Odinga awataka wafuasi kususia bidhaa za kampuni tatu Kenya

mtarimbo

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
1,529
3,919
Muungano wa upinzani nchini Kenya National Super Alliance (Nasa) umetoa wito kwa wafuasi wake kususia bidhaa na huduma kutoka kwa kampuni tatu ambazo unadai zimekuwa zikimpendelea Rais Uhuru Kenyatta.

Bw Kenyatta alitangazwa Jumatatu kuwa mshindi wa uchaguzi wa marudio uliofanyika 26 Oktoba, ambao kiongozi wa Nasa Raila Odinga alisusia akisema haungekuwa huru na wa haki.

Bw Odinga alitangaza kabla ya uchaguzi huo kwamba muungano huo utabadilika na kuwa Kundi la Pingamizi dhidi ya Serikali na baadhi ya hatua ambazo ulisema utachukua ni kususia bidhaa na huduma kutoka kwa kampuni ambazo alidai zinamfaa Bw Kenyatta.

Kampuni ambazo Nasa wamesema wafuasi wao wanafaa kususia ni:

•Kampuni ya mawasiliano ya Safaricom, ambayo ndiyo tajiri zaidi miongoni mwa kampuni za Kenya

•Kampuni ya maziwa ya Brookside, inayomilikiwa na familia ya Kenyatta

•Kampuni ya kutengeneza mafuta ya kupikia na sabuni ya Bidco


HUU NDIO UPINZANI WA KIAFRIKA
 
hio list ilikua ndefu naona wanaitoa kwa mafungu...binafsi namkumbali Raila huyu mzee ni fighter sana ila ssa na wasi wasi na washauri wake kwa kweli...
sio kila mfuasi wa Nasa anakipato cha uhakika wengi ni wababaishaji na unavyo waambia hakuna kutumia bidhaa hii ambayo pengine bei iko chee kuliko zingine naona ni shinda..Bidco wamewekeza Kenya magaribi kilimo cha alizieti,wamewajili pia wafuasi wa Nasa, Safaricom hivyo hivyo n.k je ukiacha maelekezo ya kutonunua bidhaa zao kuna wale wafanyakazi watasimamishwa na wana majukumu ya familia zao hili Nasa wanaliona aje au ndio no gain without pain.
hii picha inaanza upya...
 
Back
Top Bottom