Ofisa ubalozini Nigeria afariki dunia

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,048
Mwenyezi Mungu awape faraja wafiwa katika kipindi hiki kigumu kwao na pia ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi~AMEN

Ofisa ubalozini Nigeria afariki dunia
Mwandishi wetu
Daily News; Thursday,July 03, 2008 @00:03

Ofisa Mambo ya Nje wa Tanzania, Gaspar Hakili (54), amefariki dunia, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, imetangaza. Taarifa iliyotolewa jana na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,

Balozi Charles Sanga ilisema Hakili alifariki dunia Jumatatu wiki hii mjini Abuja, Nigeria ambako kilikuwa kituo chake cha kazi akiwa kama Ofisa Mambo ya Nje Mkuu katika Ubalozi wa Tanzania.

Balozi Sanga alisema mwili wa marehemu utawasili nchini kesho kwa mazishi. Marehemu ameacha mjane na watoto watatu. Sanga alisema Hakili alizaliwa mkoani Tabora, Agosti 27, 1954 na aliajiriwa na Wizara hiyo kama Ofisa Mambo ya Nje mwaka 1977.

Alisema Hakili aliwahi kufanya kazi katika balozi za Tanzania katika nchi za nje zikiwamo Roma, Italia, Pretoria, Afrika Kusini na Abuja, Nigeria kama Ofisa Mambo ya Nje Mkuu Daraja la Kwanza kuanzia mwaka 2004 hadi mauti yalipomkuta.
 
Back
Top Bottom