OCD na DC Mtatiro wa Tunduru wasema Tunduru kuna ugaidi

Abdul Nondo

JF-Expert Member
Oct 28, 2016
515
2,873
Wilaya ya Tunduru ni miongoni mwa wilaya sita (6) za Mkoa wa Ruvuma. Wilaya ya Tunduru ina majimbo mawili Tunduru Kusini na Tunduru Kaskazini.

Jana tar 3 Oktoba 2022 Mkuu wa Wilaya @julius_mtatiro na OCD wa TUNDURU. Wamethibitisha rasmi ya kwamba Tunduru kuna UGAIDI kupitia Barua hii waliyoiandika kuzuia ziara ya katibu Mkuu wa @actwazalendo_official @adoshaibuado . Kwamba Magaidi watamdhuru .

Hii ina maana ya kwamba Mh.@julius_mtatiro na OCD wa TUNDURU wametoa tahadhari kwa watalii wanaotaka kwenda Mbuga ya Selou kutalii kwamba Sasa hivi hali sio shwari , naona kuna haja sasa mamlaka Police @polisi.tanzania @policetanzania , IGP na Mheshimiwa Rais @samia_suluhu_hassan kuona namna Sasa ya kutoa amri ya watu wa TUNDURU na Ruvuma kwa ujumla kutotoka nje (Curfew) ili wananchi wasihatarishe maisha yao kwa uwepo wa Magaidi.

Tunduru ina vivutio vingi sana kama mbuga ya wanyama selous, mapori ya akiba ya sasawala na muhuwesi, masalia ya majengo ya wapigania uhuru wa msumbiji kupitia chama cha Frelimo, makaburi ya viongozi wa kimila, Miti inayogeuka kuwa mawe, mapango ya ajabu na nyayo za wanyama katika mwamba vyote hivi ni sehemu ya utalii na vinapatikana katika wilaya ya Tunduru pekee. Ila kwa taarifa hii ya DC na OCD maana yake Watalii hawapaswi kwenda sio sehemu salama kwao tena

Tunduru huko Ruvuma kimkoa kuna vivutio vingine vingi pia kama mapori ya akiba ya Selous,Mwambesi,ziwa Nyasa lenye samaki wa mapambo,visiwa,fukwe za kuvutia na vuvutio vingine lukuki, mto Ruvuma wenye maporomoko ya Nakatuta,Tulila na Sunda.

Pia kuna utalii wa kiutamaduni kama majengo ya kihistoria yakiwemo makanisa makongwe ya Peramiho,Lituhi na Lundu, makumbusho ya vita ya Majimaji,historia ya machifu wa kiyao,wangoni na historia ya biashara ya utumwa.Jiwe la Mbuji,mapango ya wamatengo na pango la mlima Chandamali ambalo lilikuwa maficho ya Nduna Songea Mbano wakati wa Vita ya Majimaji.

Vyote hivi vimekuwa vivutio vya watalii wengi wa ndani na nje ya nchi. Kwa kauli hii ya Mkuu wa Wilaya @julius_mtatiro na OCD ni kwamba huko TUNDURU -Ruvuma hali sio shwari kuna UGAIDI ni tangazo na hali ya hatari kwa watalii kwamba hawapaswi kwenda huko.

Serikali ituambie UGAIDI huu huko TUNDURU hali ipoje, usalama wa watu upoje nini chanzo cha UGAIDI huu.

Abdul Nondo.
IMG_20221004_073244_623.jpg
 
Nondo you wewe na chama chako ni viumbe wa jabu let me put it that way! Nyinyi si washirika wa ukandamizaji huu? eti SUK... rubbish. achana na mavi hayo pigania demokrasi ufanye ziara bila ujinga wa OCD! Badala ya kukomalia Samia aondoe ukandamizaji huu, mnapingana na chadema badala ya ku join hands katika strugle hii! Unaandika nini sasa badala ya kuungana na wapigania demokrasia kukataa ushenzi kama huu! Rubbish!
 
Naona polisi wamejichanganya kwa kudhani wanawakomoa watoto wa washirika wao kufanya mikutano yao, kumbe wanatuchonganisha nje kwa kuwatisha watalii wanaotaka kuja kutembelea Tanzania, polisi kwa ujinga wao wanasababisha serikali wanayoilinda waipendayo ipoteze mapato.
 
Wilaya ya Tunduru ni miongoni mwa wilaya sita (6) za Mkoa wa Ruvuma. Wilaya ya Tunduru ina majimbo mawili Tunduru Kusini na Tunduru Kaskazini...
Wewe ndiyo u awatangazia watalii. Uliambiwa kama Mtanzania na mzalendo kuwa kuna tishio la ugaidi ulitakiwa utunze siri, sasa hawo magaidi umewatangazia kuwa siri yao imefichuka. Hivi wewe hujui kama kuna ugaidi? Huwajui UAMSHO?
 

Tunawabana bana wapinzani kufanya siasa kwasababu tuna chama chenye viongozi wenye uwezo mdogo wa kufanya siasa za hoja.

Wakati wa JK vyama viliachwa vikafanya siasa zao kwasababu CCM ilikuwa na viongozi wenye uwezo mkubwa wa kufanya siasa za hoja. Kuanzia Mwenyekiti wa chama Taifa,Katibu mkuu hadi mtu wa Uenezi walikuwa wanajua kujibizana kwa hoja.
 
Nondo you wewe na chama chako ni viumbe wa jabu let me put it that way! Nyinyi si washirika wa ukandamizaji huu? eti SUK... rubbish. achana na mavi hayo pigania demokrasi ufanye ziara bila ujinga wa OCD! Badala ya kukomalia Samia aondoe ukandamizaji huu, mnapingana na chadema badala ya ku join hands katika strugle hii! Unaandika nini sasa badala ya kuungana na wapigania demokrasia kukataa ushenzi kama huu! Rubbish!
Kaka tunafanya kazi kubwa sana chama na viongozi kuhakikisha Demokrasia yetu nchini ina imarika na hili tupo pamoja na kila mtu anayetaka reforms ktk nchi yetu ili kuwa na Demokrasia imara.
 
Wewe ndiyo u awatangazia watalii. Uliambiwa kama Mtanzania na mzalendo kuwa kuna tishio la ugaidi ulitakiwa utunze siri, sasa hawo magaidi umewatangazia kuwa siri yao imefichuka. Hivi wewe hujui kama kuna ugaidi? Huwajui UAMSHO?
Wao wameandika kwenye Barua hii na wao ndio wameisambaza kwamba kuna Ugaidi,na pia wananchi lazima waambiwe ili hatua stahiki zichukuliwe.
 
Madhara ya kutangaza SEHEMU FULANI ya nchi yetu kuna ugaidi ni makubwa mno kuliko mikutano ya hadhara ya vyama vya upinzani!!
Wapinzani ni NDUGU zetu KWANINI tuwaogope Hadi tufikie HUKO!!?

Washauri wa mamlaka husika wasiwashauri vibaya wateule wa Rais!

Mungu ibariki NCHI yangu Tanzania!
 
Yaani Mtatiro alikuwa analalamika walivyokuwa wanafanyiwa na POLICCM naye leo amekuwa upande wao kukandamiza vyama vya upinzani analama asali kimya kimya.
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom