Tume ya Uchaguzi znz (ZEC) imetangaza kuwa itatangaza mshindi wa Urais Zanzibar sasa hivi (8:30pm) usiku huu. Hadi hivi sasa, SHEIN wa CCM anaongoza kwa 61% ya kura. Yamebaki matokeo ya majimbo 6 tu. Matatu yakiwa Pemba na matatu yakiwa Unguja.
Wadadisi wa siasa wanasema Seif Sharif Hamad wa CUF atashinda majimbo yote 3 yaliyobaki Pemba na Shein atashinda majimbo 3 yaliyobaki Unguja.
Huenda SHEIN akatajwa kuwa Rais kwani idadi ya wapiga kura wa Pemba ni kidogo kuliko wale wa Unguja.
Inasemekana kuwa Seif yuko tayari kukubali matokeo akishindwa na SHEIN, lakini wafuasi wa CUF wamesema hawatakubali kushindwa na wataingia mitaani kudai haki.
Kazi ipo visiwani usiku huu...