OFA Kubwa kwa wapenzi wa vitabu vya ALFU LELA U LELA.

MNBooks

New Member
Joined
Jan 30, 2016
Messages
2
Likes
1
Points
5

MNBooks

New Member
Joined Jan 30, 2016
2 1 5
OFA KUBWA kutoka Mkuki na Nyota! Pata vitabu vyote 9 kwa bei ya vitabu 7 na ukamilishe seti nzima ya ALFU LELA U LELA.
Vitabu hivi vinasisimua sana na kama hujawahi kuvisoma basi ukianza kitabu cha kwanza hautaweza kukiweka chini na utataka umalize vyote na mpaka sasa mfululizo umefikia vitabu 9. Changamkia ofa hii adimu uokoe pesa nyingi.

Promosheni hii ni kwa duka la @TPHBookshop au @Mkukinanyota Publishers na ni kwa muda mfupi tu. Kitabu kimoja kinauzwa shilingi 11,000 Tu na kila kimoja kimesheheni hadithi lukuki.

Wasiliana na TPH Bookshop: 0687238126 / 0759390082 / daressalaam [at] tphbookshop .com

MASIMULIZI KAMILIFU YA ALFU LELA U LELA AU SIKU ELFU MOJA NA MOJA: KITABU CHA NNE

Mfasiri: Hassan Adam


Huu ni mfululizo wa hadithi maarufu duniani kote za Alfu Lela U Lela (au Siku Elfu Moja na Moja) zenye asili ya Arabuni na Uajemi. Masimulizi haya ya Alfu Lela U Lela yametafsiriwa kutoka matoleo ya Kiingereza na Kijerumani. Lugha hizi za Ulaya ndimo zilimotafsiriwa hadithi hizi kwa mara ya kwanza kutoka lugha za Kiajemi, Kiarabu na Kihindi. Tafsiri ya kwanza ya Kiswahili ilifanywa mwaka wa 1928 na katika kufanya hivyo sehemu nyingi zilikatwa au ziliachwa makusudi bila kuzitafsiri kwa sababu wamisionari kawakutaka wasomi wa Kiswahili wasome baadhi ya sehemu kwa sababu zao wenyewe (kwa mfano mapenzi, uchawi, majini n.k) . Matoleo haya, kwa kifupi, ndiyo yenye hadithi kamilifu kwa uhakika; yaani mtiririko wa visa na maana halisi ya hadithi kama zilivyotungwa na kutafsiriwa na magwiji wa lugha hizo mbili zaidi ya miaka mia moja iliyopita. Kiswahili kina bahati ya kumpata mfasiri, Hassan Adam, Mtanzania mwenye ujuzi wa lugha zote tatu zilizohusika katika kutayarisha tafsiri hizi. Bwana Hassan Adam ni mkufunzi wa miaka mingi katika Taasisi ya Lugha za Kiafrika katika Chuo Kikuu cha Cologne, Ujerumani.
 

Attachments:

Forum statistics

Threads 1,191,008
Members 451,429
Posts 27,692,194