Odometer imefutika

RRONDO

JF-Expert Member
Jan 3, 2010
51,719
107,771
Wakuu gari yangu GX100 Cresta imefutika mileage kwenye odometer. Leo ndio nimeshtukia mpaka sasa hivi ina 256,000km. Kuna mwenye uzoefu na tatizo hili?
IMG_20190602_134635.jpg

Mrejesho:Nimewasha gari Leo asubuhi,readings zimerudi kama kawaida
IMG_20190603_063602.jpg
 
Kuna uwezekano mkubwa zile gears zinazofanya odometer isogee zimevunjika.

Kuzipata hizo gears itabidi uitoe hiyo instrumental cluster na nyuma yake zipo hizo gears uangalie ilovunjika.

Unahitaji mechanic makini ili asiharibu kila kitu.

Fundi akiitoa hiyo cluster aisafishe kwa upepo au compressd air na aifutefte kwa kitambaa laini.

Hapo pia waweza kubadilisha taa za hiyo cluster na pia kubadilisha nyaya chakavu kwa kuweka nyaya mpya.

Baada ya matengenezo hayo madogo Odometer yako itakuwa na uhai angalau wa kukusogeza kwa muda zaidi wa gari yako.
 
Kulingana na picha hapo juu, inaonekana power hamna kwenye display unit, inawezekana kuna fault mahali fulani kwenye circuit.
 
Fungua hapo kwenye dash...hako kadisplay huwa kana vimiguu flani hivi vinavyochomekwa kwenye sakiti...huenda vimelegea...chomoa na uchomeke tena...
Ha ha ha haya madude yana vituko vingi, vingine na uzoefu wote ni vipya. Hili la kufuta km tu sijawahi kukutana nalo
 
Iyo gari ilinishindaga 2012 ndio ilikuwa gari yangu kwanza. Nikaisukuma na kuhamia kwenye Allex. Gari inakunywa mafuta Kama ugomvi?
Hii ninayo tangu 2014 na siiuzi kamwe. Kuendesha hii lazima uwe mwanaume. Kwa mwezi wese si chini ya 400,000. Ila sasa hivi naitumia kama back up
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom