OCT 25: Kichwani namchora MKOMBOZI, mkono unatakaa kumalizia picha

ONTARIO

JF-Expert Member
Oct 16, 2013
1,885
17,018
Hi JF,

Kwanza kbs niseme mimi si shabiki wa siasa, but time and time again I risk my time discussing issues, siasa kwa nadra sana. Leo ni siasa.

1930 ujerumani ilipoteza mvuto wake kabisa, ilikua nchi dhaifu sana, uchumi ulikua umechuchumaa haswa, maisha yalikua magumu sana. Viwanda vilifungwa, bandari zilifungwa, hkn bidhaa sokoni, .Wajerumani waliteseka sana, walisaga meno, walilia, walikata tamaa.

Great economic depression iliwagonga utosini, afya ilikua mbovu, elimu mbovu, hakuna ajira, deutschmark (pesa ya mjerumani) ilishuka thamani, kilimo kilidorora, biashara hola, wawekezaji wakakimbia nk nk. Hiki kipindi wachumi huita hyperinflation.

Kipindi hicho Ujerumani ilikua inasikilizia maumivu ya versailles treaty, haya makubaliano yaliikandamiza sana ujerumani. pia miaka kama 15 iliyopita ujerumani ilikua imechapika ovyo WW1. Waliwekewa vikwazo vingi sana, hii ilitabinya vilivyo kimaendeleo.

Serikali ilikua imepigika mno, kila kitu kilikua hakitembei, mpaka wakatungwa jina "weimer republic" yani "kitu kilichooza". Wajerumani waliichoka serikali yao hakika.

Wajerumani wote nchini walikua wanahitaji mabadiliko, walikua wanataka ukombozi tena wa haraka sana. Walikua wanahitaji viongozi wapya wenye kuweza kuwakomboa. Viongozi wa kuwavusha, kuwapitisha ktk kipindi cha njaa na umaskini.

From no where aliibuka mtu aliyetokea kupendwa sana tena sana, alihubiri upendo+amani, kuanzia misikitini hadi makanisani, alihubiri ukombozi, alihubiri uchumi imara, alihubiri ajira, elimu, kilimo, afya, viwanda, biashara, mpaka chakula.

Alipata umaarufu mkubwa sana, yeye na chama chake. Wajerumani walihitaji mtu wa aina hii, mtu ambae angeweza kuwavusha ktk kipindi hicho kigumu. Mtu ambaye angewarudisha mchezoni.

Huyu ndiye Chancellor Aldolf Hitler ninayemfahamu.Hiki ndicho chama cha wanazi haswa ninachokifahamu.Uchaguzi uliofuata mapinduzi makubwa yalitokea, Nazi party kilipata viti karibia 230 ulilinganisha na viti 26 walivyokua navyo awali Reichstag (bunge la Ujerumani).

Lakini bahati mbaya kura hazikutosha kumruhusu Hitler kuwang'oa Hindenburg na Von Papen madarakani.Wananchi walichukia + kuumia sana kuona hitler hajaingia ikulu, Hitler akawamobilize wajerumani waishinikize serikali imteuwe awe Chancellor, lakini serikali ikakataa, ilitaka imteuwe awe vice chancellor, Hitler hakutaka uvice.

Shinikizo likazidi kuwa kubwa mwishoe 1933 Hindenburg akaamua ampe cheo cha uChancellor hitler.Watu wakapata matumaini, furaha.. wakajua mkombozi kawafikia. Wakajua ujerumani yao inarudi kuwa kama awali.

Heheheee kama vile chizi kapewa rungu, Hitler alibadilika, akawa mbogo, akawa kama kinyamkera. Kupitia Nazi akaunda Machtergreifung (ukomo wa madaraka) akaipindua serikali, huo ukawa mwisho wa Weimer republic, akawa supreme leader. Nazi kikabaki kua chama pekee ujerumani.

Alichowalipa wajerumani kila mtu anajua +aliuwa watu 17mil).Alichowafanya wayahudi-wajerumani kila mtu anajua (aliwachinja 6mil).Dunia nzima haiwezi kulisahau jina la Hitler.Alichoizawadia dunia wala sihitaji kuelezea, uroho wake wa kuitawala ulaya ulituletea WW 2.

Kipindi hiki ambacho mimi mtanzania nahitaji ukombozi, nahitaji mabadiliko, nahitaji ajira, uchumi imara, viwanda, elimu bora nk, namkumbuka Hitler.
Akili yangu inamchora mkombozi, lkn mkono unakataa kuimalizia hiyo picha.

#TanzaniaNakupenda
 
Kama itakua imegusa upande fulani naomba mnisamehe.
Lkn ni vizuri kukumbushana watu na tabia zao, kupitia mgongo wa ukombozi.
Mmhh sijui mkuu ulioteshwa yatayo tukia???? Any way Mungu ibariki Tanzania Mungu ibariki Afrika
 
  • Thanks
Reactions: BAK
mkuu Fanya urudi
hapa ilitisha sana..
nimeshangazwa kwàkuona kuwa Uzi huu una comment chache mnoooo
wakati niuzi ambao unaubongo wenye maono ya yoseph...
nimeanza kuamini Yale maneno ya watu wenye imani ya Buddha...wanaposema kuwa MTU akifa huwa anazaliwa tena ktk TAIFA lingine..
nahisi baada ya Hitler kusadikika kuwa amekufa alizaliwa upya TZ..lkini akiwa kwenye taswira na wajihi tofauti....hahahaa
 
MUNGU WANGU HATA SIAMINI MKUU ULIYAONA HAYA YOTE MUNGU TUSAIDIE WATANZANIA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom