OFFSIDE TRICK YA CUF HADI LEO SIJAIELEWA

masengobangu

Senior Member
Feb 25, 2014
127
131
Salaam WANAJAMVI
Kama tunavyojua mwaka 2015 ulifanyika uchaguzi mkuu TANZANIA BARA na VISIWANI.Kule visiwani uchaguzi ulifutwa kwa madai kwamba Maalim Seif alijitangaza,kuna kitu sijakielewa hadi leo "aliyejitangaza ni mgombea urais sasa kulikua na sababu gani ya msingi kuufuta uchaguzi wote"?.
OK,uchaguzi ukarudiwa na CUF wakacheza "OFF SIDE TRICK" ,sasa refa ameacha na CCM imeshinda na kwa mujibu wa huu mchezo refa akisema GOAL hakuna wakusema NOOO.sasa najiuliza ni faida gani ambayo CUF wameipata kwa kile walichokisusia hadi leo??
Nimesema haya baada ya jana kusikia MAUZAUZA mengine kwenye BARAZA LA WAWAKILISHI eti kuna muswada umepitishwa na Wawakilishi eti iwekwe sheria kali kwa yeyote atakaye jitangaza ,pili wale WAANGALIZI WA NJE hawatoruhusiwa kujiamulia maeneo yakwenda badala yake watapangiwa sehemu gani waende.
Hii kauli imenifanya niwaze mambo mengi sana.
1.Kwann Maalim asingeacha tu kujitangaza ,wangepindua matokeo ya URAIS then wabunge wa upinzani wangekua wengi bungeni nakuzuia miswada yote kandamizi na yeye angepata UMAKAMU,kuliko hali ilivyo sasa yaani wamepoteza MAMLAKA na SAUTI pia.
2.Kama alishakosea kujitangaza kwann asingerudi tu mara ya pili angepata walau viti kazaa vya ubunge na yeye kubakia kua MAKAMU wa RAIS?
Kwasababu hapa ninachokiona kama wamehamua kumshitakia mungu vile nahisi majibu yake yanaweza kuja baada ya miakaarobaini.
Naamini kama wangekubali 1 au 2 basi hata LIPUMBA leo asingetumiwa kuivuruga,sababu ya LIPUMBA kutumika huku inatokana na hofu iliyojengeka upande wa pili kwamba hawajui CUF wanawaza nn baada ya kuwafanyia ukatili ule wa kutisha.
MSAADA
anayejua faida za kisiasa walizozipata,wanazozipata au watakazopata kisiasa watujuze.
 
Back
Top Bottom