Elections 2015 Octoba 2015:Tanzania Has a Choice Kati ya Kuendelea na Umasikini, au Kuchagua Utajiri!. Jee... ?!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,442
113,451
Wanabodi,

Jumapili ya leo, nimepata tena fursa ya kuendelea kuhamasisha, watu wajitokeze kwa wingi kupiga kura kwa muktadha wa kuchagua kuendelea kuwa masikini, au kuchagua utajiri!.

Wakati tukiikaribia October 25, JF kama social media, ina wajibu wa kufanya trend setting, kuwaelimisha Watanzania the available options ya ukikichagua chama fulani, umechagua nini ili tarehe 25 October, Watanzania wafanye informed decision and live with their choice kwa miaka 5 mingine.

Mada hii ni muendelezo wa mada yangu
[h=3]Wito Kwa Watanzania:Tuitumie Nguvu ya Kauli, Kumuingiza Ikulu Kiongozi Tunayemtaka!. Mdomo huumba!. Tuumbe Ushindi kwa Kauli Zetu!.
[/h]Naomba kukiri, nimekuwa inspired na mchango wa mwana jf huyu
Propaganda at its best!

Kama mdomo huumba basi watu wangekuwa wanasema mimi sitaki nife milele na wangeweza kuishi milele.

Kinachoumba ni Tafiti/uchunguzi.

Bila logic, thinking, and reasoning huwezi kuumba lolote.

Tafiti/chunguzi zilizofanywa zimeonyesha Lowassa hawezi kuwa Rais wa Tanzania hata kama utahamasisha watu wengi wakapige kura.
Mkuu,MsemajiUkweli, hii sio propaganda bali ni reality, yaani ndio ukweli wenyewe!.

Jee hujawahi kusikia ule msemo wa "lisemwalo lipo kama halipo linakuja"
unamaanisha kuna jambo ukilisema, unakuwa umeliumba, then linatokea kweli!.

Au hujawahi kulisikia neno hili "sema neno moja tuu na roho zetu zitaponywa!".

Au unaijua nguvu ya sala inatokana na nini?, au nguvu ya maombi inatokana na nini?!, nguvu za sala zinatokana na kauli, ndio maana hadi kuna baadhi ya madhehebu, wanasali kwa kupaaza sana sauti na hadi kulia, wakiamini kadri unavyotoa kauli kubwa, ndipoi kauli hiyo inavyokuwa na nguvu kubwa!.

Ndio maana hata katika mazungumzo na msisitizo, ukisema kwa ukali, unatoa sauti kubwa, na utekelezaji unakuwa ni mkubwa!, ila katika nguvu ya sala, hata ukisali kimoyo moyo tuu, inatosha cha msingi ni kauli!.

Mungu ndio aliyetuumba hivyo anaona shida zetu zote na mahitaji yetu bila hata kuyataja, hata ukisali kimoyo moyo ukiwa kimya kabisa, au kufikiria tuu, Mungu tayari anasikia, but ,why watu wanasali kwa sauti?!, ni kwa sababu kauli huumba!.

Nimefanya utafiti nikagundua, hata ukiombwa pesa na mwenye shida, ukajifanya huna pesa kwa kauli za "sina kitu kabisa!", then unajiumbia kuchacha na ni kweli unakuja kuishiwa kabisa!. Lakini ukiombwa pesa huku ukiwa huna kitu kabisa, ukisema nikipata nitakusaidia, amini usiamini, utapata pesa na utamsaidia huyo mwenye shinda!.

CCM kwa miaka 54, imekuwa ukituaminisha kuwa, licha ya rasilimali zetu lukuki, lakini Tanzania ni nchi masikini, na sisi watu wake, yaani Watanzania ni watu masikini!. Kutokana na kauli hizi, sisi bila kujijua, kumbe ndio tumejiumbia umasikini!, na kweli, Tanzania imekuwa ni nchi masikini, na Watanzania tumekuwa ni watu masikini kiasi kwamba hali hii ya umasikini uliotopea, umepelekea hadi rais wetu mpendwa, Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, kulazimika kusafiri kwenda nje ya nchi na kuzunguka huku na kule kutembeza bakuli, hadi watu humu jf kumbandika jina la utani la Vasco, kwa kumfananisha na Vasco Da Gama!, tena anakwenda kuomba huku akiwa very confortable na proud kuwa omba omba!, na kujisikia fahari kuomba na kulifanya taifa letu ni taifa la omba omba!.

Tangu tumepata uhuru, uchaguzi huu ni wapili ambao Watanzania we have a choice to choose from!. Uchaguzi wa kwanza ambao Watanzania we had a choice ni ule wa 1995 wakati wa Mrema, ila tushukuru Mungu, kuna kitu ilikiona kwa Mrema, akatuepushia na balaa la kumchangua maana Mrema angeshinda, it would have been a disaster!, Hitler ana afadhali!.

Mwaka 2000, 2005 we had no choice, ilikuwa ni walkover tuu kwa CCM!. Uchaguzi wa mwaka 2010 tulitaka kuwa na choice aliposimama Dr. Wibroad Silaha, lakini kwa bahati mbaya Dr. Slaa sio presidential material!, hajawa na personality ya urais, huyu ni mtendaji zaidi, na mwana harakati, hivyo nafasi stahiki kwake ni Uwaziri Mkuu tuu!. Nashukuru hili UKAWA waliliona hivyo walikuwa na kibarua cha kumtafuta mgombea anaukubalika, anaye uzika, na anaye chagulika, hivyo kama zali tuu, Mungu akawashushia Lowassa!.

Hivyo uchaguzi wa mwaka huu, we have a choice, kati ya kuchagua umasikini au utajiri!.
Kufuatia CCM kuhubiri umasikini, kuichagua tena CCM ni kuuchagua umasikini!, hivi kweli kuna mtu mwenye akili zake timamu, anayejua umasikini wa taifa letu ni umasikini wa kujitakia tuu na umesababishwa na CCM, lakini bado akaichagua tena CCM?.

Lowassa amesema wazi, Tanzania sio nchi masikini, Tanzania ni nchi tajiri, yeye sio masikini, ni tajiri kwa sababu ametoa kauli ya kuuchukia umasikini. Amesema nchi hii ina rasilimali za kutosha kuwezesha kutoa elimu bure kuanzia chekechea hadi chuo kikuu, ukimchagua Lowassa, unakuwa umeamua kuachana na umasikini ambao CCM imeuumba kwa kauli zake, na badala yake sasa tunafanya mabadiliko ya kuuchagua utajiri, kwa kauli, kuwa ukimchagua Lowassa, umeuchagua utajiri!.

Naomba niwape ushuhuda wangu mdogo tuu, mimi ni mwandishi wa habari, na fani ya uandishi wa habari, imekuwa ikichukuliwa kuwa ni fani ya kimasikini, hivyo waandishi wa habari ni watu masikini, na mimi nikiwa ni mmoja wao, kwa wanaonijua enzi za ule usafiri wangu wa piki piki nikikaa nyumba ya kupanga Ilala Shariff Shamba!.

Siwezi kujitapa kuwa sasa mimi ni tajiri, no!, bali baada ya kufukuzwa kazi TBC ile 2002, sikuajiriwa tena, bali nimekuwa ni mwandishi wa kujitegemea ambapo sijaajiriwa na mtu yoyote, hivi sasa ninaishi Mbezi Beach kwenye kakibanda fulani!, alhamdidulahi!, nikiwa ni Mkristo Mkatoliki ninayekubali mazuri yote ya Ukristo, lakini sijapuuzia au kuatekeza mazuri ya mila zetu za Kanda ya Ziwa, hivyo nina wake 3!, watoto 8!, kati ya hao wawili wa kubwa wa mama wa kwanza, wako vyuo vikuu vya kulipia!, na wote, wana magari yao!. Watatu wa mama wa kati, wako sekondari na wawili wa mwisho wa mama mdogo, wako primary na wanasoma shule za Academy. Kila mke, ana mji wake, usafiri wake na biashara yake, hivyo siwezi kujiita masikini wala fani ya uandishi wa habari sio fani ya kimasikini!.

Hivyo umasikini is just an atitude of mind!, ukiukataa umasikini kwa kauli, amini usiamini, unasikini unakuaga!. Hivyo sisi Watanzania, katika umoja wetu, tukiamua kwa kauli moja, kuukataa umasiki kwa kuikataa CCM, na kukumbatia utajiri kwa kuichagua Chadema, amini nakumbia rais Lowasa kamwe hatafanya safari yoyote nje ya mchi kwenda kutembeza bakuli kama alivyofanya Kikwete!. Lowassa akisafiri nje ni safari za kidiplomasia na kuhudhuria tuu mikutano ya kimastaifa kama kulihutubia Baraza Kuu la UN!.

Namalizia kwa kushauri hata wewe hapo ulipo, kama umechukizwa na umasikini, tarehe 25 nenda kapige kura kwa kusema No CCM No Umasikini!, na hata kama wewe ni mwanachama wa CCM, lakini unachukizwa na umasikini na ulipanga kumchagua Magufuli, usibadilishe chochote katika msimamo wako huo, endelea kuvaa t-shirt yako ya kijani na kofia, endelea kuhudhuria mikutano ya kampeni ya CCM, ila tarehe 25 October, weka tiki yako kwenye kisanduku cha 4 chenye picha na jina la Edward Ngoyai Lowassa, kwa pamoja na kwa kauli moja, tupaze sauti zetu kusema No to umasikini!.

Kuelekea Octoba 2015:Tanzania Has a Choice Kati ya Kuendelea Kuchagua Umasikini, au Kufanya Mabadiliko na Kuchagua Utajiri!. The choice is Yours,

Tarehe 25, Sema Neno Moja Tuu na Taifa Letu Litaponywa!.


Nawatakia Jumapili Njema.

Pasco
Ukiguswa, unaweza kufuatilia nyuzi zangu nyingine hizi


  1. [h=3]Wito Kwa Watanzania:Tuitumie Nguvu ya Kauli, Kumuingiza Ikulu Kiongozi Tunayemtaka!. Mdomo huumba!. Tuumbe Ushindi kwa Kauli Zetu!.
    [/h]
  2. [h=3]Hivi Kweli Kuna Mtanzania, Mwenye Akili Zake Timam Anaweza Kuichagua Tena CCM ?!.
    [/h]
  3. Kufanya Kosa Sii Kosa, Kosa Kurudia Kosa!. Mwaka 2010 Tulifanya Kosa!, Mwaka 2015, Tusirudie Kosa!.
  4. Kuichagua tena CCM, Je ni kielelezo cha kufanya informed Decision au Kuendeleza Ignorance!.
  5. Hii 'Vox Populi' ni 'Vox Dei' Kuhusu 'Jiwe Walilolikataa Waashi ...
  6. Kuelekea 2015: CHADEMA, Don't Miss the Target!,

  7. Watanzania ni ignorants au tumelogwa?!.

  8. Edward Lowassa sio lazima yeye tu ndiye awe Rais wetu 2015!
  9. Kuelekea 2015: Chadema Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!.

  10. Yametimia!, CCM Imechokwa!, CHADEMA Ikulu Njia Nyeupe 2015!-





 
Hivi kuna siku umewahi kuanzisha mada ya kuhusu ilani na ulinganisho wa ilani hizo au unaposema "informed decision" making huwa unamaaisha "influenced decision making". . . . . . .!!!!!

Are you informed au uko influenced mkuu Pasco? ??!!!
 
Last edited by a moderator:
Hivi kuna siku umewahi kuanzisha mada ya kuhusu ilani na ulinganisho wa ilani hizo au unaposema "informed decision" making huwa unamaaisha "influenced decision making". . . . . . .!!!!!
Are you informed au uko influenced mkuu Pasco? ??!!!
Mkuu OLESA,
Mkuu Olesa, tangu kampeni zimeanza sijawahi kuhudhuria kampeni, wala kusoma ila ya chama chochote kwa sababu mimi niko kwenye kundi la kuchagua mtu, sio chama wala sio ilani!.

Nyinyi watu wa ilani, ndio pandisheni mada za kuhusu ilani na ulinganisho wa ilani hizo ili watu pia wafanye "informed decision" based on ilani!.

Mimi natoa ushauri based on performance, Tanzania tulipopata uhuru ile miaka ya 60, tumepata uhuru na nani, tulikuwa na rasilimali gani, tulipaswa kufanya nini!, leo miaka 54, tunaangalia wale tuliopata nao uhuru wako wapi, walikuwa na rasilimali gani, walifanya nini na sasa wako wapi, utakubaliana kabisa na mimi, kuwa hakuna Mtanzania mwenye akili zake timamu, atayajua haya, halafu bado akaichagua tena CCM!.

Umasikini wa Tanzania ni umasikini wa kujitakia ambao umesababishwa na CCM!, watu wana option ya kuchagua kuendelea na umasikini huu au kuchagua utajiri!.

Pasco
 
Hawa watu wa Ukawa wana matatizo sana, ni jana tena nikakutana nao ..mara likaja tangazo la Magufuri na ghafra jamaa mmoja akabwatuka.. Oooh, huyu jamaa kwanza wao ndo wameua viwanda wakati akiwa waziri wa nyumba na viwanda ..ikabidi ninyamaze kimya, baada ya kuona watu wote wamekaa kimya ikabidi ajivute taratibu huyo akasepa, tukaanza kujiuliza hivi hawa watu wa Ukawa wamevurugwa kiasi hiki? hivi ni lini Magufuri alikuwa waziri wa viwanda? sasa mtu wa hivi asiyeelewa hata Magufuri alifanya wapi kazi huyu anapoanza kuongea utumbo wa hivi maana yake nini? anyway, tukagundua mashabiki wengi sana wa Ukawa pamoja na kujifanya wajuaji ila ni mbumbumbu sana na ndo maana inakuwa rahisi kutumiwa na kudanganywa na wahuni wachache
 
Tanzania Has a Choice Kati ya Kuendelea Kuchagua Umasikini, au Kufanya Mabadiliko na Kuchagua Utajiri!. The choice is Yours.

P.
 
Pasco na wewe chagua kati ya kuandika point au hizi pumba zako...

Its too late... Matumbo na tamaa zimewaponza chadema... You are nothing but a dying child whom we expected wud be our hero....

Its over... Chadema itashindwa kirahisi, atakayefanya vurugu atakiona cha mkunyukunyu...

ACT mjipange kwa sababu tunategemea muwe chama kikuu cha upinzani miaka 5 ijayo
 
Wanabodi,

Lowassa amesema wazi, Tanzania sio nchi masikini, Tanzania ni nchi tajiri, yeye sio masikini, ni tajiri kwa sababu ametoa kauli ya kuuchukia umasikini. Amesema nchi hii ina rasilimali za kutosha kuwezesha kutoa elimu bure kuanzia chekechea hadi chuo kikuu, ukimchagua Lowassa, unakuwa umeamua kuachana na umasikini ambao CCM imeuumba kwa kauli zake, na badala yake sasa tunafanya mabadiliko ya kuuchagua utajiri, kwa kauli, kuwa ukimchagua Lowassa, umeuchagua utajiri!.

Naendelea na My Tribute to this fallen hero, Mwamba wa Kaskazini, kwa kujikumbusha baadhi ya mabandiko yangu kumhusu shujaa huyu mpaka siku atakapo pumzishwa kwenye makao yake ya milele, let's celebrate the life and the times of Edward Lowassa.

RIP Shujaa Laigwanani Comred Edward Ngoyai Ole Lowassa,
Umepigana vita vilivyo vitakatifu, imani umeilinda.
Bwana alileta
Bwana ametwaa,
Jina Lake Lihimidiwe!.

Paskali
 
Back
Top Bottom