. Nahisi kuna tukio kubwa la kisiasa au hata kinchi litatokea na kutunyima haki ya kujua kinachoendelea na tuhuma za ufisadi BOT.

  Pia ikumbukwe uhuru wa vyombo vya habari Tanzania ni kwa nadharia tu.
   
 19. M

  Mafuchila JF-Expert Member

  #19
  Feb 3, 2008
  Joined: Apr 29, 2006
  Messages: 752
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Wabongo hatuwezi kulala. Ina maana hawa jamaa kwa nguvu na network waliyonayo, kama sheria ikichukua mkondo wake wana uwezo mkubwa wa kutuingiza kule ambapo jirani zetu wanajuta kuwepo.
   
 20. M

  Mafuchila JF-Expert Member

  #20
  Feb 3, 2008
  Joined: Apr 29, 2006
  Messages: 752
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Kwa kiasi fulani naanza kupata mwangaza jinsi Thom Apson alivyopata hizo tenda za Ikulu na Benki kuu Zanzibar.
   
Loading...