OCD, RPC na trafiki wote wataje mali zao kwa kiapo na jinsi walivyozipata

shikulaushinye

JF-Expert Member
Aug 29, 2014
828
456
Napendekeza askari wa jeshi la Polisi hasa wale wakubwa na wa usalama barabarani wataje mali zao kwa kiapo ili kudhibiti suala la rushwa katika jeshi la POLISI. Maana kuna baadhi ya makamanda ni kama miungu watu.

Askari wa usalama barabarani wana utajiri wa kutisha usiolingana na pato lao huku askari wengine hali zao zikiwa mbaya sana.
 
Napendekeza askali wa jeshi la Polisi hasa wale wakubwa na wa usalama barabarani wataje mali zao kwa kiapo ili kudhibiti swala la rushwa katika jeshi la POLISI. Maana kuna baadhi ya makamanda ni km miungu watu. Askari wa usalama barabarani wana utajiri wa kutisha usiolingana na pato lao huku askari wengine hali zao zikiwa mbaya sana.
Naunga mkono hoja 100%
 
Kiapo kinaongeza mori wa kupiga dili, hakina maana yeyote kwa nchi km Tanzania itafutwe njia nyingine
 
Wote wanajaza hayo maform na kula kiapo mwisho wa siku ubadhirifu unaanzia nyumba nyeupe:confused::confused:
 
Wataje malizao? Unataka kuwaua nyie? Hapo pabaya

No wataje tu, then usalama wafanye kazi yao. nakwambia wengine wataachia kazi wenywe na kukimbia. kuna jamaa mmoja ni wa gwanda nyeupe ana miliki hiace 4, coaster 5, magari madogo 3, fuso 3. achilia mbali majumba.
 
Back
Top Bottom