OCEAN ROAD HoSPITALI

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,592
29,711
Nilimsindikiza shemeji yangu kwenda kumsalimia ndugu yake aliyelazwa pale.
Nilipokuwa eneo la hospitali nikapata tashwishwi ya haja ndogo ambapo nikaelekezwa vyoo vya wodini. wodi ya kwanza mpaka ya tatu nilizoenda nilikatishwa tamaa na kuitoa hiyo haja maana vyoo vimejaa kinyesi na uchafu mwingine. halafu vyoo hivyo vipo wodini. Maji hamna vyooni seuse ndoo za maji.

Nimejiuliza sana kuwa iweje hospitali ambayo ipo kwenye viwanja vya ikulu ikose maji na huduma ya usafi ya uhakika??? Kwa mtazamo wangu ni kuwa wagonjwa wengi waliolazwa pale wanaambukizwa maradhi mapya kutokana na hali hii.

KODI ZETU ZINATUMIKAJE???
 
Ni upuuzi na uzembe wa utawala (administration) ya hiyo Hospital. Mpe mzungu aiendeshe, kwa bajeti hiyo hiyo iliyopangiwa uone mabadiliko. Sisi bado.
 
Back
Top Bottom