Ofisa usalama adaiwa kuingilia uchaguzi..... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ofisa usalama adaiwa kuingilia uchaguzi.....

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Rutashubanyuma, Dec 13, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 13, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,716
  Trophy Points: 280
  Ofisa usalama adaiwa kuingilia uchaguzi


  Na Patrick Mabula, Chato

  MADIWANI wateule wa Hamashauri ya Wilaya ya Chato wamemtuhumu Ofisa Usalama wa Taifa wa Wilayani hiyo, Bw. Cusbert Madondola kuwa ameingilia uchaguzi wa kumpata mwenyekiti unaotarajiwa kufanyika wiki hii.Baadhi madiwani
  hao wateule kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambao hawakupenda kutajwa majina wamedai kuwa ofisa huyo ameingilia waziwazi na kutaka wamchague diwani mmoja anayemtaka yeye, hali iliyozua mgawanyiko mkubwa katika halmashauri hiyo.

  Mbali na lawama hizo, pia wamedai kwamba ofisa huyo ambaye tayari amekanusha madai hayo, amekuwa akiwatishia kuwafungia shughuli zao binafsi baadhi ya madiwani kama hawatamchagua mgombea ambaye amekuwa akitaka apitishwe katika kikao chao ndani ya chama.

  Mkuu wa Wilaya ya Chato, Bi. Khadija Nyembo alikiri kuwepo kwa malalamiko hayo ya baadhi ya madiwani huku akishangaa ofisa huyo kutuhumiwa wakati mapendekezo ya nani amepitishwa na vikao vya uteuzi bado hayajatolewa.

  "Hata mimi nashangaa kwa kuwa masuala ya wanasiasa ni kuwaachia wenyewe na kama anajihusisha ni kinyume cha taratibu na nitamwita nimuulize hali hiyo, na hayo majina ya walioteuliwa najua hayajafika hapa wilayani kutoka vikao vya mkoa, yeye ameyatowa wapi," alihoji Bi.Nyembo.

  Bw. Madondola alipoulizwa kuhusu madai hayo alikana kujihusisha na uchaguzi huo na kuonesha mshangao kwa madai dhidi yake akisema wengi walioshinda katika uchaguzi ni wapya ambao yeye hajawahi kukaa nao.

  Alisema katika uchaguzi huo kumekuwepo na mipango ya baadhi ya watumishi wa halmashauri wakiongozwa na baadhi ya wakuu wa idara kumtaka diwani mmoja kama jina lake litarudishwa kwa upande wa CCM, watahakikisha anapita kwa maslahi yao, ndiyo maana kumekuwepo na propoganda za kumchafua na kumhusisha na siasa hizo.

  "Mimi sijihusishi na mchakato wa mwenyekiti wala sipigi kampeni kwa mgombea yeyote, kwanza wagombea wa nafasi ya mwenyekiti wa halmashauri wanaodaiwa kuwa majina yao yamerejeshwa kugombea nafasi hiyo sijayapata, japo nafahamu kuna walioomba, wako tisa.

  "Kuwa upande wa CCM na walioteuliwa kupigiwa kura na vikao vyao vya ndani sijaona aliyepewa barua ya uteuzi, na mimi siwezi kuingilia uchaguzi wao. W wanaoingilia ni watumishi wa halmashauri kwa maslahi yao," alisema Madondola.
   
 2. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #2
  Dec 13, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Kwani Kura si ni Siri au
   
 3. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #3
  Dec 13, 2010
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  kweli si usalama wa taifa, ni Usalama wa CCM
   
 4. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #4
  Dec 13, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Basi na wao wajiapishie mwenyekiti wao na ofisa usalama naye aapishewa kwake!
   
 5. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #5
  Dec 13, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Rekebisheni kiswahili kwa sasa nchi hii haina usalama wa taifa,bali ina idara ya usalama wa CCM!!!.Ni vizuri sana tuwaache kwa sasa na wao wachakachuliana!!!
   
Loading...