Ofisa Habari mwandamizi wa Jeshi la Magereza, ASP. Lucas Mboje ateuliwa kuwa Mkuu wa Gereza la Wilaya ya Rombo

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
4,078
2,000
Ofisa Habari Mwandamizi wa Jeshi la Magereza, ASP. Lucas Mboje ameteuliwa na Kamishna Jenerali wa Magereza kuwa Mkuu wa Gereza Rombo Mkoani Kilimanjaro ambapo ameahidi kwenda kusimamia utekelezaji wa Agenda ya Mabadiliko ndani ya Jeshi hilo pamoja na suala zima la kujitegemea.
1592667406860.png

WASIFU WA ALIYETEULIWA KUWA MKUU WA GEREZA LA WILAYA YA ROMBO, ASP. LUCAS MBOJE

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP Suleiman Mzee hivi karibuni Juni 2020 alimteua Ofisa Habari Mwandamizi wa Jeshi la Magereza, ASP. Lucas Mboje kuwa Mkuu wa Gereza la Wilaya ya Rombo ambapo amechukua nafasi ya ASP. Ezekiel Lomba ambaye amestaafu utumishi wake kwa mujibu wa sheria.

Lucas Mboje ambaye kitaaluma ni Mwandishi wa Habari, alizaliwa wilaya ya Misungwi mkoa wa Mwanza mwaka 1980.

Kuhusu elimu yake, Lucas Mboje alisoma Shule ya Sekondari ya Musoma Mkoani Mara(1998) na Geita(2001) kabla ya kujiunga na Jeshi la Magereza mwaka 2002 ambapo baadaye aliendelea na elimu ya juu na kujiunga na Chuo Kikuu cha SAUT akisomea Stashahada ya juu ya Uandishi wa Habari na alihitimu mwaka 2007.

Pia Lucas Mboje ni mhitimu wa Chuo Kikuu Mzumbe - Shahada ya uzamili katika mambo ya Utawala(2013).

Mboje amewahi kuwa Afisa Mnadhimu wa Gereza la Kwitanga, lililopo Kigoma mwaka 2008, Mwandishi wa Taarifa katika Ofisi ya Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kigoma mwaka 2009.

Kuanzia mwaka 2009 alihamishiwa Makao Makuu ya Jeshi la Magereza ambapo alikuwa Mwandishi na Mhariri Habari wa Jarida la SAUTI YA MAGEREZA katika Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi hilo.

Kabla ya uteuzi huu hivi karibuni Kamanda Mboje amewahi kuwa Mhariri Mkuu wa Jarida la SAUTI YA MAGEREZA. Pia Ofisa Habari Mwandamizi wa Jeshi la Magereza ambapo atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa kama miongoni mwa maafisa habari wa Serikali ambao ni mahiri katika utoaji wa taarifa mbalimbali kwa umma hususani zihusuzo shughuli za Jeshi la Magereza pamoja na kuimarisha ushirikiano imara na wanahabari nchini.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom